Wednesday, June 12, 2013

ICC MAKAO MAKUU YA UKOLONI MPYA AFRIKA-2

JUNI Pili, mwaka huu 2013,Malkia wa Uingereza, Elizabeth Alexandra Mary, alitimiza miaka 60 kamili tangu atawazwe rasmi kuwa Malkia Juni Pili,mwaka 1953.
Malkia huyu alikuwa Kenya Feburuali 6 mwaka 1952 wakati baba yake,King George VI alipoaga dunia, yeye malkia akarithi kiti cha ufalme wa Uingereza na kuanza kuyaburuza makoloni yao chini ya mwavuli mpya wa ukoloni, Commonwealth.
Huyu,pia ni Mkuu wa Kanisa la Anglican tulilotazama katika matoleo yaliyopita kwamba nalo liliwahi kuwa na watumwa(Waafrika!)
Huyu mama,Elizabeth,leo anatawala kwa miaka 60;Malkia Victoria(jina lake limepewa Ziwa Nyanza kwa heshima yake), alitawala Uingereza kwa jumla ya miaka 80.
Nataka msomaji ujiulize kwamba, Magharibi na washirika wao wanasema Mugabe, Gaddafi,Mengistu Haile Mariam na wenzao wame ‘Overstay”;sasa huyu mama kukaa mamlakani huko Uingereza anawakilisha nini katika kinachoitwa,DEMOKRASIA?
Tumesoma katika toleo lililopita,mshirika mkubwa wa Uingereza,Marekani na washirika akifariki dunia,wao wakamlilia sana marehemu Meles Zenawi,mwaka 2012.
Wakati Zenawi anachinja demokrasia Uhabeshi, alikuwa ametoa ruhusa kwa madege yasiyo na rubani-drones-ya Marekani kuipeleleza nchi yoyote hapa Afrika na kufanya kituo uwanja wowote wa Uhabeshi; kasha hata kuipiga mabomu na kuisambaratisha.
Licha ya kunyamazisha Upinzani katika nchi,na kuitia gundi na kufuli midomo ya waandishi wa habari,Zenawi alikuwa ‘Darling’ kipenzi cha Marekani na Uingereza na washirika wa Ulaya Magharibi,hadi wasingetishia kumkamata na kumpeleka The HAGUE,Uholanzi kwa mauaji ya wapinzani.
Wala,Kanisa la Anglican ambalo juzi limekiri kuhusika katika biashara haramu ya utumwa dhidi ya Mtu Mweusi wa Afrika-African Transatlantic Trade-halijatolewa tamko kukamatwa kwa Kanisa hili na kupelekwa The Hague kujibu mashitaka ya kuwafanya watumwa Waafrika,ama kulipa fidia nje ya mahakama.
Tunaambiwa, Askofu Mkuu wa Canterbury,Rowan Williams(amestaafu) na mwenzake wa York,John Sentamu(raia wa Uganda) wamesema wanajuta kwa vitendo hivyo vya kishetani vya kanisa kuwageuza binadamu kuwa kama wanyama kazi!
Kanisa hili la Uingereza,lilimiliki mashamba Barbados ambayo yalitumikisha ndugu zetu Weusi kama watumwa;walipigwa mijeledi kisha wakapigwa mihuli ya chuma cha moto migongoni!
Niliwahi kuona ng’ombe wa babu yangu wakipigwa mhuri wa moto kwenye tako ama kunako nundu,huku wakilia kwa uchungu, ‘’booo!’’
Hili kanisa linalojiita la Mungu,liliwapiga mhuri wa moto watumwa,watu weusi wa Bara hili ili wawe na Mhuri, ‘SOCIETY’ migongoni mwao!
Kanisa hili lilimiliki mashamba huko Barbados,kwa hiyo likahitaji watumwa wakufanya kazi.Kwa sababu wangeweza kutoroka ama vinginevyo,kanisa liliona heri wawe na mhuri wa chuma cha moto, SOCIETY katika migongo yao!
Hiki ndicho akina Askofu Sentamu na Rowan Williams wamekiri juu juu kwamba Kanisa lilifanya makosa na dahambi ya utumwa!
Sasa,tungetazamiwa Kanisa liilipe Afrika fidia ya mabilioni ya Pauni za Kiingereza kwa kuwadhalilisha ndugu zetu huku wakiwapiga mhuri wa moto, ;Society,utadhani punda ama maksai la ng’ombe.
Kenya,tumeona juzi MAUMAU wakikomaa na kulipwa fidia ya kama shilingi 500,000 kila Maumau;na Ufalme wa Bunyoro ulishaifungulia kesi serikali ya Uingereza kwa kupora rasilimali za Bunyoro zama za Ukoloni mkongwe.
Serikali ya Uingereza iliufyata mkia na kukubali kulipa fidia,nitaeleza kisa hiki mbele ya safari.
Nia siyo kuzua chuki na mitafaruku mipya katika dunia; ni kutaka Uingereza na Marekani na washirika wao,waelewe kwamba tabia yao ya kujidai watakatifu na kuwahukumu wenzao na kuwaua kwa risasi kwamba ni madikteta ama wauaji, tunaijua fika na waache mara moja!
Burma,makampuni ya Kimarekani yaliwahi kutumikisha raia kujega bomba la gesi,raia wakafungua kesi makampuni hayo yakalipa fidia.Walishirikiana na utawala wa kijeshi wa Burma ambayo siku hizi inaitwa Myanmar.
Hatujawahi kuona madikteta rafikiki wa Magharibi, ama Kampuni mumiani kama Royal/Dutch Shell lililoua watu Nigeria wakati wa Sani Abacha, wakizungumzwa kupelekwa The HAGUE.
Mahakama ya mjini Hague inayoitwa,The INTERNATIONAL Criminal Court(ICC) ilianza kazi zake Julai Mosi,mwaka 2002.
Wao wanasema ilianzishwa ili kudhibiti mauaji ya Kimbari Rwanda na Bosnia. Mahakama hii ilianzishwa kwa makubaliano ya nchi 120 huko Rome, mwaka 1998.
Nchi nyingine za Amerika Kusini zilizunga mkono Mahama hiyo,na Ulaya nzima wanaishabikia kasoro mataifa machache hapa Afrika.
Watu kwa kutojua, wanadani mahakama hii inalenga kuondoa kiburi cha watawala wanaoua raia zao na wengine kushiriki vita, “Impunity” kumbe, hii ni mahakama kama chombo cha kuwatia kabala hasa Waafrika jeuri wenye kumpinga MZUNGU na maskahi yake!
Marekani,inayojidai kuwa pembeni na mahakama hii huchochea kila jambo;mahakama eti inapeleleza na kuendesha kesi za mauaji ya Kimbari(genocide); uhalifu wa kivita dhidi ya utu na ubinadamu na makosa ya kivita.
Sasa jiulize hata wewe unayeshabikia kila kitu cha Mzungu,Kanisa la Uingereza lilipotia mhuri watumwa migongoni kwa chuma cha moto mkali ili wawe na nembo ya ‘SOCIETY’ kwa akili zako ilikuwa nini kama siyo uhalifu mkubwa dhidi ya utu-Crimes against Humanity?
Mahakama hii ya ICC imechukua hatua gani dhidi ya MALKIA ambaye ni Kiongozi wa dini hii,mradi akina Sentamu(Mweusi)huchaguliwa na kuondoka?
Mahakama hii huongozwa na nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya(EU)na Umoja wa Kujihami Ulaya Magharibi(NATO)kasoro eti Marekani na Uturuki wamejiweka kando.
Wanadanganya wajinga kwamba eti ICC siyo chombo cha Umoja wa Mataifa(UN) isipokuwa eti ni chombo huru cheye mamlaka kamili ya kisheria(legal capacity) ambacho hujiongoza hata kifedha;kwamba kinahusika tu kwa wanachama,na kwamba makao makuu yake ni The hague, Netherlands.
Nataka nikwambie msomaji, Umoja wa Mataifa ulishashindwa kusimamia amani duniani,unashiriki kufanya unyama na kufumbia macho mafisadi na wauaji-leo mahakama hii inafanya nini?
Sasa,katazame akina nani wamekamatwa na kushitakiwa au wanatakiwa kushitakiwa,utaona akina Gbagbo,Fodday ‘Poppay’Sankoh na Charles Taylor, akina Joseph Kony,Thomas Lubanga,Jean Pierre Bemba, akina Omar Hassan al-Bashir na wengine wachache sana wa Afrika na Yugoslavia ya zamani!
Utawaona akina Ruto,rais Uhuru Kenyata, na wengine zama za akina Adolf Hitler,lakini kamwe husikii kuwakamata waliopindua serikali ya Libya ama irak ya Saddam wakiguswa!
Afrika kwa kujiingiza kichwa-kichwa katika mahakama hiyo,wamejipalia makaa kichwani,ndiyo maana utaona asilimia 99 ya washitakiwa ni Waafrika,wachache wa kutoka Bosnia na Yugoslavia ya Slobodan Milosevic.
Marekani na Uingereza wakivamia Irak ama Libya,wao si wanachama ICC kwahiyo hawaguswi,walikuwa wakitetea demokrasia tu! Hizi ndizo ‘double standards’ ambazo wenye kufikiri vema wanaona,halafu mazuzu wa Afrika wanasema ICC hureee!
Kwa hiyo utaona ICC IKIJIFICHA kushaghulikia kesi za Rwanda na Bosnia,kumbe wanalengwa watu wengine walioharibu maslahi ya Ulaya kama Wakenya hawa waliosababisha makampuni ya Kimarekani na Kiingereza kuporwa mwaka 2007,na wala siyo ile vita ya kuua watu 1400 na wengine 600,000 kukosa makazi.
Utaona wameshughulikiwa watuhumiwa wa Kenya,Congo,Sierra Leone, Liberia , Ivory Coast  ,Angola,Sudan n.k
Waafrika watakapong’amua ICC ni mtego wa kuwanasa ili watiwe chapa migongoni mithili ya watumwa wa KANISA LA ANGLICAN, watakuwa tayari na mihuri ya society migongoni!
Ufunuo 13:11-18 inasema habari ya watu ‘kutiwa chapa’ katika mapaji ya nyuso na mikono ya kulia ya utekelezaji wa sera za Magharibi.
Wau hawataki kujifunza tunakokwenda,wamesalia kushabikia kila kinacholetwa ana akina Obama na Cameron.
Safari hii siyo mhuri wa SOCIETY,ni 666, na namba hii wanaijua wenye akili tu.
Nimeandika kwamba ICC ilikubaliwa kuanzishwa mjini Rome Italia, wajanja wanapojificha ndani ya majoho ya Kanisa siku hizi tunaona wakihubiri siasa na kuwatukana wazi mawaziri na serikali hata ya Tanzania,maana wanajua wanawakilisha SOCIETY.
ICC imemweka “Chief Prosecutor” mpya kutoka Gambia,Fatou Bensouda,baada ya kelele za afrika kwamba ICC inawashitaki Waaafrika tu.
Bensouda, amekwishakanusha jambo hili maana kapewa ulaji huko Marekani na Ulaya,sasa kumrithi Luis Moreno-Ocampo,wengine wanaona Afrika imeula sana!
Marekani na Uingereza wamekuwa wakishirikiana na madikteta lukuki hapa, akina Joseph Desire Mobutu Sese-seko, “Kuku Ngbendu wa za-Banga”.
Labda,hukujua tafsiri hasa ya jina hili la rafiki mpendwa wa Ulaya na Marekani. Ni ‘Mpiganaji anayeshinda kutoka vita moja hadi nyingine,na nyuma aliacha maangamizi yasiyosahaulika!”
“The all-powerful warrior who goes from conquest to conquest, and leaves behind unforgettable destruction of his enemies”.
Sasa jiulize, huyu mobutu alishirikiana na hawa jamaa kumuua Patrice EMERY Lumumba,zama za uhuru.Kama Marekani kuna demokrasia na uhuru,kwanini Mobutu muasisi wa maangamizi wa wapinzani wake hakushughulikiwa?
Septemba 17, mwaka 1961,Katibu Mkuu wa Umoja wa MATAIFA,DK Darg Hammarskjold wa Sweden akajitia kusuluhisha mgogoro wa Congo uliodumu miaka 50, alitegeshewa bomu angani ndegeni jirani na uwanja wa ndege wan DOLA,nchini Zambia,akafa kwa kinachoitwa Ajali na NDEGE,kumbe Shirika la Ujasusi la Marekani,CIA lilimuulia mbali.
Hili shirika la CIA lilikuwa swahiba wa Makaburu wa Afrika Kusini,na liliwasaidia sana akina Jonas Savimbi na UNITA huko Angola.
Kifo cha Hammarskjold hakikuwa tofauti sana na kile cha Samora MACHEL WA MSUMBIJI.
Kuna uhalifu na wahalifu tele waliotengenezwa na CIA:Saddam Hussein,Gaddafi,Osama bin Laden,Jonas Savimbi,Charles Taylor akina Sankoh waliofia the Hague walipokea amri kutoka Washington!
Dikteta Sani Abacha aliwaua akina Ken Saro-Wiwa ili mafuta na Ogoni,Niger Delta yazidi kuwanufaisha makampuni ya nje na serikali ya kijeshi ya Abacha.
Nataka kusema kwamba,Makao Makuu ya AU,Addis Ababa na Mahakama ya mjini Hague,ni maadui wa dhati wasiojuana,ambao hata sasa wanabusiana! Itaendelea
0786 324 074
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

No comments:

Post a Comment