Tuesday, April 16, 2013

Waliowaua J.F Kennedy na Abraham Lincoln wamefika Tanzania




FUJO ZA KIDINI na kisiasa hapa nchini,hazitokei kwa nasibu,kama inavyodhaniwa, zimekusudiwa.
Ni ishara kwamba,sasa Tanzania imevamiwa na mamluki wa kimataifa,ambao kazi yao ni kuifanya Dunia Hamkani si shwari.
John Fitzgerald Kennedy (1961-63),alikuwa Rais wa 35 wa Marekani,kupitia chama tawala siku hizi cha Democrat.
Alizaliwa Mei 29 mwaka 1917 huko Brookline, kwa baba aitwaye Joseph P. na mama Rose Fitzgerald Kennedy.
Alihitimu Chuo kikuu cha Harvard,mwaka 1940,akaenda jeshini(1941-45),alichaguliwa Seneta 1952 na 1958.
Aliteuliwa kugombea Urais mwaka 1960, akajakumshinda aliyekuwa Makamu wa Rais kupitia Republican, Richard Millhouse Nixon, ambaye baadaye alikuwa Rais akaja kukumbwa na kashfa ya Watergate-1973/74.
“J.F’Kennedy,kama alivyoitwa na rafiki zake, ‘J.F’ alikuwa MPIGANIA HAKI ZA RAIA akaongeza huduma za afya kwa raia hususan wazee,uchaguzi na akaongeza fedha kwenye miradi ya uchunguzi wa anga za juu.
Novemba 22 mwaka 1963,Kennedy aliuliwa akiwa katika msafara wake Dallas,Texas.Ilikuwa saa 6.30 hivi mchana, raia wengi wakimshamnilia rais huyu,msafara wake ulipokuwa ukipita mjini humo.
Ghafla, risasi zikarindima;baadaye rais alishapigwa risasi na majahili;mwili wake ukawa  umelazwa Parkland Memorial Hospital-alikuwa marehemu tayari.
Ilikuwa Ijimaa, “The Black Friday”,   Novemba 22,mwaka 19063 gari la rais lilipopigwa risasi hapo ‘Deadly Plaza’.
Watu walitaharuki,ikaundwa Tume ya  uchunguzi, The Warren Commission, ikabaini eti    Lee Harvey ndiye alimpiga risasi Kennedy. Nataka nikwambie msomaji; Tume za Uchunguzi za vifo vya watu maarufu,aghalabu ni geresha tupu! Angalia Tume ya uchunguzi wa kifo cha Princess Diana, The Paget Probe, na nyingine nyingi…ubatili mtupu!
Lee Oswald alisemwa kumpiga risasi Rais Kennedy huko Dallas;kwamba alimfyatulia risasi nyuma ya gari lake,jirani na Dallas Depository.
Siku mbili baada ya Oswald kumuua Kennedy,Jack Ruby akamuua Oswald ili kupotezea ushahidi, na kuvuruga kabisa uchunguzi.Unakumbuka vifo vingi wauaji nao huwa wanauliwa ili kupoteza ushahidi?
 Meja Kasereka aliuliwa mara baada ya kumuua Laurent Desire Kabila katika Ikulu ya mjini Kinshasa. Unakumbuka?
Sisi tunajua J.F Kennedy, aliuliwa kwa sababu ya kutaka kuondoa majeshi ya Marekani nchini Vietnam.
Wakubwa wa dunia hii waligharimia vita vya Vietnam hawakutaka majeshi haya yaondoke huko,walitaka vita viendelee kama leo vinavyoendelea Kongo,Somali na mahali pengine,ili wakubwa wapate wanachokitaka.
Hata sasa kuna kitisho cha vita Ghuba ya Korea,na Iran iko hatarini kushambuliwa ba muungano wa wakubwa wa dunia,baada ya uchaguzi wa Marekani kukamilika na rais kuapishwa Januari 20 mwaka huu.
Tanzania imekaa kisiwa cha amani muda mrefu,sasa inanyatiwa na hawa majahili. Kuna vurugu za kijinga na fujo za kidini za Wakristo kuchinja/kutochinja.
Nigeria zilishazoeleka.Vietnam,Marekani walipeleka jeshi ili kusimika dini ya Kikatoliki,kwa hiyo wakubwa wa dunia walipeleka jeshi huko ili kusimika dini hiyo kwa maslahi  yao.
Fujo    zinachochewa makanisani/misikitini siku hizi na serikali hizi za kutegemea misaada haziwezi kukomesha fujo hizo maana huchelea kukosana na wafadhili.
Migogoro ya kidini na ushenzi mwingi huchochewa toka nje ili nchi isitawalike, na wasiokubaliana na matakwa ya wakubwa washikishwe adabu.
 Hatuko huru,kama nilivyoandika katika makala ndefu ya AFRIKA KIZIMBANI.Rais Kennedy hakuona umuhimu wa vita vilivochochewa na ma Jesuits( secret Society) huko Vietnam.
Aliyesimamia njama za mauaji ya J.F Kennedy alikuwa kiongozi wa ngazi za juu wa MAFIA,kwa sababu,rais hakutaka vita vya Vietnam,akahimiza askari 500,000 wa Marekani kuondoka na kurejea nyumbani. Wapenda haki na mani huwa hawapendwi.
 Ilikisiwa, Shirika la Ujasusi la Marekani, Central Intelligence Agency (CIA) humilikiwa kwa kiasi kikubwa na Freemasons,na siyo serikali ya Marekani peke yake.
Kennedy, alikusudia kuifumua CIA mwaka 1953 kwa kuwa lilikuwa na njama za kuangamiza watu wa madhehebu Fulani ya dini.Madhehebu ya dini yenye waumini wengi au ambayo huhamasisha mambo yasiyotakiwa,hujikuta katika maangamizi na vita.
Fuatilia vita vya Matengenezo ya Kikristo(Christian Reformation) utaona watu takriban milioni 50 waliuliwa kote Ulaya,wengine wakatimkia uhamishoni,Marekani.
Nikurejeshe mjini Dallas hiyo Novemba 22. Kennedy alitabasamu kuona anapungiwa mikono na raia.
Rosselli, alipiga risasi ikapenya kisogoni na kusambaratisha ubongo wa Rais.Frantiano alipasua taya,Oswald alisambaratisha ubongo wa rais,Brading alimvinja bega.
Baadaye, walilipwa ujira wa mamilioni ya Dola.Hata hapa kwetu wapo wanaoishi kwa uchuuzi wa raia wenzao na ugaidi;na wanajidai watu wazuri sana na wamepewa vyeo vikubwa.
Kennedy, alitetea Uhuru wa Dini(Religious Liberty),kitu kinachowachefua sana wakubwa,ndiyo maana sasa wameshavuruga mshikamano wa Watanzania kwa silaha ya utengano wa kidini.
Kuna madhehebu ya siri hapa duniani kazi yao ni kuleta machafuko, Biblia katika Ufunuo 18:3 ilimkariri Bwana Mungu akiwataka watu kuondoka Babeli(machafuko).
Tumjadili kidogo, Abraham Lincoln.Watu humjua sana rais huyu wa Republican kwa kushindwa mara nyingi bila kukata tama.
Alizaliwa Feburuali 1 mwaka 1809 akaapishwa kuwa rais mwaka 1861 katika umri wa miaka 52. Ukipenda angalia tarehe hizo zina uhusiano gani na zile za historia ya Kennedy? Hata hivyo siyo somo langu leo.
Alikuwa rais wa 16 wa Marekani, alipinga sana utumwa na akatangaza watumwa kuwa huru.Aprili 14 mwaka 1865 Abraham Lincoln aliuliwa na muigizaji wa sinema,John Wilkes Booth,katika jumba la sinema, Ford’s Theater.   Ni mjini Washington DC. Rais Lincoln    alikufa keshoye Aprili 15.
Duniani kuna mlolongo wa vifo vya watu mashuhuri sana waliouliwa kwa risasi:
Tom Mboya(1968),Samora Machel(1986),Lumumba(1960),Anwar al Sadat(1985),Laurent Kabila(2001),Edward Moringe Sokoine(1984) n.k
Mwaka 1997,Waziri Mkuu wa Israeli, Yitzak Rabi, aliuliwa kwa risasi na askari wa MOSSAD(Shirika la Ujasusi la Israeli,mshirika mkuu wa CIA)kwa sababu alitaka sana uhuru wa dini,kuheshimu dini ya kila mtu.
Alitaka kuleta maelewana kati ya Waarabu na   Mayahudi mjini Jerusalem, akawakosea wenye dunia.
Nataka niseme kwamba hawa majahili wamesababisha mauaji mengi hapa duniani,sababu ni maslahi yao ya uchumi,siasa na dini zao za siri.
Nawashauri Watanzania kuwa macho na mawakala wa Freemasons ambao leo wako makanisani na misikiti na utawatambua kwa kuchochea vurugu na vita vya kidini na utengano.
Wanachotaka ni kuondoa amani ya nchi na kurejesha utumwa na dhuluma kupitia vita kama ilivyo Somali au Congo DRC.
Machafuko haya huletwa na mungu wao wa vita,Odin(ni baba wa Aesir,mungu wa vita,kifo na uchawi) nembo yake ni mkuki na mtu mwenye jicho moja!
https://encrypted-tbn2.gstatic.com/images?q=tbn:ANd9GcRLYP-B_vbH4dgAgXpwtf7lE3gZeSFK6K74dkXV6VnvvrH8tJ0mlwOdin     http://gallery.nen.gov.uk/assets/0610/0000/0000/odin4_mid.jpg
Sababu kuu za kuchochea vita ni “Depression”-a worldwide financial panic and economic depression” kuanguka kwa uchumi na kufilisika kwa masoko ya hisa,kufilisika makampuni makubwa ya Magharibi(International Bankruptcies) na ukosefu wa ajira kwa mabilioni ya watu duniani. UFISADI!
Wanataka mataifa yote duniani kujisalimisha miguuni mwao na atakayeleta jeuri atafanyiwa kama miji ya Japan ya Nagasaki na Hiroshima ilivyofanyiwa,kupigwa kwa mabomu ya Atomiki na kujisalimisha Septemba Pili, mwaka 1945.
Demokrasia inayoimbwa duniani iko njia panda.Tunajongea katika zama za uimra, ‘Totalitarianism”.
Akina Manuel Noriega wa Panama walikamatwa na CIA Januari 1990,kwa sababu walijitia kichwangumu kuukatalia mfereji wa Panama-Panama Canal.
Hizi ni zama za akina Kaisari Nero(54 AD) watakaojidai kukataa kutawaliwa watang’olewa kama Mfalme Theodoric wa Ostrogoths mwaka 476 AD(Tazama Daniel 7:24,25. Zama za giza hizi zinatawaliwa na matajiri haramu.
Hayati Edward Moringe Sokoine alikuwa mwiba mchungu kwa hawa mafisadi.Alitetea uhuru wa dini akauliwa na(Majesuit?) angekuwa Rais wa Tanzania baada ya Mwalimu Nyerere kustaafu.
Aliyesababisha kifo chake,Aprili 12 mwaka 1985,Dumisani Dube, akiwa Ukonga gherezani akapenyeza habari za kifo hiki (Newsweek, Mei 16 mwaka 1984)
Waandishi wa habari walipewa amri, ‘kalamu chini’ siri ya kifo ikabaki siri sirini! Ilisemwa,Sokoine alikufa kwa ajali.
Sokoine alikufa kama JF KENNEDY,Lincoln,Kabila,Sadat,Samora,Lumumba na wanamapinduzi wengine. Kosa lao lilikuwa kutetea haki,amani,uhuru wa dini,usawa na haki duniani.
Wanaoendesha uchochezi na vurugu hizi dunuiani wamefita Tanzania(kisiwa cha amani) wameleta mamluki wanaochochea fujo misikitini na makanisani,wakiwa wamevalia majoho ya dini-hawa ni mawakala wa ‘secret societies’ wametumwa!!
0713 324 074















1 comment:

  1. Umejichanganya kinoma Lincoln na vita ya Vietnam umejichanganya kinoma back school bro kuusu amani bongo aiezi kupotea kiraisi niwaarabu tu awataki kupoteza Mila zao wanatumia kigezo cha dini

    ReplyDelete