Monday, June 17, 2013

ANAKULA NYETI ZA WAPINZANI WA SERIKALI?



‘mungu’ wa Equatorial Guinea anayekula ‘nyeti’ za wapinzani wa serikali yake!
TEODORO OBIANG NGUEMA MBASONGO, alitawazwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Guinea ya Ikweta Agosti 3, mwaka 1979,kufuatia mapinduzi dhidi ya mjomba wake,Marcias Nguema Biyogo.
Nguema Mbasongo,ni miongoni mwa viongozi wa kiimla hapa Barani Afrika, ambao viongozi wa Magharibi humfananisha na Robert Gabriel Mugabe wa Zimbambwe, “Zim Country”
Ni mpwa wa Rais wa Kwanza,Dikteta Fransisco Marcias Nguema Biyogo, alimpindua kupitia jeshi mwaka 1979 ambao hapa Afrika ulikuwa mwaka wa anguko la madikteta.
Baada ya kukanyaga Ikulu,akatangaza kupitia redio ya taifa kwamba sasa yeye ni ‘mungu’ ambaye anao uwezo wa kula maini na hata makende(testicles) ya watu wanajitia kichwa ngumu kumpinga!
Guinea ya Ikweta,ni taifa dogo la watu kama 500,000 hivi.Ukubwa wan chi hii ni maili za mraba 10,800 katika Ghuba ya Guinea.
Alizaliwa Juni 5, mwaka 1942; akawa rais Oktoba 10, mwaka 1979 kupitia mapinduzi ya kijeshi katika taifa hili lililopata uhuru wake Oktoba 12,mwaka 1968.
Huyo mjomba wake, ‘Masie’ alikuwa pia mbabe sana aliyeisababishia nchi kufilisika. Ndipo Agosti 1979 Teodoro Mbasongo akaongoza Mapinduzi ya kijeshi, akapiga marufuku nyama vya siasa.
Hii Guinea,huzalisha sana mafuta hapa Afrika; ni kama nchi ya tatu hivi nyuma ya Nigeria,na Misri.Na Wazungu huitamani hata walitaka kumpindua mwaka 1994 akanusurika.Waliofanya njama ni pamoja na mtoto wa Waziri Mkuu wa zamani Uingereza, Margaret Thatcher, Sir Mark Thatcher.
Nchi ni tajiri sana,watu wake ni masikini sana, nadhani msomaji umewahi kusikia ‘laana ya rasilimali’-The resources curse!
Hata hivyo,Jarida la Forbes limemtaja Teodoro Nguema miongoni mwa viongozi matajiri sana hapa duniani;utajiri wake ukifikia Dola za Marekani milioni 700.
Utajiri huo unafuatiliwa na Shirika la Kupambana na Rushwa, Transparency International ili kubaini mahali alipouficha Ulaya.
Hivi sasa inasekemekana anaugua saratani. Katika viwango vya Utawala Bora na Haki za Binadamu vinavyotolewa na Mo Ibrahim, alipata asilimia 46 kati ya nchi 54 za Umoja wa Afrika.
Nchi hii haina uhuru wa habari kama huku kwetu;kuna rushwa kupindukia.
Kuna redio moja tu ya taifa inayotegemewa na watu kupata habari.Sasa kama hujipendi nenda ukapeleke maneno huko uone cha mtema kuni!
Unakatwa ‘nyeti’ zako halafu zinawekwa kwenye friji,kabla ya kuliwa baadaye!
Alipata alama 34.7 katika viwango vya Mo Ibrahimu vya Utawala Bora.Mwaka 2003, katika kipindi cha redio ya taifa kinachoitwa, “Bidze-Nduan” tafsiri yake Kuzika Moto!
Kipindi hiki cha redio ya taifa huhimiza amani,utulivu na kuheshimu mamlaka katika nchi, ilitangazwa kwamba Rais Teodoro Obiang Nguema Mbasongo sasa anawasiliana na Mungu moja kwa moja!!
Kwamba Rais alikuwa na mawasiliano ya Mung Mwenyezi moja kwa moja.
Radio hiyo ilisema kwamba rais Teodoro ni kama Mungu wa mbinguni, ambaye anayo mamlaka yote juu ya wanadamu na viumbe wengine.
“Ana maamuzi ya kuua chochote,pasipo yeyote kumuuliza,kwa sababu yeye pia yu mungu”,Tangazo la redio hiyo lilisema.
Mwandishi wa Shirika la Utangazaji la Uingereza,BBC,Angue Nguema, akasema kwamba redio hiyo ya taifa husikilizwa na raia wengi kwa kuwa hakuna redio nyingine na hakuna utitiri wa magazeti kama hapa Tanzania.
Nguema amekuwa akishinda chaguzi kwa asilimia 100.MHULA WA UCHAGUZI HUKO HUCHUKUA MIAKA SABA.Mara ya mwisho uchaguzi ulifanyika 2009;na utafanyika tena 2016.
Wasaidizi wa rais huyu husema kwamba, ana nguvu za miungu ndani yake-redio huwaonya watu wanaotaka kuondoa amani ya nchi wachukue hadhari-watakiona cha moto, ‘nyeti’ zao zitang’olewa na kuwekwa kwenye friji kasha kuwekwa kwenye sahani za ‘State House’.
Hivi sasa Obiang ana umri wa miaka 71; na ametawala kwa jumla ya miaka 32.
Mke wake anaitwa Constancia,ambaye ni miongoni mwa wake za Marais wa Afrika, “First Ladies” wanaoponda sana maraha,yeye na Mke wa ‘RG’Mugabe,Grace.
Mugabe alikuwa Rais Zimbabwe tangu 1987,kabla ya hapo alikuwa Waziri Mkuu.
Gazeti la East African la Desemba 27 mwaka 2011 likamweka Rais huyu miongoni mwa marais madikteta watano wabaya Afrika
Wengine waliorodheshwa chini ya kichwa cha habari, “THE LEAGUE OF EXTRAORDINARY DICTATORS”ni pamoja na Omar Ahmed Omar Hassan al-Bashir, Mugabe,Isaias Afwerki wa Eritrea,Laurent Gbagbo sasa yuko rumande The HAGUE.
Nchi zinazoongoza kwa utawala Bora hapa Barani ni Mauritius,Cape Verde,Botswana,Ghana,Namibia,Afrika ya Kusini,Seycheles,Sierra Leone,Mali sasa imetiwa doa na vita ya wenyewe kwa wenyewe na Tanzania.









No comments:

Post a Comment