CONGES MRAMBA TODAY

Monday, July 22, 2013

AMIN

Dk.Milton Apollo Obote, alikuwa akihudhuria Mkutano wa kilele wa Commonwealth,huko Singapore alipopinduliwa na Amin.
Vikosi vilivyomtii Amin Dada,vilikamata uwanja wa ndege wa Entebbe,na jiji la Kampala likawekwa chini ya Ulinzi mkali,Makazi ya Obote yakazingirwa na jeshi,kasha mabarabara makubwa yaliwekewa vizuizi.
Radio Uganda,ikamlaumu Obote na serikali yake kwamba ilijaa upendeleo hususan kwa kabila lake la Acholi na Lango.
Raia nao hawakai mbali kwa viherehere,walishangilia majeshi kuipindua serikali ya mjini Kampala,wakidhani Amin angekuja na jipya,labda kuwapikia chai ya asubuhi!
Amin akatangaza kwamba yeye si mwanasiasa,nia skari;hivyo jeshi likashika hatamu hadi hapo siku ya uchaguzi mkuu ingetangazwa,baada ya hali kuwa shwari.
Haikutangazwa.Ila,wafungwa wa kisiasa waliachwa huru,ni wale ambao serikali ya Obote iliwasweka jela ama kizuizini.
Wakati huo msafara wa Obote uliokuwa Singapore ulilazimika kutua Dar es salaam,Obote akawa mkimbizi wa kisiasa kwa rafikiye, Hayati Mwalimu Nyerere. Obote aliungana na Waganda wenzake hapa Tanzania.
Mwaka 1972 hawa wakimbizi walijaribu kuipindua serikali ya Nduli Iddi Amin.Hawakujipanga vizuri;walishindwa vibaya.Amin akitaka kujikosha, akawaachia huru wafungwa wa kisiasa na akampa mazishi ya kitaifa Sir Edward Mutesa,aliyefia uhamishoni.Mazishi hayo yalifanywa Aprili, mwaka 1971.
Feburuali Pili, mwaka 1971 Amin alijitangaza mwenyewe kuwa Rais,Mkuu wa Majeshi,Mnadhimu Mkuu na Mkuu wa Vikosai vya Anga na akawa kila kitu.
Baadhi ya vipengele katika katiba ya Uganda vilibadilishwa vikaondolewa kabisa,Baraza la Kijeshi likaongoza nchi,wanajeshi wakaongoza Mahakama,serikali, Ikulu ya Kampala ikawa ‘Command Post’.
Amin aligeuza kikosi cha General Service Unit(GSU) kuwa kikosi cha kupeleleza wanaomsema vibaya The State Research Bureau,na ole wako ukutwe unaisema vibaya serikali ama Amin mwenyewe!
Unapelekwa Nakasero,unateswa kinyama hadi unakufa kasha maiti yako wanapewa mamba wa Mto Nile.
Tafuta filamu ya Whittaker,  THE LAST KING OF SCOTLAND, utajua Amin alikuwa nani?
Polisi nao walipewa ruhusa kukamata wenye midomo mirefu vijiweni asubuhi-subuhi,na kulikuwa na ma ‘MP’ wa jeshi na kikosi cha usalama wa Raia(PSU) kikitanda kila sehemu kubaini wapinzani wa serikali.
Ndugu zake Obote,Acholi na Lango waliteswa sana maana walihusishwa na jaribio la mapinduzi la 1972.
Kambi za Mbarara na Jinja zilifanya mauaji ya wapinzani wa serikali hii ya kiimla.Askari 5000 Waacholi na Lango waliuliwa kinyama sana,inakisiwa raia 10,000 walipotezwa!
Hawa walikuwa wa makabila hayo ya Obote na wale viongozi wa dini waliojitia kugeuza madhabahu kuwa kijiwe cha siasa za kumpinga Amin.Wanahabari pia walichinjwa ‘wakapotezwa’,wasanii waliokosoa serikali,majaji,wasomi,wanasheria na wanazuoni na raia wa kigeni,miili yao ilikuja kugunduliwa ikiliwa na mamba Mto Nile.
Utawala wa Amin(1971-1979) uliua watu wengi wasiofahamika idadi.Inakisiwa labda watu 80,000 walikufa ama labda 300,000.Amnesty International walisema Amin aliua watu 500,000.
Miongoni mwa watu maarufu waliouawa ni Benedicto Kiwanuka,Waziri Mkuu wa zamani na Jaji Mkuu,mwingine Askofu Mkuu wa Anglikan,Janani Luwum,Joseph Mubiru,Frank Kalimuzo,BYRON Kawadwa,na mawaziri,Erinayo Wilson Oryema na Charles Oboth Otumbi-unakutwa asubuhi nyumbani kwako na maofisa wa SRB unachukuliwa ndani ya buti ya gari,kisha mke wako hakuoni tena-umeliwa na mamba wa Mto Nile.
Amin aliwalisha mamba wa Nile kwa maiti za wapinzani wa serikali yake,mwaka 1972 ilikuwa Agosti,Amin akatangaza vita vya kiuchumi. Aliwatimua Waasia 80,000 walioishi Kampala huku wakiwa na passport za Uingereza,maduka yake walipewa nduguze Amin.
Hawa Wahindi wengine walizaliwa Uganda zama za ukoloni,wakajidai kutojipambanua kama raia,wakafanya biashara na passport za kigeni mkononi,walitimuliwa wakaacha maduka yao nyuma,magari na mali nyingine.
Walijifanya si wazalendo wa nchi, wakijidai kuthamini uraia wa Uingereza,Canada,Marekani na mahali pengine.Amin alivunja uhusiano na Uingereza, akataifisha biashara 85 za Waingereza.
Uhusiano wa Uganda na Israeli nao ulikufa,ingawa Waisraeli walishajenga miradi kadhaa pamoja na uwanja wa Entebbe.Israeli iliwauzia Waganda silaha. Walikuwa washauri wa kijeshi lakini Amin akawatimua akajenga uhusiano na Kanali Muammar al Qaddafi na Warusi.
Mwaka 1976 Juni,likatokea tukio la Wapalestina(PFLP-EO) na Wajarumani wa Revolutionare Zellen kuteka Waisraeli hadi Entebbe,watu 156 ambao hawakuwa na passport za Israeli waliachwa huru ndege hiyo ilipotua Entebbe.
Watu 83 na wengine 20 wakiwemo wafanyakazi wa ndege walishikiliwa na wateka nyara hao hapo uwanja wa Entebbe.
Umewahi kusikia Operation Thunderbolt? Ama umewahi kusoma 90 Minutes at Entebbe? Umewahi kutazama filamu ya Raid on Entebbe? Nitakupa full stori katika matoleo yajayo juu ya Waisraeli kukomboa mateka wao hapo Entebbe, usikose toleo lijalo
0713 324 074
 





Posted by CONGES MRAMBA at 5:24 AM
Email ThisBlogThis!Share to XShare to FacebookShare to Pinterest

No comments:

Post a Comment

Newer Post Older Post Home
Subscribe to: Post Comments (Atom)

welcome to Mwanza The Rocky City

About Me

CONGES MRAMBA
IS AMONG THE BEST WRITERS IN THE EAST AFRICA REGION
View my complete profile

Blog Archive

  • ►  2014 (2)
    • ►  June (1)
    • ►  February (1)
  • ▼  2013 (127)
    • ►  December (4)
    • ►  November (3)
    • ►  October (6)
    • ►  September (16)
    • ►  August (8)
    • ▼  July (11)
      • MISRI NA DEMOKRASIA YA AFRIKA
      • amin
      • AMIN
      • amin
      • MAGUFULI JEMBE BWANA
      • marekani na uasi Afrika
      • MANDELA NA OPRAH
      • MAREKANI INAPATA SHIDA KUJISAFISHA
      • DAR HATARINI KUVAMIWA
      • mandela alimpenda sana Oprah Winfrey
      • MISRI INAVUNA ILICHOPANDA
    • ►  June (31)
    • ►  May (13)
    • ►  April (7)
    • ►  February (7)
    • ►  January (21)
  • ►  2012 (151)
    • ►  December (41)
    • ►  November (9)
    • ►  October (20)
    • ►  September (1)
    • ►  August (29)
    • ►  July (9)
    • ►  June (9)
    • ►  May (20)
    • ►  April (2)
    • ►  March (4)
    • ►  February (3)
    • ►  January (4)
  • ►  2011 (49)
    • ►  December (7)
    • ►  November (2)
    • ►  October (3)
    • ►  September (2)
    • ►  August (2)
    • ►  July (4)
    • ►  June (17)
    • ►  May (3)
    • ►  April (9)
Simple theme. Powered by Blogger.