Thursday, August 1, 2013

AMIN DADA

KANALI Muammar al-Gaddafi, alimpa msaada wa mkijeshi na kifedha Nduli Iddi Amin Dada wa Uganda.
Mwaka 1974,Wafaransa walitengeneza ‘Documentary’ iitwayo, ‘General Iddi Amin Dada’ iliyoonesha Amin alipokuwa akipanga mipango mahsus ya kuivamia Israeli.
Eti, angetumia skari wa miavuli,mabomu na watu wanaojitoa mhanga.Wakati huo alipewa silaha na Muungano wa Kisovieti(USSR);wakati Ujerumani Mashariki(Berlin) walimsaidia Amin kuimarisha GSU na kile kikosi cha kifo, The State Research Bureau(SRB)kilichosulubu wapinzani.
Wamarekani walisitisha msaada kwa Amin, ambaye alianza kugeukia ulimwengu wa Kiarabu.
Amin aliwaruhusu Wapalestina kuwashikilia mateka 83 wa Kiisraeli na baadhi ya wafanyakazi wa ndege, Air France Air Bus.
Operesheni ya kuwakomboa mateka wa Israeli, Operation Thunderbolt, ilifanyika usiku wa Julai 3,kuamkia Julai 4 mwaka 1976.
Makomandoo wa Israeli waliteka Entebbe ili kumfungia kazi Amin aliyekuwa amelala usingizi mjini Kampala,kilomita 27 kutoka hapo Entebbe.
Mateka watatu waliuliwa katika Operesheni hiyo na wengine 10 walijeruhiwa.Wateka nyara saba walifagiliwa kwa risasi za makomandoo wa Kiisraeli waliojipenyeza katika jengo walimokuwa mateka,wakaongea Kiyahudi.
“Wote laleni chini”,Yule ambaye alisita kutekeleza amri hata kama alikuwa Muisraeli alifagiliwa kwa risasi haraka sana!
Askari 45 wa Amin walipigwa risasi na makomandoo hao katika Operesheni ya dakika 90 tu(The 90 minutes at Entebbe).
Komandoo mmoja wa Israeli,Jonathan ‘Yonnie’ Netanyahu aliuliwa na askari wa Amin.Huyu Yonnie ni kakaye mkubwa Waziri Mkuu wa sasa wa Israel,Benyamini Netanyahu.
Mama mmoja, Dora Bloch(75) aliyekuwa amekwamwa chakula kooni, alilazwa katika Hospitali ya Mulago siku hiyo makomando walipofika Entebbe usiku.
Amin kwa hasira, alimfuata asubuhi hapo hospitalini akamuua mama huyo kinyama ili kulipa kisasi.Alimuua pia Muingereza mwenye asili ya Kiyahudi ambaye alikuwepo pia hapo Mulago,mjini Kampala.
Serikali ya Uingereza ilifunga uhusiano wa kibalozi mjini Kampala.
Silaha za Amin zilitoka Urusi kupitia Bandari ya Mombasa, baadaye Kenya wakaanza kumwekea mizengwe, na uhusiano wa kibalozi baina ya Kenya na Uganda ukawa mashakani.
Mwaka 1976 alitamka kwamba eneo la kati la Kenya na hata kilomita 32 ndani ya Nairobi lilikuwa eneo la Uganda zama za ukoloni wa Kiingereza.
Juzi,tulisherehekea siku ya mashujaa,na kuwaenzi askari wetu takriban 620 waliopoteza maisha katika vita vya Kagera vilivyomchakaza Amin hadi akatimkia Saudi Arabia.
Amin aliivamia nchi yetu Novemba 1978, na ilipofika Aprili 11 mwaka 1979 Kampala ilikwishatekwa na majeshi ya Tanzania.
Sherehe za Kumbukumbu ya vita hivi zilihudhuriwa na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Tanzania, Jakaya Kikwete, ambaye ameonya kwamba bado tuna nguvu nyingi za kumchakaza adui yeyote atakayejitia uchokozi kama Nduli,Joka Kuu Amin.
Askari 100,000 wa Jeshi la Tanzania(TPDF) waliungana na vikosi vya Waganda waliompinga Amin, baada ya kukaa kikao chao mjini Moshi(The Moshi Conference) wakaunda kikosi,The Uganda National Liberation Army ,na kumfungia kazi Amin.
Vita vilianza rasmi Oktoba 30 mwaka 1978 ili kumwondoa Kyaka alikokuwa amevamia na kufanya unyama mkubwa huko Kagera.
Awali, jeshi la Tanzania lilikuwa na skari kama 40,000 tu;wakaongezwa wanamgambo,polisi, JKT n.k hadi kufikia askari 100,000.
Yoweri Museveni, sasa Rais wa Uganda,wakati huo aliongoza kikosi maalum cha FRONASA,na Tito Okello na David Oyite Ojok,waliongoza kikosi kingine.
Kulikuwa na vikosi vingine kama Save Uganda Movement; hiki kikiongozwa na p’Ojok,William Amaria na Ateker Ejalu.
Sisi Tanzania wakati huo tukivurumisha makombora ya Katyusha ama BM ya Kirusi ambayo yalipopigwa KAMPALA walihaha wakasema walipigwa na Mwalimu Nyerere mwenyewe kutokea viwanja wa Sabasaba,Dar.
Gaddafi ambaye sasa maiti yake inaota kaburini, baada ya kufanyiziwa na Wamarekani alituma askari 2,500 ili kumsaidia Amin Nduli Joka kuu.
Waarabu hawa walichapwa katika mstari wa mbele wa mapambano, wakatekwa nyara wengi tu.Gaddafi alimpa Amin silaha kama vifaru,T-54 na T-55,BTR APCs,BM-21,Grand MRLs,artillery,MiG-21 na TU-22 Bomber.
Turejee kidogo Entebbe,usiku wa kuamkia Julai 4,mwaka 1976.
Muda kitambo baada ya makomandoo 100 washirika wa Mossad,kumtia adabu Amin,Marekani walituma ndege Uganda,naam Entebbe, ili kuwasaidia majeruhi wa Operesheni ile kamambe.
 Unajua, maofisa 53 wa Ubalozi wa Marekani walishikiliwa na wanamgambo wa Kiislam mjini Tehran,huko Iran.
Wateka nyara wa Kipalestina waliuliwa katika tukio hilo la Entebbe, na kabla ya kukumbwa na mauti walisikika wakitaka Israeli iwaachie huru Wapalestina 40 walioshikiliwa nchini Israeli.
Hadi sasa akina Mahmoud Abbas na Benyamin Netanyahu, wanazungumza hay o hayo hata baada ya kifo cha Yasser Arafat.
 Naam vita vya kisasi vya miongo mingi.
Hadi sasa Israeli  inapambana na wanamgambo wa Kipalestina, na wakati mwingine ndege zimetekwa ama zimejaribiwa kulipuliwa angani-VITA VYA KISASI.
 
Kamanda wa Operesheni ya Entebbe, Muki Besta, alikiri kwamba Operesheni ya Entebbe ilifanikiwa kufuatia ukusanyaji wa data nyingi na muhimu wa Mossad.
Vita vilivyokuja kupiganwa hadi Rntebbe Julai 3,mwaka 1976 ili kuwakomboa mateka 103 wa Israeli,tumewaona makomandoo 100 walioandaliwa vema na Mossad wakimkomesha Mwarabu na rafiki yao Amin Dada.
Naam, vita vya dakika 90 tu, The 90 minutes at  Entebbe.
Kwa Israeli, Waziri Mkuu anayekuliana na Waarabu ili kuleta amani anauliwa kama Yizak Rabin aliyepigwa risasi Novemba 4 mwaka 1995.
Itaendelea
0786 324 074
 
 
 
 
 
 
 
 

No comments:

Post a Comment