Monday, July 22, 2013

MANDELA NA OPRAH

MANDELA ‘alimzimia sana’ Oprah Winfrey

                      Na Conges Mramba
SHUJAA wa Afrika,ambaye sasa yu mahututi hospitalini mjini Pretoria,Nelson Mandela, alimhusudu sana nyota wa Marekani mwenye asili ya Afrika, Oprah Winfrey.
Katika makala yake fupi iliyochapishwa Mei 14,mwaka 2007 katika Orodha ya watu mashuhuri 100 wa Gazeti maarufu la TIME(The TIME 100 List),Mandela alisema Oprah alikuwa nguzo ya kimataifa yenye kuumba upya njozi za wasichana wadogo wa Afrika Kusini waliokata tamaa.
‘Tata’Madiba, alimueleza Oprah alimueleza Oprah katika makala hiyo kuwa miongoni mwa mwatu mashuhuri sana duniani. Makala hiyo ilikuwa miongoni mwa nyingine zilizoonyesha wasifu wa watu mashuhuri duniani, makala ambazo pia ziliandikwa na watu mashuhuri.
Makala hiyo ya Mandela ilimweka Oprah miongoni mwa watu wengine mashuri sana walioandikwa katika jarida hilo la TIME, ambao ni pamoja na Papa Benedict XVI aliyejiuzulu, Hillary Clinton, Sonia Gandhi, Hu Jintao,Ayatolla Khamenei,Angela Merkel, Arnold Schwarzenegger, Thierry Henry, Barack Obama na wengine.
Mandela alimtaja Oprah mwanamitindo tajiri,anayemiliki gazeti na kuendesha kipindi cha televisheni, ‘Oprah Winfrey Show’ kama nguzo muhimu sana katika kuwaondolea vikwazo watu wenye shida kote duniani.
Oprah, alizaliwa Januari 29,mwaka 1954 huko Kosciusko,Marekani, sasa tajiri aliyeorodheshwa na jarida maarufu la Forbes miaka michache tu iliyopita kama ‘tycoon’ miongoni mwa Wamarekani Weusi.
Ameanzisha shule ya wasichana Afrika Kusini-The Oprah Winfrey Leadership Academy for Girls- iliyoko jijini ,Johannesburg.
Shule hiyo huchukua watoto wa kike kuanzia elimu sawa na darasa la saba hivi hadi kidato cha nne,na ilifunguliwa na Mandela.
Katika hotuba ya ufunguzi,Madiba akasema ingeangaza ‘Future’ ya wasichana Afrika ya Kusini.
Oprah(59) amekuwa akitazamwa na Mandela kama ‘Potential Figure’ katika kuwasaidia wasichana na akina mama kujinasua katika  hali duni ya maisha.
“Wasichana wanakabiliwa na laana ya matarajio duni ya kimaisha na fursa zisizo sawa na wanaume”,aliandika Tata Mandela katika makala hiyo katika gazeti la TIME,akifafanua kuwa Oprah ni  “A Model for all of them and for all of us”
Tata Mandela alimwita Oprah kuwa shujaa wa kizazi chetu.Katika orodha hiyo  ya gazeti la TIME(The 100 TIME List)Rais Barack Obama alikuwa nambari Moja,kufuatia TUMAINI LA KUPENDEZA njozi aliyoota tangu akiwa seneta huko Illinois,aliikopa kwa mchungaji wake wa Kanisa la Kilokole analoabudu, The Trinity United Church of Christ, huko Chicago.
Katika orodha hiyo ya TIME La Mei 14, mwaka 2007 ya watu maarufu walikuwemo pia akina Condoleezza Rice ‘Condi’,Raul Castro,Osama bin Laden,Omar Hassan Ahmed al Bashir, Malikia Elizabeth II, Warren Buffet na David Rockefeller.
Wengine ni George Soros,Al Gore na Leonardo DiCaprio,aliyecheza filamu ya BLOOD DIAMOND inayosimulia vita vya almasi za damu huko Sierra Leone wakati wa Charles Taylor na Waasi wa RUF.
Taylor sasa amefungwa Uingereza na kiongozi wa Waasi,Fodday ‘Poppay’Sankoh alifia rumande huko The Hague,Uholanzi.
 
 
 
 
 
 

No comments:

Post a Comment