Monday, June 24, 2013

MISRI ITAPIGANA VITA ISIYOSHIDA DHIDI YA AFRIKA MASHARIKI



            
SERIKALI ya Misri, iko katika vita vya maneno na Ethiopia,kufuatia Ethiopia kujenga Bwawa la kufua umeme kwenye Mto Nile.
Mto Nile, huanzia Ziwa Victoria,katika maporomoko ya Owen,Jinja nchini Uganda,mahali ambapo pia Uganda hufua umeme unaouzwa hata mkoani Kagera hapa Tanzania.
Kuna mito kama Kagera unaoanzia Burundi na kutiririka hata Rwanda,kabla ya kufika Kagera na kuingia Ziwa Nyanza linaloitwa Victoria, ambako hutiririka chini kwa chini hadi Owen Dam,Jinja unapoanzia Mto Nile.
Kuna Mto Nzoia huko Kenya;Mito miwili:Kagera na Nzoia huchangia takriban nusu ya maji ya ziwa hili la kwanza kwa ukubwa Afrika.Ni ziwa la Pili kuwa na maji baridi duniani,nyuma ya Ziwa Superior huko Marekani.
Ipo mito mingine mingi kama Ruvubu na Nyabarongo ambayo pia huingia ziwa Victoria na kuchangia Mto Nile kufurika na kutiririka kutoka Afrika Mashariki.
Mito mingine ni Suguti,Mori,Sio,Yala,Nyando,Sondu,Miriu,Mara,Simiyu n.k ambayo humwaga maji yake ziwa hili wakati wa msimu wa masika,na hufanya Nile kutiririka kwenda Bahari ya Mediterranean.
Bonde la Mto Nile linajumuisha nchi za Rwanda,Burundi,Uganda,Tanzania,Kenya,Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo(DRC),Eritrea,Ethiopia,Sudan na Misri yenyewe.
https://encrypted-tbn1.gstatic.com/images?q=tbn:ANd9GcSaIEMRk4--8iHz109R0_lPBqZtTDTok1K4ZLdDU79kRY6sU534
Hata hivyo, serikali ya Misri ikitambua kwamba Mto Nile ndiyo chanzo kikuu cha Uhai wa Taifa; na kwamba Nile ni hatma ya maisha na kifo kwa watu wao,walikimbilia kuingia mkataba na serikali ya kikoloni ya Uingereza mwaka 1929;mkataba ambao ulipiga marufuku nchi nyingine hizo kutumia maji ya Ziwa Victoria na Mto wenyewe kumwagilia mashamba ama kufua umeme.
Mkataba huo ulisainiwa tena mwaka 1957 kati ya Misri na Uingereza ili kuzuia nchi za Bonde hilo la Mto Nile kumwagilia mashamba yao na kufua umeme kwa ajili ya maendeleo ya watu.
Misri, imewahi kutishia kupigana vita vikali na Kenya,endapo ingechukua maji ya Ziwa Victoria ama matawi ya Nile(Blue Nile na White Nile kwa miradi ya maendeleo; kwamba kungesababisha maji yasitiririke kutoka huko Owen falls, Jinja.
https://encrypted-tbn1.gstatic.com/images?q=tbn:ANd9GcRzsqB8dqKYwRbARSlJH66u_n4bbRcghhkAJJZa8UJEqNlSZoMZ
Mto Nile hutiririka kwa zaidi ya kilomita 6,900  kutoka Afrika Mashariki hadi Misri na kuingia Bahari ya Mediterranean.
Kitendo cha Tanzania kwa mfano kuchukua maji ya Ziwa Victoria na kuyapeleka Kahama,Shinyanga eti ingeomba ruhusa ama kibali kutoka Misri!
Hapa ndipo shida ilipoanzia.Ethiopia imeamua kujenga Bwawa la kufua umeme katika Mto Nile ili kujiepusha na tatizo la nishati iliyo muhimu sana katika maendeleo ya watu hivi leo.
Ingeweza hata kumwagilia mashamba,ili kuepukana na janga la njaa inayoikumba dunia ya Ulimwengu wa tatu.Kwa Misri, eti Ethiopia imekiuka mikataba ya kale ya Misri na utawala wa Malkia wa Uingereza.
Hivyo, Misri imetangaza vita na Ethiopia, na kama mgogoro huo hautamalizwa kidiplomasia, basi vita vya maji ya ziwa hili vitakuwa vimeanza.Ethiopia inatuhumiwa na Misri kukiuka mikataba hiyo ya 1929 na 1957;mikataba inayozuia nchi zetu kutumia maji haya kwa namna yoyote mbali na kunywa,kuoga na kuoshea mifugo tu.
Misri na Sudan,hupata maji ya Nile  baada ya maji haya kuwa yamesafiri kutoka kwetu kutokana na mvua zinazonyesha huku za masika katika miezi ya Aprili na Mei na  maji hayo hutiririka hadi Misri na kufika Agosti na Septemba.
Mvua zinaponyesha Tanzania,Kenya,Uganda,Burundi na Congo maji huingia ziwa hili kwa mito mingi,halafu huanza kusafiri hadi Misri. Hawa Wamisri hufikiri kwamba tukitumia maji haya ya ziwa huku au ya Mto Nile Sudan na Ethiopia,basi kina cha maji yam to kitapungua kwa takriban mita(cubic meters) bilioni 50.
“Maeneo mengine Misri,watu wamefariki kwa njaa na wengine hulazimika kula mbwa ili wasife njaa kufuatia ukame”, alisema Waziri wa Maji ya Umwagiliaji wa Misri, Dk. Mahmoud Abu-Zeid.
Wanataka kina cha maji kiwe kikubwa kabisa hadi juu ya kingo kama cubic metres bilioni 150 hivi, ili wawe na amani na mataifa ya Afrika ya Mashariki.
Hivyo,kupungua kina cha maji huko Nile ni kitisho cha maisha ya watu milioni 85 huko Misri,ambako Nile huabudiwa kama moja ya miungu tangu zama za Nabii Musa(BC 1500).
Binti Farao wakati akienda kuabudu mto huo asubuhi ndipo alipokiona kitoto Musa ndani ya chombo kilichotengenezwa kwa majani ya Mto Nile.Wakati Misri inawakataza watu wa Bonde hilo kutotumia maji haya,yenyewe inafanya midadi mikubwa ya umwagiliaji na vyanzo vya umeme.
Kuna Mradi wa Bwawa la Aswan-Aswan High Dam,ili kutengeneza Ziwa Nasser.Misri ni jangwa,na mvua hazinyeshi jangwani.maji yake yametoka hapa Kwetu Afrika Mashariki.
Misri huendesha mradi mkubwa wa mashamba ya umwagiliaji katika Bonde la Toshka,ambao ni takriban ekari 600,000.Mradi huo uko katika jangwa la Kusini,umejengwa mfereji wenye urefu wa kilomita 310 ambao utabeba maji yenye ujazo wa cubic metres bilioni 5.5 kutoka ziwa bandia la Nasser.
https://encrypted-tbn1.gstatic.com/images?q=tbn:ANd9GcQC8A75CtBnxYUgwpTBpwkdL2mh30XBsGx2P26GBYAvt-phinNZWA
Hali hii huonesha kuweko kwa miradi mikubwa sana ya kilimo cha umwagiliaji huko Misri na miradi hiyo hutumia jumla ya cubic metre bilioni 25 za maji ambayo chanzo chake ni ziwa  Victoria.
Watu wengi Misri huishi kandoni mwa mto huu na wamekuwa wakimwagilia mashamba tangu zama za Nabii Musa nakabla ya hapo kama miaka 3000 BC.
Hata hivyo, mataifa ya Afrika Mashariki yamegomea ‘ujanja’ huo wa Misri na wakoloni wakisema Kenya,Uganda,Tanzania n.k walipata uhuru miaka ya 1960,hawakuwepo wakati Misri ikiingia mikataba ya kitapeli na Uingereza-hatukushirikishwa- iweje kufungwa na mikataba ya 1929 na 57?
Ziwa Victoria liliitwa hivyo na Mwingereza wa kwanza kuliona,John Hanning Speke,ambaye aliliita Victoria kwa heshima ya Malkia Victoria wa Uingereza.
https://encrypted-tbn0.gstatic.com/images?q=tbn:ANd9GcQt36TCl5srJPh9QvwwXJpY61fXiuXL1QSl6hPCzuuUNxY1abOWfQ
Zama za Ukoloni,Uingereza ilijitia kumiliki ziwa hilo hivyo ikawauzia Misri ‘Mbuzi kwenye gunia. Ili wakamwagilie mashamba yao kwa maji ya ziwa hili,wakati sisi tunapokufa na kuzimia kwa kiu na njaa huko Afrika Mashariki.
Je, mikataba ya takriban karne moja iliyopita,itatuzua nchi zetu kutumia maji ya Ziwa Nyanza ili kumwagilia mashamba na kupata nguvu za umeme?
Uganda,hutumia maji haya kupata umeme huko Owen falls Dam,Jinja.Rais Yoweri Kaguta Museveni amesema, “Hatutaki Misri wafe njaa,lakini lazima sisi tukae na kuzungumza suala hili,kwani hata sisi tunahitaji chakula”.
Sasa Misri hutaka kutumia vita kutuogopesha sisi kutumia maji hayo kwa miradi ya maendeleo ama nishati-hydroelectric projects.
Umoja wan chi za Bonde la Mto Nile-Nile Basin Initiative(NBI)Makao makuu ya sekretariati yao yako Jinja Uganda,kandoni mwa ziwa kubwa lenya ukubwa wa kilomita za eneo 68,000.Tanzania humiliki asilimia 51,Kenya asilimia 6 na Uganda humiliki asilimia 43 ya ziwa hili.
Maji ya ziwa hili ambayo hufika hata Misri na kuingia Mediterranean,baada ya kukusanywa na mito ya Afrika Mashariki katika eneo la kilomita za mraba 193,000 Rwanda,Uganda,Kenya,Tanzania na Congo.
Takriban watu milioni 35 wanaishi kandoni mwa ziwa hili katika nchi hizi zetu,na ziwa ni chanzo cha samaki takriban tani  500,000 kwa mwaka.
Sasa,vita viko mlangoni kati ya Misri na nchi za Afrika Mashariki,vita vya kugombea maji ya Ziwa hili.
“Ole wan chi ya uvumi na mabwawa,iliyoko mbali kupita mito ya Kushi(Ethiopia),taifa ambalo Mito inakata nchi yao(Tanzania) ambayo bendera imeinuliwa Mlima Kilimanjaro”, Isaya 18:1,3.
Congesmrambatoday.blogspot.com
0713 324 074/0786 324 074




No comments:

Post a Comment