Friday, July 12, 2013

MAREKANI INAPATA SHIDA KUJISAFISHA

TANGU UHURU,miaka 237  kamili iliyopita, ‘demokrasia-njiwa’ ya Marekani haijawahi kuruhusu mwanamke kuwa Rais.
Hillary Rodham Clinton, alishindana na Barack Obama katika chama chao cha Democrat, pasipo kufua dafu; alikuwa akiwania uteuzi wa kugombea urais,Novemba mwaka 2008.
Kuna akina mama wengi wasomi katika taifa hili, wana uwezo mkubwa labda kushinda wanaume.
Lakini, hakuna hata mmoja aliyevuka vizingiti na mizengwe katika uteuzi ndani ya vyama vyao vilivyokithiri kwa mfumo dume.
Condoleezza Rice(57), utotoni akiitwa, “Condi”, alikuwa Mshauri wa Rais wa Usalama wa Taifa,kabla ya kuwa ‘Secretary of State’ ama Namba 3 wakati wa Utawala wa George W.Bush .
Baada ya Bush kumaliza mhula wake 2008,wengi walidhani angeteuliwa kuwania urais kupitia chama chao beberu cha Republican.
Wapi bwana!
“CONDI’mwanamke,tena Mweusi mwenye asili ya Afrika,ateuliwe na Republican kugombea urais?
 Thubutu!!
Susan Rice,Balozi wa Marekani Umoja wa Mataifa(UN) na Mtaalamu wa Usalama wa Taifa, aliyeteuliwa punde baada ya Barack Obama kuingia mamlakani,ni mwanamke,tena kama alivyo ‘Condi’ ni Mweusi wa asili ya Afrika; anayemshauri Obama masuala ya Afrika.
Namkumbuka Balozi Dk.Jendayi Frazer, alikuwa Msaidizi wa Condoleezza Rice wakati wa utawala wa Bush;msomi mwenye Shahada ya Uzamivu(PhD);Mjuvi  katika masuala ya Bara la Afrika.
Hata hivyo,kama ilivyo kwa Dk Condoleeza na Susan Rice, hawa ni ‘wanawake’ tena Weusi wa asili ya AFRIKA;watakuwaje Marais katika macho ya Wamarekani Weupe?!
Hillary Clinton(64) angeweza kuwa rais wa Marekani na kuweka rekodi ya mke wa Rais Mstaafu(Bill Clinton) kuwahi kuwa Seneta wa New York, na Rais wa kwanza mwanamke.
Angeweza kuwa miongoni mwa viongozi wa  nchi; akina mama kama Angela Merkel wa Ujerumani,Ellen Johnson-Sirlief ama Joyce Banda hapa Afrika,kama siyo kama Waziri Mkuu wa zamani India,Indira Gandhi, na wengine wa Brazil,Argentina,Korea Kusini n.k
India,ni taifa lenye demokrasia pevu duniani kuliko Ulaya na Marekani.Je, Marekani inaweza kumchagua Rais mwanamama,halafu Mhindu?
Marekani,waweza kumchagua rais mwanamke asiye na shahada ya chuo kikuu ili kuwaongoza?
Kwa miaka takriban 240 sasa tangu wapate uhuru kutoka Uingereza, Marekani hawajawahi kumchagua rais asiye Mkristo!
Sembuse Muislam kuwa Waziri Mkuu Uingereza
! Ama Bahai kuwa Mkuu wa nchi hizi,zenye kutangaza sana haki za binadamu,usawa wa jinsia na demokrasia?
Obama, kavunja mwiko wa kuchaguliwa Mtu wa asili ya Afrika kuwa Rais wa Marekani.MARAIS wa Marekani aghalabu huwa wanaume;tena Wazungu kamili!
Walimpinga sana Obama,wakasema huyu kazaliwa Kenya; Obama naye akamuua Osama Bin Laden,basi kelele zikazimwa za kumpinga.
Ndiyo maana,Obama akijua misingi ya Ubaguzi wa rangi na siasa za kimwinyi na kihafidhina, aliposhinda Urais 2008 akasema, “THE CHANGE HAS COME TO AMERICA”.
Hizi ndizo siasa za akina Martin Luther King Jr, Malcolm X,Luis Farakhan na wenzao Weusi wa Marekani zama hizo.
Turejee India,nchi ya demokrasia pevu duniani.
Sonia Gandhi mwenye asili ya Italia,tena Mkatoliki,mjane wa Rajiv Gandhi,ambaye alihitimu tu High school-hakuwa na shahada ya Chuo Kikuu!
Miaka 16 tangu kuuawa kwa mumewe,Rajiv,Sonia nee Maino Gandhi,aliongoza Chama cha Congress,ambacho mwaka 2004 kilishinda;na Sonia angekuwa Waziri Mkuu wa India,akakataa mwenyewe na kumteua Mchumi,Manmoahan Singh.
UWAZIRI Mkuu wa Singh ukaletwa Sonia Gandhi ambaye ana watoto:Rahul na Priyanka,ambao waweza nao kuuata nyayo za ukoo wa Gandhi.
Uingereza, Mawazari wakuu wote wamekuwa Waanglican kasoro wachache; hawataki watu wenye mawazo mapya kama Askofu Peter Akinola,Askofu Mkuu wa Nigeria.
Akinola(68) alipinga kanisa hili la Anglikan Marekani kumchagua shoga-V.Gene Robinson kuwa askofu huko Hampshire, Marekani mwaka 2003.
Kanisa lenye waumini takriban milioni 80 duniani(sawa na raia wote wa Misri) sauti lazima Kutoka kwa Malkia wa Uingereza, ndiyo maana mawaziri wakuu wengi wamekuwa Waanglikan hata kama kuna Waislam,Budha,Wahindu,Bahai sijui Wasabato n.k
Eti hii ndiyo demokrasia pevu ya Ulaya na Marekani na Haki za Binadamu tunazoimbiwa huku,ambayo akina Obama na Bush hujidai kustawisha kwa mabavu huku Afrika!
Tuwe na akili.Tanzania,INDIA,Malawi,Brazil,Uganda n.k wanajali zaidi haki za akina mama kuliko hawa.
Hata Ulaya,Margaret Thatcher wa Uingereza kawa Waziri Mkuu,wakati India tayari akina Indira walishatawala.
Marekani hakuna rais au Makamu wa RAIS Mwanamke,Uganda ilishakuwa na Makamu wa Rais Mwanamke,na Tanzania kuna SPIKA Mwanamama.Rwanda kuna wanawake wengi wabunge,sasa utatwambia nani anawanyima haki wanawake?
Marekani wanajalije akina mama wakati miaka takriban 40 hakuna rais au Makamu wa rais mwanamke?
Uingereza,ni Thatcher tu,Waziri Mkuu mwanamama,wengine wote madume,wakati hata Ghuba ya Korea sasa kuna rais tena msichana tu sawa na Brazil na Argentina na hata Chile kwa akina Michelle Bachelet.
Leo,nataka kuwafumbua macho watu wan chi hii kudhani Ulaya na Marekani kuna demokrasia ya ajabu sana!
Wakiona Obama analindwa sana huku hata hawezi kutokeza katika gari la wazi,wanadhani Marekani ama Uingereza angekwenda disko peke yake bila ulinzi!
Wakati hata London, magari yangeondolewa barabarani ili Obama apite, na asingethubutu kukiuka itifaki ya ulinzi kama kawaida.
Itifaki haichagui Afrika ama Ulaya,hata Papa alichapwa risasi mchana kweupe Ulaya,na Marais wengi wa Marekani waliuawa ndani ya nchi-tuwe na akili jamani.
Marekani,Oprah Winfrey hawezi kuwa rais kwani ni mwanamke tena Mwenye asili ya Afrika.
Akina Mohamed Ali walivuliwa taji la ubingwa wa ndondi duniani kwa sababu walipolazimishwa kwenda kupigana vita vya Vietnam 1968/69 wakakataa ikawa shida.
Hapa kinachoitwa ‘demokrasia’ participation of majority na serikali za watu na watu kwa maslahi ya watu wote ni uongo.
Washington kuna maslahi ya Wamarekani tena wa sili na si Weusi; Katrina ilipopiga mwaka 2005 Wazungu kwanza waliokolewa kwa helkopita,Weusi wakabaki wanaomboleza juu na mapaa ya nyumba zao!
Itaendelea
0786 324 074,0713 324 074,0754 324 074
 

No comments:

Post a Comment