Friday, April 8, 2011

Safari ya Dunia nzima kutoka Uhuru kwenda Utumwani


      *Huu ni Mpango wa Freemasons na Ibilisi
     *Dunia kuwa na mtawala mmoja,Fedha moja, Dini Moja na soko la pamoja(Common Market)

  MWAKA 1973, ilichorwa katuni moja matata ikimwonesha Mwarabu akiwa amewaweka chini ya ulinzi  viongozi wakuu wa mataifa mababe sana hapa duniani,kwa pampu ya mafuta.
   Katika katuni hiyo, Kansela Willy Brandt wa Ujerumani Magharibi (zama hizo), Georges Pompidou wa Ufaransa, Waziri Mkuu Edward Heath wa Uingereza na Richard Milhous Nixon wa Marekani, katika katuni hiyo walikuwa mbaroni na mafuta ya Waarabu,hadi hapo nchi zao zingelipa fedha za kuwakomboa ili waachiliwe huru.
  Wakati huo, kwa sababu ya Ulimwengu wa Kiarabu kuwa na nguvu za kiuchumi kutokana na mafuta yao, waliweza kuyaburuza mataifa ya Magharibi katika uchumi,katika siasa kufuatia ‘silaha’ hiyo ya mafuta.
 Naam, miaka ya 70 mafuta yalikuwa ‘silaha’ madhubuti ya nchi za Waarabu katika masoko ya Dunia na katika siasa za kimataifa.
 Mataifa makubwa yenye viwanda, yalihaha kutafuta mafuta kwa ajili ya kuendeshea viwanda vyao na kusafirishia bidhaa zao kwenda na kutoka nchi zingine.
 Ni kwa sababu ya mafuta, mataifa ya Mashariki ya Kati, Amerika Kusini, Afrika na kwingine kwenye mafuta,kumekuwa Hamkani si shwari, kwa sababu ya mataifa haya kutokwa udenda kwa nishati hiyo muhimu sana   kiuchumi.
   Nchi masikini, kama Tanzania hulazimika kuugua kiharusi cha uchumi,mafuta yanapopanda bei kufuatia vita katika Mashariki ya Kati.
 Bei maradufu zinapanda katika soko la dunia.
 Kwa sababu hiyo,kupanda kwa bei ya mafuta hutuletea sisi mfumuko wa bei usiosemeka. Maisha huwa magumu,na twalemewa na mzigo wa madeni na hivyo kulifanya taifa kuwa tegemezi kwa Marekani, Ulaya na washirika wao.
   Mafuta huchimbwa mengi Saudi Arabia, Irak,Iran, Kuwait,Libya, Abu Dhabi, Algeria,Russia, Marekani, Venezuela, Nigeria, Indonesia, Mexico, Ecuador, Norway n.k
  Marekani, Uingereza, Italia na Ufaransa wana makampuni makubwa ya mafuta, na wanaongoza duniani kuhitaji mafuta mengi ili kuendeshea viwanda vyao na mitambo yao na kusafirishia bidhaa zao na malighafi zao.
 Kila wakati, mataifa haya yanatafuta kujinasua katika  ‘umateka’ wa mafuta hususan kutoka Mataifa ya Kiarabu,ambayo kwa pamoja humiliki soko la mafuta duniani.
 Kwa sababu ya undumilakuwili,siku hizi Waarabu wanageuka mateka kwa Marekani na washirika wake, wanaachilia mafuta mikononi mwa Marekani na washirika wao na makampuni yao makubwa kama British Petroleum, Elf, Exxon, Conoco, Phillips, Chevron, Total, Royal/Dutch Shell n.k
 Urusi, Marekani na Uingereza wanamiliki zaidi ya asilimia 23 ya mafuta yanayozalishwa Ulimwenguni.
 Hata hivyo, mafuta hayo hayawatoshi,kulingana na mahitaji makubwa ya viwanda na mitambo yao. Hutegemea kuagiza mafuta kwa zaidi ya asilimia 30 toka nje.
 Nigeria, Venezuela,Mexico, Ecuador,Uchina, Norway na mataifa mengine ya Afrika kama Sudan, Guinea ya Ikweta, Angola na Misri, mafuta yao yanagombaniwa na makampuni haya makubwa ya Magharibi.
 Nataka kusema kwamba, mafuta ni bidhaa adhimu mno, ni silaha na chimbuko la migogoro,maandamano na vita. Mafuta huwasha taa katika nyumba zetu,na wakati mwingine tunapika chakula chetu kwa mafuta,lakini huwasha miali ya moto wa vita na machafuko hususan Mashariki ya Kati, Angola, Sudan Kusini,Nigeria na sasa Libya n.k
 Mataifa haya ya kikoloni, huzivamia nchi zenye mafuta kwa visingizio tele, na wakati mwingine wanapindua serikali inayowanyima mafuta ili kumsimika kibaraka wao atakayelinda maslahi yao.
 Marekani, Ufaransa, Uingereza, Italia n.k hawana rafiki wa kudumu. Wana maslahi ya kudumu.Wanapotokwa udenda na maliasili ya mtu; mafuta,almasi, gesi au Uranium,wanatafuta kuchochea machafuko ili wapate nafasi ya kupenya na kukamata mahali rasilimali hiyo ilipo-ndiyo maana leo Libya wamewapa Waasi silaha ili wakamate visima vya mafuta kwanza,ili biashara haramu ya “Silaha kwa Mafuta”( Guns For Oil) ianze!
 Tena huzitokea udenda bahari za watu, maziwa,mito, mifereji kama Suez na Panama Canal huko Panama.
 Ni kwa sababu hiyo, Marekani hutafuta vibaraka katika nchi za mafuta kama Iran zama za Mfalme Shah,kabla hajafurushwa na Ayatollah Khomeini.
  Waandamanaji vijana(wamachinga) mwaka 1978 waliandamana mitaani hadi Shah akakimbia nchi,mfano wa alivyokimbia Ben Ali na Hosni Mubarak huko Tunisia na Misri.
  Shah, alikuwa ametawala Iran kwa miaka 37, na akakaribia kuiuza nchi kwa Wamarekani na    washirika wake wenye viwanda,kwa ahadi eti kuisaidia Iran kuwa, “Westernized Industrial State”.
   Waislam wenye msimamo mkali wa Kikomunisti, wakaungana ili kumpindua Shah, akatimkia Mexico, baadaye akaenda Marekani ili kutibiwa saratani.
 Ukomunisti ulishatoweka, umebaki Uislam wenye msimamo mkali kama walionao akina Mahmoud Ahmadnejad wa Iran.
 Wafuasi wa Ayatollah Khomeini walitaka   Shah arejeshwe Iran ili akashitakiwe kwa kuua raia na kuiweka rehani nchi kwa Wazungu.
 Machi mwaka 1979 Iran ilijiita nchi ya  Taifa la Kwanza Duniani kuunda ‘SERIKALI YA KWANZA YA MUNGU DUNIANI’ baada ya Shah kurejea nchini humo akitokea uhamishoni, Paris, Ufaransa.
 Nataka msomaji atazame uhusiano wa Iran na mataifa ya Magharibi yakiongozwa na Marekani kuanzia zama za Shah na baadaye Ayatollah Khomeini, hata sasa anapotawala Mujaheddin, Mahmoud Ahmadnejad.
 Tutazame pia ugomvi wa Israeli na Misri. Kwamba, Juni 6 mwaka 1973 vikosi vya Misri vilipenya Mfereji wa Suez na kuishambulia vikali Israeli.
   Ulikuwa wakati wa Sikukuu ya Kiyahudi inayoitwa, Yom Kippur, wakati Waarabu wa Misri na Syria wakisadiwa na zana nzito za Kirusi;vifaru 2,600 vya Misri na 2000 vya Syria viliwazidi nguvu Israeli waliokuwa na vifaru 1,700 tu,wakapigwa kweli kweli.
 Naam, nazungumzia Vita vya Siku Sita, Israeli ilishachakazwa sana,Waziri Mkuu wa Israeli, Bibi Golda Meir akaomba msaada Marekani, Rais Richard Nixon akampa ndege 80 za vita na vifaa vingine kwa ujumla wake vilikuwa na uzito wa tani 22,000.
 Nataka kusema kwamba, Marekani ilishaungana na ‘Uzayoni’ kupambana na Waarabu wenye mafuta, ambao pia ni Waislam.
 Mikataba ya amani kama ile ya Camp David mwaka 1978 haina maana kubwa kwa kuwa vita vingalipo Libya, Yemen,Misri na hata Iran inatafutwa kwa kuhisiwa inarutubisha Uranium kwa ajili ya nyuklia.
 Siasa za Mahariki ya Kati ni siasa za mafuta, yaani “Middle East Oil Politics” na visingizio vya mabeberu kumbe ni vingi kwamba Waarabu ni magaidi na wanaunga mkono ugaidi,kumbe na Marekani na mashirika ya ujasusi kama        CIA, Mossad n.k NI MAGAIDI!
 Mwaka juzi, Shirika la Atomiki( International Atomic Energy Agency) lilisema Iran ilikuwa na kilo 630 za Uranium iliyorutubishwa tayari, wakati Misri na Uturuki wanatamani kurutubisha Uranium ili nao watengeneze mabomu ya Nyuklia.
 Sasa, unaweza kuona kwamba Waziri wa Ulinzi Robert Gates, anafanya njama kuzitoa kamasi nchi hizi kwa mapinduzi ya Wamachinga, mashambulizi ya madege ya kijeshi n.k
   Lazima WAARABU wabanwe mbavu, wasiweze kuungana na kujinasua. Marekani lazima iwaweke vibaraka wake huko kwa maslahi mapya,kama ilivyotokea kwa akina Anwar Sadat, Hosni Mubara huko Misri,na Mobutu Sseseseko huko Zaire, Shah wa Iran n.k
 Zamani, mabepari walitishwa sana na UKOMUNISTI, siku hizi wanatishwa sana na misimamo mikali ya kidini kama Uislam na watu kutaka kujikomboa na kujitegemeza wenyewe kwa fursa zao, ili kuunda umoja wenye lengo la kujikomboa kiuchumi,kisiasa na kidini.
 Hili ndilo lililokuwa kosa la Kwame Nkrumah wa Ghana, Patrice Emery Lumumba wa Congo,na ndilo kosa kubwa la Kanali Mouammar al-Gaddafi wa Libya,kutaka mataifa yote ya Afrika yaunde dola moja la Afrika, UNITED STATES OF AFRICA.
 Yaani, Gaddafi alitaka Waarabu na Weusi wawe pamoja, wakopeshane pamoja,wafanye biashara pamoja, wawe na utamaduni moja pengine na dini tofauti na Magharibi…
Wanaweza kuwa na miungu yao ya asili na kutengeneza madhabahu huku Afrika na Asia,halafu….
 Namcha Mungu mmoja aliyeenea Marekani hadi Ulaya na Asia. Lakini Mungu anathamini uhuru na uchaguzi wa kila mtu, Afrika yenye mafuta, almasi na dhahabu,uranium na mifereji kama Suez ingeweza kujikomboa kwa rasilimali hizi, na Mungu hufurahi kuona Waafrika wakiwa matajiri, siyo Wazungu tu.
   Mungu hajawahi kukataa Waafrika na Waarabu kuwa taifa kubwa(Super power)tena taifa huru bila ukiritimba wa makampuni ya Wazungu.
 Ni kwa sababu hii,tunapaswa kung’amua kwamba Marekani ambayo Biblia katika Ufunuo wa Yohana 13:11-18 inafananishwa na Mnyama(serikali nyingi duniani alama zao ni wanyama na ndege) mfano wa kondoo mtoto mwenye uhuru wa dini na demokrasia, sasa anamwasi Mungu na kutaka kuwalazimisha watu wa dunia nzima,kuwa na dini moja, itikadi moja ya kisiasa,soko la pamoja(Common Market), Fedha  moja n.k
 Wanataka kukamata uchumi wa dunia nzima, kuwafanya watu wote duniani kuwa watumwa wake,bahari ziwe zake, mifereji yote,maziwa na mito,madini yote,mafuta yote n.k yawe mikononi mwake, na anayempinga apigwe na madege au awekewe vikwazo vya kiuchumi!
 Watawala wote wanaoipinga Marekani, akina Hugo Chavez, Robert Mugabe, Gaddafi, Fidel Alejandro Castro Ruz wa Cuba, Ahmadnejad wa Iran n.k wakamatwe na kufungwa jela, wauawe au wawekewe vikwazo vya uchumi, na raia wao nao wafungwe jela mpaka wakubali kusalim amri!
 Marekani, wanataka watu wote wawe na imani moja,itikadi moja Uyahudi, Uislam,Ubudha,Ukristo usigawanyike,uwe dini moja! Upagani nao ugeuzwe kuwa katika dini ya aina yake,kwa ahadi kuwa dunianzima iwe “Westernized Industrial State”.
 Hizo ni njama za Ibilisi na Freemasons kuwafanya watu wote duniani kuamini na kutekeleza matakwa ya matajiri wa Ulaya Magharibi na Freemasonry.
 Iran walipotaka Shah kurejeshwa Iran ili ashitakiwe, Rais James Carter akakataa, akatangaza vikwazo vya uchumi kwa Iran wasiuze tena mafuta yao Ulaya!
 Kumbe hii silaha ya vikwazo vya uchumi-tusiuze wala kununua tena- ni silaha ya kuwakomesha watu wanaokaidi Marekani na Washirika wake, Ma Free mason na Ibilisi!
 Ukitazama Ufunuo wa Yohana 13:17 UTAONA vikwazo vya kiuchumi vitatumiwa na Marekani kuwalazimisha watu wote duniani kuamini dini moja,itikadi moja,soko la pamoja,utamaduni mmoja n.k
 Na kwa sheria hii ya Marekani, watu wanaabudu dini moja, mfumo mmoja wa biashara,uchumi na maisha.
 Marekani yenye uhuru wa dini(Religious Liberty) na uhuru wa kisiasa,imeshaasi Nguzo zake mbili,imegeuka mnyama anayesema kwa niaba ya Ibilisi na maFreemasons.
    Hii nguvu ya Marekani ya dini na siasa (Religio-Political Power) inaunda alama yake ya mamlaka(The Great Seal) ili sote tuiogope na kuisujudu(Ufunuo 13:15-17) hii ni alama ya Freemasons na Ibilisi na washirika wake dhidi ya wale wote wanaotaka kuipinga!
   0786/0754-324 074


No comments:

Post a Comment