Wednesday, May 22, 2013

ZIARA YA OBAMA TANZANIA HAINA TIJA(4)



Imethibitishwa na Ikulu ya Marekani  kwamba,Rais Barack Hussein Onyango Obama, atawasili Dar es salaam Juni Mosi mwaka huu. Obama na mkewe,Michelle, watakuwa na ziara ya siku nane Afrika,katika nchi za Senegal,Afrika Kusini na Tanzania.
Amesita kwenda nyumbani Kwao,Kenya,kwa sababu huko kuna kilio cha makovu ya ukoloni waliofanya washirika wa Marekani,Uingereza, yaani Kenya imedai ilipwe fidia ya ukoloni.
babaye Obama(OBAMA sr) alifariki dunia Novemba 24,1982 kwa ajali ya gari.
HII SI MARA YA KWANZA Mwafrika kudai fidia ya ukoloni.
OMUKAMA(Mfalme) Solomon I wa Bunyoro, Magharibi wa Uganda , alitishia kuidai serikali ya Uingereza Pauni Trilioni 3.7; kama  fidia ya mali iliyoporwa wakati wa ukoloni.
   Mali hiyo, ni pamoja na mifugo iliyoporwa miaka ya 1890 wakati wa utawala wa babu yake, yaani Omukama Kabarega II.
  Naam, wakati wa vita vya miaka mitano.
   Kama Mfalme Solomon angefungua kesi hiyo, na mahakama ikampa ushindi, akalipwa hiyo fidia ‘nzito’ ya Pauni trilioni 3.7, miaka tisa iliyopita, serikali ya Uingereza ingefilisiwa.
    Raia takriban 800,000 wa Bunyoro wangejipatia kitita cha pauni milioni  4.63 kila  mmoja. Kiasi hiki mwaka 2004 kilikuwa sawa na shilingi za Uganda bilioni 15.2. Siku hizi nikama shilingi za Tanzania bilioni 6.3 kila mmoja Omukama Solomon  alisema, kamwe hajawasamehe Waingereza waliomwandoa madarakani babu yake, Omukama Kabarega II wa Bunyoro.
    Alisema, waliiba ng’ombe wakati huo wa vita dhidi ya babu yake, walichoma moto nyumba, waliharibu mazao na kuambukiza wanawake kaswende. 
  “Wanawajibika kwa vifo vya watu milioni 2.4; zaidi sana waliiba ng’ombe wa babu yangu na pembe za ndovu”, Mfalme Solomon alisistiza miaka michache iliyopita.
     “Ni unyama ambao tusingetegemea ungefanywa na watu wanaojidai kustaarabika sana . Walichofanya, hakina tofauti sana na wanavyotenda magaidi kama  al shabaab ama al-Qaeda leo”, akafafanua.
   Alikuwa amepata wanasheria ndani  ya Uganda na Uingereza kwenyewe; akatarajia kesi hiyo ya madai kuanza kusikilizwa mjini London mwaka huo wa 2004. Kiasi cha pauni trilioni 3.7 za fidia kilibuniwa baada ya Katibu wa Mfalme huyo, Yolamu Nsamba, aliyesoma uchumi katika Chuo Kikuu cha Hull , kufanya tathmini.
   Mwaka 2004, pato lote la Taifa(GDP) Uingereza, lilikuwa  takriban pauni trilioni moja kwa mwaka. Hivyo, fidia ya pauni trilioni 3.7 isingekosa kuifanya Uingereza Muflis.  Kama Ufalme wa Bunyoro ungeshinda ‘dili’ hiyo, kila raia wa Uingereza angelazimika kukamuliwa pauni 60,000 ambazo ni zaidi ya milioni 144 za hapa.
   Mchumi huyo wa Ufalme wa Bunyoro alisema, kiasi hicho kilihusisha mali ya Mfalme iliyoporwa na Wakoloni wa Kiingereza,mifugo, chakula, pembe za ndovu na akiba ya chumvi iliyochukuliwa katika nyumba ya Mfalme.
   Fidia hiyo haikujumuisha fidia ya ardhi ya watu wote, hasa waliouliwa. Ilikisiwa, fidia ya jumla ingekuwa mara 10 zaidi.
   Mwanasheria mwingine, Ernest Kizza, Spika wa Bunge la Bunyoro, aliingiwa kiwewe kwamba, kama hawa Waingereza wangeshindwa kesi hiyo na kuamuriwa kulipa fidia, basi uchumi wa Uingereza ungevurugika mno, kama chumi za Afrika ulivyovurugwa.
   Kama wasingeuchafua ufalme wa Bunyoro, Kizza alisema, basi leo ungekuwa taifa kubwa duniani(Super Power); na kwamba wangekuwa na ubavu wa kuikemea Marekani ikaufyata!
    Mfalme Kabarega, alitekwa na Waingereza katika mapigano ya 1899, akapelekwa uhamishoni, Seychelles , alikoishi kwa miaka 24. Wafungwa wenzake huko walikuwa wafalme wa Ashanti ( Ghana ) na Bahrain .Siku hizi Ashanti ni kampuni ya Mzungu.
   Aliachwa huru 1923, lakini akafia njiani wakati akirejea nyumbani Uganda , kabla ya kufika jirani na mpaka wa Bunyoro. Ufalme wa Bunyoro uliharibiwa baadaye na Rais Milton Apollo Obote katika miaka ya 60, ukarejeshwa na Rais wa sasa, Yoweri Kaguta Museveni mwaka 1993.
    Mfalme Solomon I  alikuwa amekaa mamlakani miaka 14 tangu atawazwe, na Wabunyoro wanalaani wizi wa Waingereza wa ng’ombe na mbuzi wao wakati wa ukoloni; wanaona ndiyo chimbuko la ufukara wao.
    Naam, nimetangulia kueleza kisa hiki cha miaka minne iliyopita, kufuatia Kasisi mmoja kuniandikia ujumbe kwa njia ya simu ya mkononi, kwamba niliwasingizia Wazungu kuhusika na vita na umasikini wa Waafrika, hususan katika vita vya 1999 nchini Sierra Leone .
   Kwamba, kama ni tamaa ya mali, watu wa mataifa yote,  bila kujali kabila na rangi walipenda mali na si Wazungu peke yao.
  Alikuwa akiilalamikia makala yangu iliyotokana na Filamu, “Blood Diamond”, inayowashushua Wazungu kuchochea vita  na machafuko Afrika, ili waendelee kusomba rasilimali; mafuta, pembe za ndovu, almasi(kama ya Sierra Leone ), dhahabu, samaki , ardhi kama ya Zimbabwe n.k
    Hadithi ya Mfalme Kabalega wa Bunyoro na tishio la mjukuu wake kufungua kesi ya madai mjini London , ni kielelezo cha namna ukoloni ulivyoidhalilisha Afrika; na  bado wageni hawa hawajatosheka kuinyonya Afrika, wanachochea vita, fujo na mauaji, ili Waafrika tuuane, wao wakisomba utajiri wetu. Mafisadi, madikteta na magaidi kama Osama bin Laden, wanawaandaa wao!
Juzi,Uingereza imekiri kuilipa serikali ya Museveni fedha hizi ambazo zilikuwa hazijafika Bunyoro,Uingereza ilikubali yaishe nje ya mahakama,na Kenya imerudia kutaka Uingereza kuwalipa Wakenya fidia ya utumwa.
    Ni kwa sababu hii, tunamuunga mkono kwa dhati Omukama Solomon I wa Bunyoro, kuona kwamba umasikini wa mtu mweusi haukujileta wenyewe; kuna mkono wa mtu, anayestahili kufunguliwa mashitaka.Anastahili kulipa fidia, tena kufikishwa The Hague kujibu mashitaka, sambamba na Taylor, Sankoh, Hitler, Milosevic n.k
    Vita vya Sierra Leone , vinavyosimuliwa katika filamu, ‘Blood Diamond’ vinaonyesha mtu mweupe akifanya uchochezi ili viendelee.
   Wakati katika sura nyingine, Mataifa yenye viwanda(G8) ambayo yaliwahi kuigawana Afrika mwaka 1884, yakijidai kuweka vizuizi eti  almasi ya nchi hiyo isiingizwe katika nchi zao…nikasema unafiki mtupu! Hivi, vitendo vya RUF, al-Qaeda, na vile vya Waingereza dhidi ya Ufalme wa Bunyoro , Ashanti n.k, vina tofauti gani?
    Kasisi, alitaka kusema ufukara wa Afrika ni shauri yao wenyewe na upumbavu wao, wakati makovu yapo yanaonekana; yalitokana na utumwa, ukoloni, vita vilivyoletwa na hawa, wakavuruga tawala zetu, wakawateka viongozi wetu wa Falme kama Ashanti na Bunyoro, wakawakata vichwa viongozi wetu kama Mkwawa na wengine. Waliiba dhahabu, almasi, mifugo mingi….walibaka akina mama na kuwaambukiza maradhi ya zinaa.
   Walifanya mengi yanayofanana sana na na   yale ya Saddam Hussein aliyenyongwa, magaidi kama al-Qaeda, au kuzidi. Baadaye, walikuja wakafungua  ‘dirisha dogo’ la misaada, wanawalazimisha viongozi wetu wa leo, wawapigie goti, ili eti watupe msaada!
  Afrika, madikteta wengi wana mizizi yao kwa Wazungu. Jean-Bedel Bokassa, alikuwa na mizizi yake kwa Wafaransa, kama alivyo Kanali Mohamed Bacar, aliyetaka kupora Anjouan. Wafaransa haohao bado wana makoloni Afrika.Wamejificha katika vivuli vya hawa vibaraka wao. Akina  Dikteta Augusto Pinachet wa Chile walikuwa na mizizi yao kwa wakubwa hawa.
   Marehemu Foday Sankoh, kiongozi wa waasi wa RUF wa Sierra Leone , waliokuwa wakikata wananchi mikono, midomo na miguu kwa mashoka, alikuwa na mizizi yake kwa Wazungu. Amini usiamini.
    Charles Taylor, kiongozi wa zamani wa Liberia aliyekilea kikundi hiki nchini mwake,  alikuwa akifanya biashara haramu ya kutorosha almasi za Sierra Leone hadi kwa Wazungu, huku mapigano makali yakiendelea.
 Popay  Sankoh, aliyezaliwa Oktoba 17, mwaka 1937 alifariki Julai 2003, akiwa mahabusu alikokuwa akisubiri hukumu ya kesi yake ya mashitaka 17 ya uhalifu wa kivita. Alitiwa mbaroni mwaka 2000.
    Hakuzaliwa akiwa katili na shetani. Alipata mafunzo ya vita vya msituni Libya , ambako alikutana na Charles Ghankay Taylor, aliyekuwa pia akiendesha vita vya msituni dhidi ya utawala wa Liberia .
Wakati huo Rais wa Libya,Gaddafi alikuwa Mtu wao na walimtuma kuwafundisha jeshi Taylof na Sankoh,nadhani unajua Taylor alitoroshwa jela na CIA huko Boston.
    Baada ya kupata mafunzo ya kijeshi na harakati za kijeshi nchini Libya , walirejea Liberia mwaka 1990, wakafanya walivyofanya hadi Taylor akawa rais Liberia . Baadaye, wakisaidiwa na Taylor, waliunda RUF kwa msaada wa biashara haramu ya almasi walizouzia Wazungu, huku wakibadilisha almasi kwa bunduki.
   Umoja wa Mataifa, na  Guinea kwa msaada wa hao Waingereza, wakaingilia kati mgogoro wa Sierra Leone , ndipo vita vikakoma mwaka 2002.
  Revolutionary United Front(RUF) walijigeuza chama cha siasa kilichoitwa, RUFP, na kushiriki uchaguzi uliofanyika miezi michache baadaye.
    Popay Sankoh, akiwa tayari katupwa kolokoloni, Almamy Pallo Bangura ndiye aliyegombea urais kupitia chama hicho, wakaambulia asilimia 1.7 ya kura, wala hawakushinda hata kiti kimoja cha Bunge.
    Wakati kesi yake ilipokuwa ikiendelea mwaka 2002, Sankoh aliangua kicheko mahakamani, bila sababu dhahiri na kusema: “Ninashangaa kuona nahukumiwa, kwani mimi kiongozi wa dunia?”
    Ni kweli kwamba alikuwa na ugonjwa wa kiharusi, alikuwa akipelekwa mahakamani kwenye kiti cha magurudumu. Alikuwa tayari dhaifu wa mwili na akili. Lakini, kauli yake hii, ilikuwa aikihoji mambo Fulani yaliyohusiana na mashitaka yake na Wazungu wanaojifanya viongozi wa dunia.Kwamba, yeye alikuwa nani kufanya biashara hiyo bila Wazungu kuikubali?
   Charles Ghankay Taylor aliyewekwa kolokoloni mjini Freetown kwa miaka mitatu kabla ya kupelekwa, The Hague Uholanzi, aliwahi kusema kauli kama hii, “Adui yako anapokuwa ndiye Bosi wako(Marekani), basi wewe umekwisha”.Hawa jamaa, walikuwa wakishangaa Wazungu kuwatosa, wakati walikuwa pamoja msituni.
    Miongoni mwa mashitaka 11 yaliyomkabili Taylor katika Mahakama hiyo ya The Hague, ni kushiriki vita Sierra Leone sambamba na waasi wa RUF, waliotuhumiwa kubaka, kuua na kufyeka watu miguu, midomo na mikono kwa mashoka.
Tayari Taylor kafungwa Uingereza ili anyamaze kimya!
    Lakini, kwa vyovyote, Ghankay Taylor na Popay Sankoh, walikuwa na sababu ya kutaka kuwahusisha wakubwa wa dunia(Wazungu) na vita walivyopigana Sierra Leone , unyama wao, mauaji na biashara haramu ya silaha, na almasi.Sina sababu ya kuchochea ukabila, naweka mambo hadharani.
    Waziri wa Sheria wa Sierra Leone , Frederick Carew, alisema: “Ushahidi tulio nao ni kwamba Taylor alitumia almasi kuchochea vita na kuleta dhiki isiyosemeka katika nchi yetu”.
 Je, almasi aliiuza wapi kama si alishirikiana na hawa Wazungu, waliompa hata silaha ili yeye na rafikiye, Foday Sankoh, waendelee kuua watu? Hawa jamaa walibadilisha silaha kwa almasi-na ndivyo filamu ile, ‘Blood Diamond’ inavyosema, kwamba Wazungu walifuata silaha hata Afrika Kusini, wakaziuza katika makambi ya waasi, wakachukua wanachi mateka na kuwalazimisha kuchimba almasi waliyouza Ulaya na kuendesha vita. Kasisi, aliyenitumia ujumbe wa SMS ananiona mzushi, nawazushiwa Wazungu!
    Charles Taylor,aliyezaliwa Feburuali 28, mwaka 1948, alitokana na waliokuwa watumwa wa Marekani, walioachwa huru. Mwaka 1997 raia wa Liberia walimpigia kura kwa woga, akashinda
   Juni 2003 waasi wa Lurds waliingia mjini Monrovia , Taylor akatimka. Alikamatwa Mashariki mwa Nigeria , baada ya kutoweka kijijini, Calabao, alipokuwa akishikiliwa tangu Agosti mwaka 2003.
   Alitaka kutimkia Cameroon na Chad , akashindwa. Alitiwa mbaroni Machi, mwaka 2006 akapelekwa The Hague.
   Uingereza ilishapiga ‘ndogondogo’ kwamba akatumikie kifungo nchini humo.  Ikawa hivyo.
Hii haina tofauti sana na Ufaransa kujidai kumpeleka Kanali Mohamed Bacar mahakamani, wakati ni mshirika wao wa karibu,- waafrika wanapigwa ‘changa la macho’.
    Madiktea wengi Afrika walioleta vita na kuwaburuza raia ni vibaraka wa hawa Wazungu. Amin Dada, kwanza alikuwa kibaraka wa Wazungu, wakamtema. Mobutu alikuwa kibaraka wao-alipoiba mabilioni ya fedha, akazificha kwao, wakati nchi ikikauka.
     Hata leo, hawa Wazungu wanafanya ufisadi mwingi hapa Afrika. Mikataba ‘hewa’   kama  ya rada mbovu inayowaweka akina Waziri Andrew Chenge matatani leo, imehasisiwa na hawa jamaa.
  Wanangoja siku ,wakikosana, ndipo waseme kuwa kuna fedha katika mabenki yao . Kwanini wasingesema  mapema, wakati zinapelekwa huko kufichwa?Fedha chafu zinafichwa kwao-ndiyo biashara hata ya baadhi ya Wahindi matapeli hapa.
   Hata fedha  zinafichwa na vigogo wetu katika mabenki yao.Zinajenga uchumi wao.
   Hawa na mafisadi, lao moja! Ni walewale, kasoro tarehe ya kuzaliwa!
   Watajibaraguza hivi na vile, lakini  hakuna hatua zaidi itakayochukuliwa.Mafisadi wataachwa watambe, kwa sababu wana mizizi mirefu Uingereza, Ufaransa, Marekani, Uswisi, Ujerumani , Canada n.k
     Migogoro ya kisiasa Afrika huletwa na Wazungu, ili wachukue mafuta, almasi, dhahabu, samaki, mazao ya misitu, wanyamapori, mazao ya kilimo, ardhi n.k. Tangu shambulio la magaidi la Septemba 11, mwaka 2001 hawa jamaa wanapunguza utegemezi wa mafuta na rasilimali nyingine Mashariki ya Kati. Huko, kunawaka moto.
    Wako katika Pwani ya Bahari za Atlantic , na Hindi, wanachukua mafuta na madini hapa; wanachochea migogoro mahali ambapo hawapokelewi kwa urahisi. Wanauza bunduki kwa vikundi vya waasi wanaopewa mafunzo  ya msituni katika nchi tajiri, kama tulivyoona, Sankoh na Taylor wakiwa Libya .
    Wangalipo watuhumiwa wengi wa uhalifu wa kivita Afrika…hawa wanatawala katika mbawa za wakubwa Wazungu, bila wasiwasi. Pindi akina Bush wanapokuja huku, hutandikiwa zulia jekundu na kuondoka pasipo kuhoji Demokrasia kwa hao ‘rafiki zao’ ambao situ  ni madikteta, bali wahalifu wa kivita kama Taylor, Sankoh, Milosevic, Hitler, Mohamed Bacar n.k
   Hawa vibaraka wa Wazungu, badala ya kusubiri kuchaguliwa na wananchi, wao ndio wanaochagua watu watakaowaweka madarakani-Nazungumzia Tume zisizohuru za Uchaguzi…kila kiongozi  mshirika wa  hawa Wazungu, ana tume yake inayomweka madarakani. Wazungu wako kimya. Wanampigia kelele yule anayewasaliti.
    Marekani na Wazungu wengine wanaruhusiwa kujenga ‘base’ zao katika Pwani ya nchi tajiri za mafuta, madini na rasilimali zenye thamani kubwa. Wanashirikiana na watawala mafisadi kuhamisha utajiri wa Afrika hadi huko Ughaibuni.
  Waafrika huendelea kuteseka na kulia njaa…ndipo  Wazungu wanapofungua vidirisha vidogo vya misaada ya kinafiki. Hawa na mafisadi, magaidi kama Bob Dinard, madikteta kama Bokassa na Mobutu, na wezi wa mali ya umma, lao moja. Amini usiamini…
Juzi Uingereza ikakimbia kuilipa fidia Uganda kufuatia madai ya Ufalme wa Bunyoro nje ya mahakama,maana waliona wanaaibika. Wamelipa Pauni milioni 700 lakini hazijafika, bado Ufalme huo unadai
Itaendelea
    0786\0754-324 074
     www.congesmrambatoday.blogspot.com
  
   

Be a better friend, newshound, and know-it-all with Yahoo! Mobile. Try it now.


No comments:

Post a Comment