Tuesday, December 13, 2011

UTATU MTAKATIFU WA FREEMASONS,SHETANI NA DINI

SEPTEMBA  mwaka huu,nilikuwa miongoni mwa waandishi wa habari waliohudhuria mafunzo ya kuongeza uelewa wa kupinga  unyanyapaa, “Anti Stigma Awareness”.
Tukajifunza kwamba, unyanyapaa ni mbaya; ni chimbuko la majanga makubwa kitaifa na kimataifa, na kwamba aslani, hakuna unyanyapaa chanya duniani.
Hata hivyo, nikajikuta nikibishana mno na Mwalimu juu ya Jamii za Kiafrika kuachana na  UNYANYAPAA juu ya wanaume wanaoingiliwa kimwili,yaani mashoga ama wanawake wanaowaoa wanawake wenzao, wasagaji.
Tulifundishwa kwamba, unyanyapaa hata dhidi ya mashoga ni ukatili, ni kinyume cha ‘Haki za Binadamu’ ni ubaguzi,ni kutenga watu ni udhalilishaji.
 Kwamba, Afrika,imeshindwa kushughulikia watoto waishio mazingira hatarishi, imeshindwa kupambana na umasikini,ufisadi na utawala mbovu, inakazania kunyanyapaa watu wa ndoa za Jinsia Moja-Mashoga na Wasagaji!
 Naam, hii ndiyo Sauti ya Marekani,Ulaya na NGO zetu na Wanaharakati wa Haki za Binadamu. Bado kitambo kidogo, hata vyama vya siasa vitakuwa na sera hizi ili vipate kuungwa mkono na Mabwana wakubwa wa Magharibi.
Ni kwa sababu hii, msomaji ajue, Marekani na Ulaya wameamka ili watufundishe sisi Waafrika kubadili mtazamo wetu ili tusiwanyanyapae mashoga!
Katika mafunzo haya(siwaambii yaliwezeshwa na mashirika gani) tukafundishwa wimbo ufuatao:
“Unyanyapaa,kejeli,viboko,dharau na manyanyaso dhidi ya watoto na Jamii ya mashoga ni janga-unyanyapaa tuulete,tuuchane-chane,tuutupe!”
Ubeti wa Pili tuliuimba hivi:
 “Watoto wetu(wakiwa mashoga) vipaji vyao,busara zao,hekima zao-tuwalete,tuwakumbatie tuwabusu!”
Hakika, huu ndiyo mtazamo wa Bara la Ulaya na Marekani katika kuwashughulikia vijana wetu wanaojiingiza katika  usagaji na ushoga. Kwa Wazungu, ushoga siyo janga(janga ni watoto wa mitaani)ushoga ni uhuru zaidi na maamuzi ya mtu mwenyewe-hakuna  kubeza na kuhukumu!
Katika Unabii wa Biblia, katika Ufunuo wa Yohana 16:13 kumetabiriwa ‘Roho Tatu za Uchafu’(Utatu Mtakatifu wa Uovu) za vyura, zinapotoka kinywani mwa Shetani,Mamlaka kuu za Dunia na Muungano wa Dini na Serikali za Dunia.
Kumbe Biblia inatabiri kwamba mambo haya yatatoka katika kinywa cha Mamlaka za Dunia zitakapoungana na Mamlaka za Madhehebu ya Dini, ambayo ni pamoja na Umizimu, Teknolojia na ukisasa utakaokwenda kuandaa ‘Vita vya kiroho’ vya Har Magedon.
   Roho Tatu mfano wa vyura,maana yake nini?
Chura, ni alama ya uchafu. Katika Misri ya kale,chura alikuwa nembo ya mungu mke,Heget, aliyeaminiwa kwamba alikuwa chimbuko la uhai kwa watoto wanaozaliwa-nguvu kwa vijana.
Huu Utatu Mtakatifu wenye sura ya chura(Evil Trio) umevaa umizimu wa kisasa,uasi wa kidini, na hali ya vijana kuona DHAMB( uasi wa sheria za Mungu) kama kitu cha kawaida tu.
Leo, vijana wengi wakifanya makongamano,hujiuliza,”Hivi Mungu yupo kweli?”
Ndivyo alivyouliza Farao wa Misri zama zile za Nabii Musa, kama miaka 1500 BC.
Vijana wanataka kuwa huru kutoka hofu ya kuwapo kwa Mungu; wanakusudia kuishi huru, na wanamwona Mungu na sheria zake Dikteta-vijana wanataka haki zaidi katika kufanya mambo yao.Ndivyo zilivyokuwa siku za Nuhu na Loti.
Mila na desturi nyingi za Afrika zinakinzana na vijana wa kileo wa kizazi hiki cha ‘dot com’ katika zama za utandawazi za karne hii.
Mila na desturi za Afrika,zingali zikiheshimu sana ndoa ya Jinsia tofauti(heterosexual couples).
Ndoa kati ya mume na mke, ndiyo mwanzo wa familia bora na imara iliyoasisiwa na Mungu katika Bustani ya Edeni, kadiri ya miaka 4004 BC.
Roho Tatu za vyura zinapinga kwa dhati uhalali wa ndoa za Jinsia Tofauti pekee. Roho hii inayotoka mdomoni mwa watawala wa dunia walioungana na Freemasons na teknolojia, wanataka kuwe na ushoga, usagaji, ndoa za mikataba, useja wa kudumu maishani,kuasili(adopt) watoto, ama kupata watoto kwa njia ya maabara (test-tube babies); na hata binadamu kutengenezwa katika maabara,yaani human cloning.
Maisha ni magumu, Haki za Binadamu hizi zinawapigia debe wanaume na wanawake kufanya biashara ya ngono(Commercial Sex Work) ili kujipatia kipato.
 Ndiyo maana, ukienda katika vilabu vya usiku na madanguroni utawakuta wasichana wetu “Dada Poa” wakijidaki ili wapate ujira. Wanashindana na makaka poa(mashoga) katika biashara hii, inayopingwa huku wakati imehalalishwa tayari na Wazungu,Mashirika yao na NGO na wanaharakati wa huku kwetu.
Kwa sababu lipo wimbi kubwa la watu kuhamia mijini(Urbanization) huu Utatu Mtakatifu wa vyura utawakuta vijana wengi wanaohama vijijini kwenda mijini,wakiwa waongufu wapya. Maadili ya Muafrika yataondoka na Wazee ambao sasa wana miaka kuanzia 55 na kuendelea na ni wachache tu.
 Afrika,kuna vijana wengi na watoto kuliko hawa watu wazima wanaojidai kupinga ushoga na mmomonyoko  wa maadili siku hizi.
Vijana, kupata watoto waliozalishwa katika maabara kama Marehemu Michael Jackson, hapo sawa. Kwanza ,wasichana na wavulana hawataki watoto-wanawatupa kwenye madampo.Heri wabebe midoli  hata ya ‘dogi’na kutembea nayo mitaani.
 Sasa, nani atalea watoto na maisha haya magumu? Hata kilimo sasa hatutaki,tutakula mchele wa maabara. Ni kuongea na simu na kutazama ngono mtandaoni,kusikiliza muziki kwenye simu, asubuhi hata jioni.
Hata  wasichana wakizaa hawataki kuwanyonyesha  watoto ziwa la mama, wasije kuzeeka bure na kukosa starehe.Wengine wanawatupa chooni ama dampo kwenye mifuko ya Rambo! Nani alee, sasa?
Vijana wanachelea kuwa wazee, wanakazana hata kumeza vidonge wasizeeke, na wazee wengine wanameza dawa za kuwarejesha ujanani-Afrika uzee sasa ni janga kuliko Ukimwi! Hawataki kukonda, wananunua dawa za Ki-China.
Wasichana wakizaa kabla ya ndoa, hawanyonyeshi watoto titi la mama.Wengi wao wameingia katika ndoa za mikataba,kwa sababu wanasema ndoa siku hizi ni utumwa. Nani aolewe? Kuoa ama kuolewa eti ni utumwa, sababu ni uchumi wa dunia kuwa mgumu. Hata kuosha vyombo ni utumwa.
He! Mwe!! Msichana mrembo aache kujipamba na kwenda kujiuza mitaani apate maisha, eti aolewe? Ndiyo maana ndoa inafungwa saa sita mchana, inavunjika saa 12, jioni saa za kwenda Villa Park!!
Ndoa ni ndoano.
Hata walioko kwenye ndoa nao wanakwenda kujiuza katika  ‘Viwanja vya Fisi’ kwa sababu maisha siku hizi ni magumu. Ndoa ni utumwa siku hizi kwa watoto wa siku hizi.
 Wanaharakati wanatufundisha kwamba Baba  ‘Siku hizi’ hana watoto, hawa ni watoto wetu!
Naam, vijana wetu hawa tunaowaita “wa Siku Hizi” wanatafuta maisha namna hii kwa sababu wazee wameng’ang’ania ajira, wanafanya ufisadi na kuhujumu uchumi ;sasa ‘Kaka-Poa’ na ‘Dada-Poa’ ni wasomi hasa wa vyuo vikuu, na wanafanya umalaya wa mtandaoni kupitia simu za mikononi ,zenye internet kama Broad band, sijui Twitter, Face book n.k
Hata watoto wa kiume wanatamani kubadili jinsi zao za kiume ili wawe wake(Trans Gender) ili ,wajiuze na kufaidi maisha. Akina mama nao wanajibadili jinsi ili wawe waume waoe na kuolewa kwa pamoja! Wamiliki jinsi mbili tofauti,“Two in One” Ili akipatikana  sugar mammy au sugar daddy, sawa. Kaka Poa au Dada poa, ni poa tu.
 Hizi ndizo sera za akina David Cameron na Barack Obama, kama mtu anapinga atanyimwa msaada! Kawaulize wenye NGO kama hawatachangamkia ‘deal’ hii ya kutetea  ‘Haki hizi za Binadamu za mashoga?
 Hili niliache, wasije kunitoa nyongo bure.Tumempinga David Cameron juu juu tu.
Thomas Beatie(37) ni :Dume-Jike” ,Mmarekani, aliyezaliwa Hawaii mwaka 1974 akaitwa Tracy Logondino.
Alipofikisha umri wa miaka 20 akadungwa sindano zenye hormone za kiume(testosterone Injections) ili awe na nywele za kiume tabia ya kiume na sauti nzito.
Mwaka 2002, alifanyiwa operesheni ya kuondolewa matiti(Mastectomy) kwa sababu alitamani kuwa mwanamume. Aliwekewa uume; lakini uke wake haukuondolewa mwilini mwake. Alioa mwanamke aitwaye Nancy, akazaa naye watoto; Susan, Austina na Jensen.
Beatie, akawa ‘Dume-Jike’ ingawa matiti yalishaondolewa kifuani pake. Nataka kusema kwamba, ingawa alioa mke,Nancy, alikuwa pia mke aliyefanya tendo la ndoa na mwanaume mwingine! Yaani alikuwa mume na mke kwa pamoja!! Hii ndiyo Marekani sasa.
Jamaa huyu sasa amepata ujauzito, anakaribia kujifungua mtoto. Licha ya kuwa baba wa hao watoto watatu: Susan, Austin na Jensen, sasa atajifungua mtoto wa baba mwingine- atakuwa Baba na Mama kwa mpigo!!
Anaishi Arizona, na akijifungua anasema ataondolewa kizazi. Mkewe naye alishaondolewa kizazi- hysterectomy!
Sasa, atakapoondolewa kizazi, anasema atakuwa “Dume la Mbegu” maana anapopata ujauzito basi hormone za kiume huacha kufanya kazi ili kumpa fursa mtoto aliye tumboni kuwa na afya njema. Shaabash!!
Nataka kusema kwamba, Barack Obama , David Cameron, Mashirika yao ya misaada na NGO ZETU(ZIKIWEMO ZA MFUKONI) wanaingia vitani kufanya semina ili sote tubadili “Mind sets” kuuinamia ushoga, usagaji,kubadili jinsi(transgender) n.k
Hakuna noma, eti?! Basi, Poa kaka, lakini siyo wewe kaka poa..
Roho Tatu za vyura zinahamasisha uchafu huu, miujiza ikiwemo ya kisayansi na kishetani, ishara, maajabu, ibada bandia,utajiri wa haraka,picha za uchi(pornography)ngono za mtandaoni, sinema chafu,hadithi za ngono, magazeti ya ngono-ngono,vijarida vya uchi-uchi,kutembea uchi,vivazi vya ajabu vya nusu uchi,miziki ya ngono-ngono ya siku hizi,mitindo ya kidunia n.k
Makanisa na misikitini hawako salama. Madawa ya kulevya,ulawiti,ufisadi na uchafu,madawa ya kulevya yako huko. Rais Kikwete aliposema kuna madawa ya kulevya makanisani na misikitini, watu wakabisha, kumbe ndiyo biashara yao ya siku nyingi, na wametajirika kimiujiza.
Hata makanisani siku hizi, kuna ma-Disko kuliko vilabu vya usiku.
 Eti “disko la Yesu”… Yesu ana disko? Anapigia ukumbi gani nyie? Kuongea na wafu(spiritualism) miujiza ,ya uponyaji kwa fedha ni nini kama siyo nguvu ya  Freemasons, mizimu na dini bandia hizi?
Misikiti inayumba,makanisa yanapoyumba.Maaskofu na makasisi ni walawiti,hata Baba Mtakatifu, Benedicto XIV anaomba radhi kila siku. Viongozi wa dini wanamwaga damu kama Kibwetere wa Kanungu,Uganda. Niliandika siku chache zilizopita juu ya Yunus Santy, kasisi toka Italia kuwabaka wasichana wa shule Mwanza, serikali ikagwaya  kumfunga miaka 30 jela.
Roho Tatu za Vyura huhamasisha uhuru na Haki za Binadamu zaidi na kumwona Mungu ‘Jambazi sugu’ na Dikteta. Laiti wangejua Mungu anakaa mtaa gani,leo wangekwisha mshitaki The Hague,Uholanzi, kwa kosa la kutishia kuleta kiama duniani, siku ya mwisho.
Watu wanageukia teknolojia kuwa mungu wao, aliye muumbaji wa wanyama,watu na mimea bandia.’Thiories’ kama uibukaji, evolution huondoa hofu kwamba kuna Mungu, sasa wanaume nao wanapata mimba?Wanawake nao wanaoa!
Hata hivyo, najua kuna watu wana NGO za kupinga unyanyapaa dhidi ya wanaume watakaoolewa na wanaume wenzao,wanawake watakaoolewa na wenzao na wanaobadili jinsi zao,ili waoe au kuolewa, machangudoa,kaka poa n.k
Haki za Binadamu wanatwambia ,TUSIWANYANYAPAE! Hili ndilotangazo la Desemba 10 mwaka 1948.
Mtu mmoja hunisumbua  sana nimwambie namba za simu za Freemasons; mimi siwajui Freemason na simo. Mimi ni maskini;sina kitu.
 Bila shaka, hawa nia yao ni kupata utajiri wa haraka,  katika fahamu zao walisha mkataa Mungu, Mungu wao ni tumbo.
 Hii ndiyo Injili Mpya ya Utatu Mtakatifu(Evil Trio)  iliyopata kibali Marekani na Uingereza, na mtu akiikubali anapewa msaada, ama analipwa utajiri. Wapo wengi wanaopenda utajiri wa namna hii; wasinisumbue. Mimi sijui Freemasons wanaishi nyumba namba ngapi?
Mtaa gani…sijui!! Na huyo  ‘Jike-Dume’ simjui, msisumbuke kuniuliza!! Alamsik.
0754/0786-324 074





1 comment:

  1. i want to share my testimony of how i become rich and famous today… i was deeply strangled up by poverty and i had no body to help me, and also i search for help from different corners but to no avail… i see people around me getting rich but to me i was so ashamed of my self so i met a man on my way he was very rich and he was a doctor so he told me something and i think over it though out the day so the next day i looked up and i keep repeating what he said to me. ” if you want to get rich quick and be famous” you need to cross your heart and do what is in your mind so i tried all i could in other for me to do as he said so later on i told my fellow friend about this same thing then my friend was interested in my suggestions so i decided to look in the internet and i found their number so we decided to contact them and unfortunately we did as they instruct us to do and later they told us to get some requirements and all the rest… so this initiation took us just a week and later on the great fraternity gave us $1,200,000 to start up our lives…. and now am testifying that if in any case you want to join any great fraternity all you need to do is for you to contact them because they are legitimate and they do as what they instructed them to do, so you can as well WhatsApp me +2348106618681 or for more information +1(705)8062021 you can Email: illuminatipowerful666@gmail. com...

    ReplyDelete