Friday, April 19, 2013

WALIOWAUA J.F KENNEDY NA ABRAHAM LINCOLN WANAFANYA USHENZI TZ(2)




Desemba  26, mwaka 2004, sahani inayobeba sakafu ya Bahari ya Hindi ikapasuka na kusababisha ebneo la kilomita 975(maili 600) kuwa shimo kubwa chini ya ardhi!
Bahari ya Hindi ikakosa pa kutuama, juu hadi chini na kutoka upande mmoja kwenda wa pili.Matokeo yalikuwa ni tetemeko kubwa la ardhi lenye ukubwa wa 9.0 katika kipimo cha Richter,ambalo halikuwahi kutokea miaka 40 iliyopita katika Bahari ya Hindi,jirani na Pwani ya Magharibi ya Indonesia na Kisiwa cha Sumatra.
Tetemeko hilo kubwa la ardhi,lilisababisha tani trilioni moja za maji ya bahari kugongana na kusababisha mawimbi makali ya maji yaliyotimka mbio mithili ya ndege!
Miamba ilikuwa imefumuka chini ya ardhi ya sakafu inayobeba hiyo bahari ya Hindi;sasa maji yaliharakisha mahali pa kukaa,yakasababisha mawimbi makali ya kutisha.
Hili ndilo janga la tsunami,lililoua watu zaidi ya 150,000 na kuwafanya wengine mamilioni kukosa makazi katika nchi 11 duniani. Unakumbuka  tsunami?
Bila shaka,utakuwa hujasahau kwamba janga lile lilisombwa kwa yale mawimbi makali,baada ya maji kusukwa sukwa,kutoka Indonesia na Visiwa vya Sumatra hadi hapa Afrika ya Mashariki.
Dar es salaam,Mombasa,Somalia pia kulitokea vifo na upotevu wa mali.Nataka kusema kwamba,balaa moja linaloanzishwa na Ibilisi katika pembe moja ya dunia, mawimbi yake(athari) husafiri kwa kasi na kuenea katika dunia yote.
Tsunami,iliyotokea Desemba 26,mwaka 2004 na kuua maelfu ya watu katika nchi 11 duniani,ni dalili kwamba Watanzania hawako salama na kila ‘ushenzi’ unaotendeka mahali pengine duniani.
Ukisikia Marekani, demokrasia  maana yake ni hata kichaa ama mvuta bangi kuwa na uhuru wa kumiliki bunduki,na akijisikia anakwenda kulipua watu ‘kidemokrasia’; na ukisikia Rais Barack Obama amekwama kutaka sheria ibadilishwe,umiliki wa silaha ufanyike kwa makini,watu wamempinga!
Ujue Tanzania ‘Katiba Mpya’ nayo itakuja na uhuru huo wa mtu kumiliki ‘Revolver’ na  ukimnyang’anya mshushu wake baa, anakulipua wewe,mkeo,watoto ,nyanya n.k
Ndiko demokrasia ya uhalifu inakotupeleka,na hushadidiwa na majununi walio wengi siku hizi!
Umesikia Marekani inagugumia kwa milipuko ya mabomu na watu wengi wamekufa wengine kuumia-haya ndiyo matokeo ya kiwenda wazimu ya kila mtu kuwa huru kununua bunduki  na vilipuzi(explosives)dukani, hata mvuta bangi na wazimu,mradi anazo pesa!
Mauaji na milipuko ni vitu vya kawaida kwa watu wanaojidai kuwa na uhuru,na wendawazimu wana uhuru hata wa kuua!
Kiama cha World Trade Centre(WTC) cha Septemba 11,mwaka 2001 walisingiziwa magaidi wa al-Qaeda, na twajua Septemba 16 mwaka 1920 mitaa tajiri ya Wall Street,ilishawahi kulipuliwa kwa mabomu watu 30 wakapoteza maisha.
Feburuali 26 mwaka 1993 majengo ya WTC yaliwahi kulipuliwa(kabla ya Osama) kwa bomu watu sita wakapoteza maisha.
Sababu za majanga na mauaji ya kuangamiza namna hiyo ni ushenzi unaoitwa demokrasia na ujuaji,kila mwehu anaruhusiwa kumiliki bunduki ama mabomu!!
Matokeo yake,Marekani, Rais James J. Garfield alipigwa risasi na Charles Guiteau,jijini Washington akafa Septemba 19,mwaka 1881.
Katika sehemu ya kwanza,nikaandika kwamba Rais Anwar Sadat wa Misri naye alifumuliwa risasi na Komandoo,akati akikagua gwaride la heshima mjini Cairo.Ilikuwa Oktoba 6, mwaka 1981.
Askari 7 waliuliwa 28 wakajeruhiwa;aliyemuua Sadat akafumuliwa risasi ya kichwa ili kuficha siri.
Ninakuonesha vigogo waliowahi kuuawa kwa risasi katika nchi zilizoendelea ambako watu wananunua bunduki kama nyanya sokoni.
Waliowahi kujeruhiwa kwaa bunduki ni wengi: Theodore Roosevelt alikua Rais wa Marekani, alijeruhiwa Oktoba 14 mwaka 1912.Adolf Hitler(Julai 20 mwaka 1944),Harry Truman pia rais wa Marekani(Nov,mwaka 1950),Papa Paul II(Mei 12,mwaka 1982),Rais Gerald Ford pia wa Marekani(Sept. 5,mwaka 1975),Ronald Reagan pia rais(Machi 30, mwaka 1981,hata Margaret Thatcher,  “Iron Lady” aliyezikwa juzi mjini London alinusurika kulipuliwa kwa bomu lililotegwa na magaidi wa Irish Republican Army(IRA) huko hotelini Grand ,Brighton ,England.
Watu wengine wane walikufa wakiwemo wabunge, akina Pinochet,Mubarak anayeshikiliwa kizuizini huko Misri, akina Castro,Nyerere-orodha ni ndfu, walishanusurika njama za mauaji.
Naam, hii ndiyo dunia tunayolilia kwamba iwe na demokrasia na kila mpumbavu awe huru kusema upumbavu wake na kusikilizwa hata na watoto. Usishangae leo Tanzania waliodhaniwa wenye hekima kufuatia kuvaa suti,ni wakola na kauli zao ni chafu zilizojaa uchochezi hata kwa watoto!
Haya hayakuanza hapa,tumeyakurupukia tukidhani ‘uhuru’ wa kusema “Freedom of Exspression” na bahati mbaya sana hatuwezi kupambanua ujinga na werevu.
Watu wanadai uhuru wa kuua,kutukana,kuiba,kuumiza watu hasa wanyonge n.k
Novemba 4,mwaka 1995(siyo mwaka 1997 kama nilivyosema katika makala iliyotangulia)Yitzak Rabin,Waziri Mkuu wa Israeli aliuliwa na Yigal Amir,mjini Tel Aviv.
Sababu ilikuwa Rabin akitaka uhuru wa dini mjini Jerusalem, hawa jamaa wa Mossad wakamwasha risasi, wako akina Cyprien Ntaryamira na Juvenal Habyarimana,Olof Palme orodha ni ndefu.
Chuki,uhasama,kugombea madaraka(supremacy struggle),kugombea utajiri,mradi sasa mwenye nguvu ndiye atasalia(survival of the fittest) sisi dhaifu tutakuwa mbolea!
M asikini ni nadra kupona katika mbio hizi za kugombea maisha(struggle for existence), matokeo yake tunajua vita vitaanzia Bungeni,serikalini,mahakamani,katika vyombo vya habari vinavyojidai kuzodoa wengine,hatimaye  mitaa inaenea damu mbichi!
                               DUNIA UWANJA WA FUJO ZA KIJINGA!
Dunia ni sayari ya tano kutoka kwa ukubwa nay a tatu kutoka kwenye jua.Uzito wake ni tani 6,580,000,000,000,000,000,000!!
Dunia ina kipenyo cha maili 7,926 Ikweta na maili 7,900 tu kutoka ncha ya Kusini hadi Kaskazini. Humo ndani ni UWANJA WA FUJO za kijinga,kufuatia choyo,ubinafsi mwingi(Yakobo 3:16,17).Wajinga wengi wanaharakisha kila mtu awe tajiri, awe na heshima na cheo(1Timotheo 6:10).
                WANASIASA UCHWARA?
Nimewahi kuimba wimbo wa Mwanamuziki Roger Whittaker, kwamba:
“Politicians are like a bunch of bananas. They hang together, they all are yellow and there is not a straight one”
Wanasiasa wote hufananishwa na ndizi katika chane. Ndizi zote hushikana mahali pamoja, zinakula kwa mama mmoja, zina rangi moja ya njano zinapopevuka,na hakuna hata ndizi moja iliyonyooka!
Naam,ndizi  zote zimepinda! Na wanasiasa wamepinda,hakuna mnyoofu! Pole wajinga wanaowaamini wanasiasa wenye maneno mengi.
Waziri Mkuu wa Uingereza, Winston Churchill (1940-45) aliwahi kusema kwamba, “No sentence should be more than nine words” Kwamba maneno katika vifungu vya maneno yawe mafupi yasiyozidi  kenda katika kila sentensi moja.
Churchill, alikuwa Mwandi wa habari mahiri sana, na alijifunza kanuni ya uandishi ‘Word economy’ lengo likiwa watu wame na maneno mafupi vitendo vyema vizungumze.
Bahati mbaya,kila Mtanzania siku hizi husema sana hata povu kutoka mdomoni,kila mahali kuna Bunge lake-Freedom of Expression!!
                           KUCHINJA/KUTOCHINJA
Shida hii ilianza katika Karne ya kwanza A.D,shida ya Wakristo kutaka kuchinja nyama zao,kwa sababu Wachinjaji hugeuza kuchinja ibada(ya miungu); kwamba kula nyama iliyotolewa kafara kwa miungu ni ibada ya sanamu?
Baraza la Yerusalem lilipiga marufuku Wakristo kula nyama zilizotolewa kafara kwa sanamu na wale wachinjaji ambao walikuwa makuhani wa miungu?
Tazama Matendo ya Mitume 15:29 utaona Mtume Paulo akipuuza ugomvi ule wa watu kususia kula nyama, kununua nyama buchani. Tazama 1Wakorintho 8:8-13 utaona Paulo anasema hata kama wachinjaji walifanya ibada huko ya miungu,wewe mlaji kama hujali inakuathiri vipi?
Wakristo wasijidai kukataa kula nyama zilizotolewa kafara kwa miungu,wakati wanaabudu miungu tele,na hawajatengana na dhambi,wanatenda dhambi huku wakisema  Roho haichafuliwi na matendo ya mwili!
Eti angalia roho yangu acha kuangalia matendo ya mwili! Uzinzi,uchafu,ubakaji,ufisadi,uongo,ujambazi,ushenzi wa kila namna! Lakini kula nyama zilizochinjwa na Waislam,dhambi!! Dhambi ni uasi wa sheria ya Mungu,unaitunzaje kama wewe unabaka watoto chekechea na kupora wake za waumini ndani ya joho la Ukristo?
1Wakorintho sura 8 Paulo anaonya tabia hii ya kinafiki,na kuwataka Wakristo kuishi kwa amani na waabudu sanamu.
Nataka kuwaambia Watanzania kwamba yapo mambo ya uchochezi toka mbali sana,yanaingizwa hapa nchini na kukurupukiwa na watu hawa ili kuvuruga amani. Haya yametokea mbali sana kwa Ibilisi,lengo kuleta vita vya kidini,ili kuwe na maangamizi makubwa zaidi.
Tsunami ilikuja kasi huku Pwani ya Tanzania,na fujo zitakuja nyingi wapumbavu watazipokea na kuongeza mawimbi katika bahari,na mwisho hayo mawimbi huwa makubwa mno na hugharikisha watu.
Itaendelea
0713 324 074








No comments:

Post a Comment