Thursday, May 2, 2013

waliowaua J.F Kennedy na Abraham Lincoln wataivuruga Tanzania(4)




OKTOBA, mwaka 2006,gazeti la New African, linalochapishwa 7COLDBATH Square, Jijini London,liliandika katika Toleo lake Nambari 455 kwamba, “  HOW THE ANGLICAN CHURCH TREATED ITS SLAVES”!!
 
Kwamba kanisa la Uingereza,Anglican, liliwahi kuwa na watumwa! Tena, watumwa wenyewe WAAFRIKA ama watu Weusi wa Asili ya Afrika, ‘negros’ wakatumikishwa na kanisa,wakateswa na kulimishwa katika mashamba ya miwa,kisha wakauliwa!
Kanisa hili, ambalo siku hizi huunga mkono ndoa za jinsi moja;ushoga,usagaji na kubadili jinsi(Kanisa la Afrika linajidai kuwa kichwa maji),Mkuu wake ni Malkia.Ndiye anayeteua maaskofu wakuu,makasisi na maofisa wengine.
Kanisa maarufu Uingereza,Westminster Abbey,(1050-1760) ndiko wazikwako watu wakubwa sana wenye kuheshimiwa.
Turejee katika ajenda ya leo,kwamba Feburuali 8 mwaka 2006,Askofu Mkuu wa Cantebury,Rowan Williams(mkuu wa Kanisa wakati huo) aliomba msamaha kwa DHAMBI hiyo ya kanisa kuwatumikisha watumwa,hasa watu WEUSI katika mashamba yaliyokuwa katika makoloni ya Uingereza huko Barbados,katika Visiwa vya Caribbean.

Nataka nikwambie msomaji,uwe makini na kila unachoambiwa na maaskofu,makasisi,wachungaji,manabii wa siku hizi,mitume uchwara na masheikh.Pima matendo yao na kauli zao kwanza.
Mwandishi, Adam Hochschild,  aliandika makala ndefu kwamba visiwa  vya Caribbean(walikopelekwa watumwa ndugu zetu wapendwa) viligeuka nyumba za kunyongea watumwa,kupigwa na kuteswa mithili ya magereza ya Abu Ghraib,Guantanamo na magereza mengine ya siri Ulaya.
Leo,Uingereza huongoza mataifa 54 ya Commonwealth,yaliyokuwa makoloni yake ili kuendeleza ukoloni mamboleo hapa Afrika.
Yangalipo makanisa na misikiti,masinagogi na nyumba za ibada,yanayopokea shuruti toka nje,ili yumkini kuzivuruga nchi zetu kwa ghasia na mauaji. Hivi,makanisa na misikiti,utumwa,mauaji,kunyonga watu na fujo vina uhusiano gani?
Waafrika wengi,hasa vijana wa siku hizi hawajiulizi ‘repercussions’ za kulipwa posho na vi NGO vya Ulaya ili kufanya vurugu hapa,na fujo za kijinga,kwa malipo ya chakula na ahadi.
Tazama Irak na Libya, siku hizi hamkani si shwari na Syria wameitumbukiza nchi katika miali mikali ya moto wa mabomu kwa kisingizio cha kutafuta demokrasia, nadhani tumeona hata Misri na kwingineko. Je, tumeshindwa kudai haki zetu kwa amani?
Wengine,hutumia dini kama zana za kueneza ‘Imperealism’-utawala wan chi moja dhidi ya mataifa mengine duniani.Dini zinapogeuka mlango wa kushawishi mataifa ya Afrika kuwa chini ya akina Malkia ama matajiri wafuasi wa Freemasons Ulaya ama Marekani!
Nakiri,dini halisi haifanyi unyama ninaosema hapa,mbali na kuwafundisha watu amani na upendo na heshima kwa viongozi wa serikali. Kuna serikali katiti na fisadi kuzidi Dola ya Rumi? Mbona Paulo katika Warumi sura 13 anawataka wafuasi wa Ukristo kuheshimu serikali?
Demokrasia na Haki za Binadamu hutumiwa siku hizi na hawa wauaji kama njia ya watu kutafuta haki zaidi,kumbe vijana wanaingia mkenge! Hawa ni wauaji wale wale ambao baba yao ana jicho moja na mkuki mkononi mwake.
Kuna kiitwacho, European Hegemony au tuseme ni ‘Political Domination’ ndicho huwasukuma hawa Wazungu kuvuruga  mataifa ya Afrika kwa vita,fujo,maandamano ya kipuuzi  kwamba ndiyo demokrasia na haki za binadamu!
Wee unachoma moto nyumba na magari ya wenzako kwamba ndiyo haki gani? Unaua wenzako na kuwanyima makazi halafu unasema ni kutafuta haki gani?
Bahati mbaya sana,viongozi wengi wa dini hupokea posho na maagizo kutoka Ulaya na mahali pengine zinakotoka dini zao,mwisho wa siku Afrika inawaka moto kwa machafuko.Huu ni ugaidi unaochochewa na dini hizi.
Mtu mmoja kaandika kwamba, “we need mental decolonization” kwamba tunahitaji kuondokana na utumwa wa fikra-utumwa wa mawazo.
Vyombo vya habari vya Afrika vingali utumwani,Marekani,Uingereza, Ufaransa,Ujerumani,Italia n.k
Kila kinachosemwa na vyombo hivi hushikiliwa na kushabikiwa pasipo kufikiri. Kila upuuzi na ujinga hushangiliwa sana. Mke wa Prince William akiingia hedhi,itatangazwa sana, akipata mtoto ndiyo  ‘Burning Issue’ siku hiyo watu wanapiga simu na kutuma SMS siku nzima! Hamnazo?!!
Kuku wa Mzungu akitaga mayai,watapiga kelele, timu ya Mzungu ikiishinda ya Afrika,watashangilia usiku mzima! Punguani??!!
Naam, huu ndiyo UTUMWA WA AKILI. Ili mradi, televisheni na magazeti ya Afrika na vijiredio vya siku hizi, vimepoteza akili na kutumbukia katika mijadala kuhusu wavuta bangi na wakola wa Ulaya na Marekani(nakisi ya ubongo) hushabikia ‘biased stories’ za Mzungu dhidi ya Afrika.
Kila mawazo ya upumbavu wa Mzungu kwamba Afrika ni nchi iliyopata uhuru mwaka 1994,rais wake ni Mandela na mji mkuu ni Nigeria,hushabikiwa hapa,SMS zitatumwa kila mjinga apate cha kujadili siku hiyo!
Nyimbo zinazopigwa katika vijistesheni vya redio ni upuuzi mtupu,mradi kapiga jambazi mmoja mbwia unga wa Marekani ama Ulaya.Nyimbo za Msondo Ngoma  siku hizi huonekana za kishamba sana!
Rais wa zamani wa Marekani,Thomas Jefferson, aliwahi kusema kwamba,
All men are created equal..But it would be impossible for black people to understand…”
Kwamba,watu wote wameumbwa wakiwa sawa,lakini ni muhali Mtu Mweusi kuwa na maarifa. Labda niseme utabiri wa Jeffersonb ulishatimia,ndiyo maana tumekosa ufahamu?
Sisi hatujitambui kwamba Mungu alituumba huru na tuko sawa na Mzungu au Mchina? Lakini watu wako radhi kuitwa ‘dog’ la Mzungu ama Mchina,na nywele tumebadili,rangi ya Afrika tumeitupa,hakuna Mwafrika siku hizi, nywele za Mzungu,makalio ya Kichina!
Sikiliza vinyimbo vya vijiredio vyetu..upuuzi. Ndiyo vile Mungu alimwambia Nabii Amosi, “Keep away the noise of your songs” peleka mbali nyimbo za kipuuzi(Amosi 5:23).
Akili za Mtanzania zimelala,zimelevywa na mvinyo wa Magharibi hadi uzalendo kwa nyi yetu umekwisha.Mafisadi huiba ili kuficha mali Ulaya,wanatamani wakaishi Ulaya.Wanaota Ulaya.
Ukiona habari. “The Most Influential People in The World” hakuna Mweusi hata mmoja,utaona wavuta bangi,wabwia unga wa Ulaya humo,hakuna kitu Afrika,na hakuna watu wenye mvuto!
Nijadili kidogo kuhusu uandishi wa habari Tanzania.Mwandishi sharti kuwa na “A Professional Attitude”Mtazamo wa kitaaluma kuhusu unachotaka kufikisha kwa wasomaji,watazamaji ama wasikilizaji.
Kwa kuwa hatuna chetu ila kushabikia upuuzi wa Marekani na Ulaya,basi watu wetu wanageuzwa kuwa Mzungu anavyotaka!
Kauli ya weledi na taaluma katika habari zinazotangazwa na vyombo vyetu vya habari hakuna.Kwanza waandishi humaliza miezi 10 bila kulipwa-wamedhulumiwa nao hufikiri kuitoroka nchi ama kuisaliti kama wanavyosalitiwa!
BBC,VoA,DW,CNN n.k wanachotangaza siku hizi ndicho kinachoingia akilini mwa watu na kushabikiwa katika mijadala ya vijiredio vingi,Watanzania wameporwa sauti,Mzungu amepewa sauti Afrika.Wakisema, Afrika hakuna fikra ni njaa na ukimwi na vita kutoka Cairo hadi Cape Town,tunakubali.Wakisema Dar hadi Accra  hakuna maarifa,tunasema ndiyoo! Hamnazo??
Kuna dhuluma,ufisadi na ushoga wa kifikra, sauti kapewa Mzungu hapa kwetu.Juzi tumeona Venezuela wabunge wakikunjana ngumi bungeni, tusubiri hapa akina Tundu Lissu wetu na akina Stephen Wassira na Lukuvi!
Watanzania tumegeuka watoto.Tunalalamika kama watoto.Tuna akili za kitoto,tunaidai serikali itufanyie kila kitu kama watoto: Itununulie maziwa, itupe nguo na chakula…hatudai kusimama na kufanya mambo mengi kama watu wazima.
Mwisho wa siku,Bunge hili, serikali na wanasiasa hawa wanatuona sisi kama watoto wadogo;wanatudanganya, “Takununulia pipi,peremende,chips’wakati wa chaguzi kumbe tunadanganywa huku tukisema,’sidanganyiki!’Chizi??!
Niimbe wimbo wangu uliotungwa na rafiki,
“Each time we blame the government for failing to keep us safe, and the government goes back to treat us like children!”
Leo,tunasukuma gari la mwanasiasa huyu, kesho serikali inakuja kumwaga peremende na chips,tunahamia huko na kuimba nyimbo za shangwe; hatuna akili,tunahadaika na wanasiasa wanajua sisi ni watoto wadogo,ndiyo maana serikali imechelea kutwambia kwamba ni ujinga kila kitu kuandamana na kuchoma matairi barabarani!
Watu wa aina hii hakuna kuwakataza,ni kuja na staili ya kuwadanganya maana ni watoto,kila mwenye hadaa huwateka akili.Siku hizi wanawafuata wenye ahadi, “Takununulia kaptula enhee!” Wanasema Hureee! Chizi?
Tujikinge na propaganda,tuamke,tusidanganyike kwa upuuzi wa kutumiwa ili nchi yetu iwake moto wa matairi na maguruneti  bure.
Tunahitaji Mtazamo Mpya, “New Attitude’ ili kujilinda na chachu ya Mafarisayo wa siku hizi.Busara Tanzania imekwisha, akili zimelala,uzalendo uko ICU’’Tumekwisha,tunahitaji dose  dhidi ya   ukoloni wa akili- mental decolonization.
Bila hivi,Waliowaua J.F Kennedy na Abraham Lincoln wanaivuruga nchi yetu, kwa kutumia makanisa,misikiti,majukwaa ya siasa n.k
TAMATI
0786 324 074




No comments:

Post a Comment