Tuesday, June 11, 2013

WANAUME HUFIKIRI NGONO MARA 60,480 KWA MWAKA


UINGEREZA, kuna imani kwamba,wanaume wengi hapa Duniani wamejenga tabia ya kufikiria kufanya ngono kuliko kingine chochote!
Kufuatia hali hiyo, wataalamu wa Saikolojia hudhani wanaume wengi hupenda ngono kuliko chakula, ama kuliko kufanya kingine chochote.
Naam, kuliko fedha na maisha!
Wanaume wengi wato tayari kfa kuliko kukosa ngono!
Inakisiwa kwamba, kila baada ya dakika mbili,mwanaume hufikiria kufanya ngono.
Kufuatia Filosofia hiyo,katika muda wa saa moja tu,mwanaume hufikiria kufanya ngono mara 30.Sijui Mungu hufikiriwa mara ngapi?
Hii ni kusema kwamba,wanaume hufikiri mambo ya ngono mara 720 kila baada ya saa 24(siku moja); na kwa wiki nzima wazo la kufanya ngono hutokeza katika akili ya mwanaume mara 5,040! Hapo upo?
Kwa mwaka mzima(siku 365,saa 5,dakika 48 na sekunde 47.8 za Dunia kulizunguka jua)wanaume hufikiria kufanya ngono mara 60,480!!
Kufuatia utafiti huo,ingawa wanaume wamejengwa kwa misuli imara iliyokakamaa(wanawake wamejengwa kuwa  ‘soft’)kumbe,ukweli ni kwamba wanaume ni dhaifu(strongest but weak) kuliko inavyofikiwa
Kupitia mazoea uya kupenda kufanya ngono, wanaume ni dhaifu, wengine hupoteza uhai na kufilisika,kufukuzwa kazi,wengine wamefukarishwa na matendo ya kingono;ni watumwa wa ngono,naam watumwa wa mapenzi,watumwa wa wanawake.
Tamaa ya ngono ya akina baba,imewafanya akina mama wawe na sauti kubwa,na wawe wenye nguvu(stronger sex) kuliko ilivyotazamiwa.Mwanaume akinyimwa ngono katika unyumba, atapiga mayowe makubwa,ufanisi wa kazi utaporomoka, msongo wa mawazo,atamwaga chozi na kulalama na kuomboleza hadi kupiga magoti na kuihari hata kutoa uhai wake kuliko kuikosa ngono.
Mwanaume akinyimwa ngono na mpenziwe,hata biashara yake itashuka ufanisi wake, aghalabu hugeuka zuzu.
Naam, tamaa ya ngono imewageuza wanaume wengi kuweka rehani mali na maisha yao,wamegeuka dhalili kupindukia(weaker sex) na wengine wametimuliwa katika nyadhifa zao kubwa zenye ukwasi,kwa kubaka ama kufanya mahaba mahali pasiporuhusiwa.
Aliyekuwa Mkuu wa Fuko la Fedha la Kimataifa(International Monetary Fund),Dominique Straus Khan(DSK) mwenye umri wa miaka 64, alitimuliwa wadhifa wake wa Rais wa IMF,kufuatia tama na ngono-alibaka!
Msichana mwenye umri wa miaka 32 wakati huo,mrembo wa haja kutoka Guinea-Conakry,mfaya kazi wa usafi na kutandika vitanda hotelini,Diallo, akasababisha DSK kupandishwa kizimbani kwa tuhuma za kubaka msichana huyo kutoka Afrika Magharibi.
Ilikuwa Mei,mwaka 2011,DSK alipopandishwa kizimbani kwa tuhuma za ubakaji,huko New  York ,Marekani.
DSK ni mtu aliyeogopwa sana; alikuwa mbabe sana,na alipozungumza dunia ikatetemeka!
Lakini, alishindwa kuzuia tamaa zake za ngono, akasahau wadhifa wake mtukufu wa Mkuu wa IMF,kabaka-alikuwa mtumwa wa ngono;ametimuliwa madarakani na wadhifa wake kapewa Mfaransa mwenzake,mwanamama Christine Lagarde.
                        RUSHWA YA NGONO
Rais wa zamani wa Benki ya Dunia(WB)Paul Wolfowitz, aliachia ngazi Juni 30 mwaka 2007,kufuatia rushwa ya ngono wakati wa Urais wake hapo WB.
Walfowitz,Balozi wa zamani wa Maekani huko Indonesia na Naibu Waziri wa Ulinzi katika Makao Makuu ya Jeshi la Marekani,The Pentagon,tamaa ya huba kwa kidocho Mfanyakazi wa Benki hiyo,ilimpokonya wadhifa mtukufu duniani,na marupurupu makubwa!
Alipoondolewa WB nafasi yake alipewa Mmarekani mwenzake,Robert Zoellick.Alikuwa mpiganaji wa mstari wa mbele wa rushwa na ufisadi katika mataifa yanayoendelea,waliwanyima wananchi wan chi nyingi mikopo kwa sababu ya utawala mbaya,lakini yeye naye akaondolewa kwa kosa la rushwa ya ngono.
Alikuwa mwenye nguvu kisiasa,kijeshi,kijamii na kiuchumi,lakini dhaifu sana wa kuzuia tamaa ya ngono katika nafsi dhalili iliyovikwa mifupa na misuli iliyokakamaa ndani ya suti safi na tai!
Alitoa nyongeza ya mshahara na kumpandisha vyeo kidosho wa Kiarabu,Shaha Ali Riza,hadi Kamati ya Maaadili ya WB ilipomsitukia.
IMF na WB ndizo Taasisi za kikoloni zilizobaki uiburuza dunia leo,wakikemea umasikini,rushwa,utawala mbaya,kumbe wao hususan vigogo hawa walikuwa dhalili katika medani ya ngono hadi wakatoa rushwa kwa vimwana,mwingine akabaka binti wa usafi hotelini!
Shaha Ali Riza(sasa 59) alipendana na Walfowitz tangu wakifanya kazi Pentagon, hawa ndiyo walichochea mambo hadi Saddam Hussein akapinduliwa na kuuawa huko Irak.
Huyu mama,wakati huko kidosho wa Kiarabu kutoka Tripoli,Libya alikozaliwa mwaka 1954,akaja kupata uraia Uingereza na akahamia Marekani.
Huyu binti wa Kiarabu alifanya MZEE Walfowitz kuachana na mkewe wake,na SHAHA Ali Riza naye aliachika kwa muwewe mwaka 2005.Hili ni penzi la wizi.
“Maji yaliyoibiwa ni matamu na mkate ulioliwa kwa siri ni mithili ya asali” Mithali 9:14-18.
Mzee wa watu alipagawa kwa penzi la mtoto wa Kiarabu,naam penzi la tashtiti; akampandisha mshahara Shaha Ali Riza hadi Dola za Marekani 180,00 bila kodi kwa mwaka nzima.Fedha hizi leo ni sawa na shilingi milioni 288 kwa mwaka bila makato ya kodi.
Naam, silikiza shairi hili: “Mtu chake apendacho, hakina ila machoni,
                                              Huridhika kuwa nacho,japo hakina thamani,
                                              Mapenzi hayana kificho,yaamkapo moyoni,
                                              Mwenye mapenzi haoni,ingawa anayo macho!”
Walfowitz, alikuwa haoni wala kusikia kwa kidosho huyo wa Kiarabu,akampandisha mshahara kutoka Dola za Marekani 132,660 hadi 193,590 kwa mwaka.
Hizo ni kama sh.milioni 309,744 kwa mwaka na hakuna kodi.Kidosho alitafutiwa kazi Benki ya Dunia baada ya kuhamishiwa huko kutok Pentagon,akapandishwa mshahara mkubwa,kwa sababu, “MKUBWA ANATAKA!”.
Watumishi wengine kuona hivyo wakaja juu,wakalalamika sana ingalikuwa TANZANIA yangezuka maandamano na watu kuchoma moto magari na nyumba za CCM!
“Maji yaliyoibiwa ni matamu na mkate ulioliwa kwa siri hupendeza” Mithali 9:17.
Alipoulizwa na Kamati ya Maadili ya WB,akajibaraguza hivi na vile,wafanyakazi wakasema anawakatisha tamaa anawashuha moyo wa kazi kumpendelea mshushu wake namna hiyo!
Kupewa U-Boss na kuanza kumwita mshushu wake halafu kumpandisha mshahara kwa fujo,huitwa, ‘KAZI NA DAWA!”.
Mke wa Walfowitz ,Clare Selgin, alishastukia sana huba la wizi-mqtumizi mabaya ya madaraka na tamaa ya ngono.
Nakumbuka,mtu mwingine aliyekumbwa na kashfa ya ngono ni William Jerfferson(BILL)Clinton  kwa mwanamama Yule Monica Lewinsky-The Monicagate!
Hapa kwetu,Maprofesa wanaopigia kelele kuporomoka kwa ubora wa elimu, wana kashfa ya kuwatunukia digrii wasichana vigori wanaowapa ngono-Naam Digrii za Chupi!!
Jambo hili huitwa, ‘WOMAN POWER’ na limewaangusha miamba wanaume lukuki, akiwamo Samson kwa kimwana Delillah(Waamuzi 16) zama za Wafilisti,siku hizi Wapalestina.
Taifa linaangamia kwa sababu ya udhaifu wa ngono wa akina baba. Hata hivyo ngono iliruhusiwa na Mungu ili kuleta afya na Baraka na aslani siyo laana kama tulivyoona katika mfululizo wa makala haya.
Mungu alimuumba mwanamume na mwanamke(Adam na Hawa) katika Bustani ya Eden, akawaba ashiki ili wafanye tendo la ndoa na kuzaa watoto katika ndioa takatifu.Sizungumzii uzinzi,uasherati,ushoga na usagaji tafadhali!
NGONO,imeruhusiwa na Mungu katika ndoa(Mwanzo 1:26-27 na Mwanzo 2:18).
                                     NDOA NI TAASISI BORA
Mwanaume(Ish) na mwanamke(Ishah) walifanywa kuwa mwili mmoja katika noa ya awali hapo Eden. Ni kwa sababu hiyo tunasema Mungu ni “Romantic” anajihusisha katika mahaba ya wanandoa,na kamwe siyo ngono nje na kabla ya ndoa.
                                 ‘’HONEY MOON’’ SIKU 365?
Katika Biblia,kuna ushahidi wa Mungu kuwashangilia maharusi wakati wa Fungate. Mungu alibariki ndoa ya Adam na EVA,Ibrahim na SARAH,Isaka na Rebecca,Yakobo na Rachel n.k
Mungu huridia ngono katika ndoa, “Married sexuality”.Katika zama za WAISRAELI maharusi waliruhsiwa kuwa na fungate(Honey moon) kwa mwaka mzima! Tazama Kumbukumbu la Torati 24:5).
MUNGU napinga ngono miongoni mwa watu wasiooana,na watu wa jinsi moja(hommosexuality) kwamba kuna madhara ya kiafya na kiroho na kiakili. Ngono holela ni hatari zaidi,tumeona walioruhusu mapenzi ya wizi kupokonywa wadhifa mtukufu,kupoteza mapato na kuishia kushitakiwa kwa kesi za ubakaji.
Jarida la New African la Julai 2011,liliandika makala ndefu, ‘WOMAN POWER’ kueleza hatma ya ushawishi wa akina mama kupitia athari za kingono,hususan kwa watu wakubwa hapa Barani Afrika.
Jarida hilo lilisema kwamba, mama anapomtunuku vizuri mzee unyumba, awapo katika nafasi nyeti serikalini hufanya vema,lakini mvuto mbaya wa mama husababisha majanga katika taifa zima.
Wapo wakubwa wenye ‘Pepo la Ngono’ ambao mwisho wa siku wameipeleka nchi husika katika dhahma.
Jacob Zuma Mushorozi,Rais wa Afrika ya Kusini, yeye amejitwalia vimwana watatu na anampango wa kuongeza mwingine na alikwishataliki mwingine-watu wengi humwita ‘Kijogoo’.
Wakeze ni Nonmpumelo Ntuli,Thobeka Mabhijja, na Sizakele Khumalo huyu ni Bi mkubwa.
Ameachana na Nkosazana Dlamini Zuma, ambaye sasa ni Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika(AU) jijini Addis Ababa.
Ana kashfa tele za ngono hata kujamiana na wenye virusi vya Ukimwi;na hudhihirisha udhaifu wa mwanamume rijali kwa ngono.
Mfalme Muswati III anaoa kigoli mpya kila mwaka; na anawake dazeni na ana mpango wa kuoa.Sijui anawaza ngono mara ngapi kwa mwaka!
Robert Gabriel Mugabe(RG)mkewe,Grace anakula sana maraha, inasemekana ni mwenye sauti chumbani hata Ikulu ya mjini Harare! Mzee anahusudu sana ‘Romantic Life’ kwa mkewe,sawa.
Lucy Kibaki, akiwa ‘First Lady” katika ikulu ya Nairobi, aliwahi kuwachapa makonde vigogo wengi na akabomoa hata makompyuta ya magazeti kwa kumwingilia mambo yake.
Ifuatayo ni orodha ya baadhi ya vigogo hapa Afrika na wake zao:
Patience,ni mke wa Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria,kule kwenye Boko Haram.Mke wa Rais Blaise Compaore wa Burkinafaso ni Chantal na mke wa Ange-Felix Patasse wa Afrika ya Kati ni Angele.
Wengine,orodha yao katika mabano ni;Yaya Jamme wa Gambia(Zineb),Bingu wa Mutharika(Callista),Abdulwaye Wade zamani rais wa Senegal(Viviane),Bai Koroma wa Sierra Leone(SIA);Obiang Nguema Mbasongo wa Guinea ya Ikweta(Constancia);na aliyekuwa Rais wa Kenya,Kibaki(Lucy) na Waziri Mkuu wake Odinga(Ida).
Wengine wake za wakubwa ni Chantal Biya(Cameron),LoboTraole(Mali),Djibo Aizouma(Niger),Janet Museveni(Uganda),Sylvia Bongo(Gabon),Tekber Ould Ahme(Mouritania),Monique Bozize(CAR),Antoine Sassou Nguesso(Brazaville),Chantal Yayi Boni(Benin),Casta Bruni mke wa Sarkozy,Thandiwe Banda(Namibia),Maria de luz Guebuza(Msumbiji),Mathato SARAH Mesili(Lesotho),SIA NyamaKoroma(Sierra Leone),Anna Dos Santos(Angola) na Inkoskat Lambikiza(SWAZILAD)
Mke wa hayati Yar’Adua wa Nigeria ni Turai, na mke wa Hayati Meles Zenawi wa Uhabeshi ni Azeb Mestia.
Mke wa Rais Joseph Kabila ni Marie-Olive, Salma Kikwete ni mke wa Kikwete na Graca MACHEL alikuwa mke wa Samora kasha akahamia ikulu ya Afrika Kusini zama za Mandela.
Mke wa Laurent Gbagbo ambaye sasa yuko The Hague ni Simone Gbagbo na mke wa Jerry Lawrings ni Nana,mke wa Obama ni Michelle n.k
Naam, wake wengi wa Marais, ‘First ladies’ wamezitumbukiza nchi katika majaga kwa kupenda starehe na kutumia ushawishi wa ngono kuwageuza ‘wazee’. Ndivyo ilivtotokea kwa Mfalme Suleyman na Ahabu kwa Yezebeli.
Kwa kutumia vibaya ushawishi wao,”WOMAN POWER’ akina mama wanaweza kuleta Baraka ama laana kwa dunia.
Ngono kwa wanandoa ni zoezi linalodumisha ndoa ni upendo na kichocheo cha furaha na faraja(Mithali 5:18,19 na 1Wakorintho 7:2-5).
Aina hii ya upendo ama ashiki miongoni mwa wanandoa, ‘sexual drive’ huitwa kwa Kigiriki, Eros,
Ngono takatifu ni baina ya mume na mke katika ndoa,kwa wafanyao ngono nje ya ndoa au kabla hujikuta katika madhara makubwa ya kiakili.
Mazoea ya ngono chafu “Sexual Addiction” huleta uchungu na chuki na masikitiko makubwa hata kuleta kifafa,magonjwa ya moyo,msongo wa mawazo n.k
Mungu amepiga marufuku uzinzi na uasherati(Mithali 5:3-20 na Mithali 9:13-18).
Kapiga marufuku pia picha za ngono mitandaoni(pornography and cybersex).
                     AINA NNE ZA UPENDO
Nimejadili katika mfululizo wa makala haya madhara hasi ya ngono nje ya ndoa ama kabla ya ndoa. Mapenzi na harara huitwa wa Kigiriki, Eros ama Erao.
Erosm ni tamaa za kimwili hutoweka pindi tendo la kingono linapokamilika. Hii harara ama ashiki(strong sexual drive ama Desires) siyo upendo wa dhati ni tamaa.
Kuna upendo wa kitoto,Storge,wakati Eros ni sexual love, upendo wa kingono,storge ni upendo wa watoto wadogo kwa mtu kufuatia fadhila,zawadi,ahadi,pesa,chakula n.k
Eros hupatikana katika Biblia,katika Mithali 7:18-23 na Methali 30:16.
Aina nyingine ya upendo huitwa,Philia kwa Kigiriki.Philia maana yake ni kumfikiria sana mtu,kumhitaji sana kama ilivyo mke kwa mume ama mume kwa mkewe na watoto wao-huu ni upendo wa familia.
Kupenda sana pesa ni eros na wakati mwingine ni storge hususan kwa machangudoa ambao hupenda sana pesa na hawajali mtoa pesa-hupenda zawadi,mtoa zawadi hawampendi!
Tumeona aina tatu za Upendo;Philia,Eros na Storge; upendo wa aina zote hizi hufika ukingoni hatimaye faida ama kinachotarajiwa kinapotoweka,
Huu ni upendo wa faida,huisha misisimko inapotoweka na kupisha uchungu na majuto,pesa zinapomwishia ‘Buzi’ basin a upendo huo hufika kikomo.
Tujadili kidogo aina ya upendo uitwao,Agape ama Agapao.
Huu ni upendo usio na faida au lengo la kujipatia chumo la faida na manufaa. Huitwa upendo huria.
Kwa Kiebrania mahaba aina hii Agape huitwa,Ahaba!
Ahaba, ni upeno huru usioshurutishwa na uzuri wa mtu,urembo,mwili wa kusisimua,tabasamu tamu mithili ya asali ama fedha na cheo n.k
Upendo huru,  Impartiality Love, ni upendo wa kujitolea mhanga. Ni mithili ya mshumaa unavyojiteketeza wenyewe wakati unapoangaza wengine!
Mshumaa huangaza wengine wakati unapojiteketeza wenyewe,nah ii ni kujitoa kafara, “Sacrificial Love”.
Wakati ashiki, sexual drive ama sexual desires huishia mahali ngono inapogeuka chungu na majuto mjukuu, wakati Philia ya wanandoa inapotoweka, wakati baba anapobaka bintiye na kumtia uchungu,Agape haina mwisho wake wala kujuta!
Wakati ndugu wanapogombana na kuapizana,wakati storge inapofika mwisho mtoto akinyimwa pipi ama maandazi,Agape ni kama ifuatavyo:
Takriban miaka 2420 iliyopita, Mgiriki aitwaye Euripides aliandika kisa cha mahaba ya dhati zama hizo ya mwanamama mrembo sana,ALCESTIS kwa mpenzi wake aitwaye Admetus.
Admetus, alikuwa mfalme tena kijana ‘handsome’ huko Thessaly,Ugiriki.
Wanawake wengi hupenda wanaume wenye sura nzuri,wenye cheo na pesa nyingi wanaoishi maisha ya fahari sana-wanataka kuangukia kunako pesa.
Admetus,yeye alipatwa faradhi,aliugua sana wazazi wake wakaenda kuiuliza miungu na mizimu yao kwamba kifanyike nini ili apone?
Miungu ikasema Admetus asingepona hadi apatikane mtu mwingine wa kufa badala yake(substitute).
Admetus akiwa mgonjwa sana akamwomba babaye afe badala yake,akakataa.Alimwomba mamaye afe badala yake, akagoma!
Hakuna aliye tayari kufa badala ya mwingine-ndugu,rafiki na jirani walikataa kufa badala ya huyu Admetus,potelea mbali wakose mfalme ni mvulana mfuauji.
Hatimaye,Yule kidosho Alcestis alikubali kufa badala ya Admetus,kwa kuwa alimpenda sana kuzidi upendo tuliojadili hapa.
Alcestis alimpenda Admetus hata akajitoa kafara “sacrificial love” akafa badala ya Admetus.
Baada ya msichana huyu mrembo kufa badala ya Admetus, alipona lakini akaomboleza hivi:
“Nitakuombolezea sana oh waridi wa moyo wangu,siyo kwa mwaka mmoja,bali maisha yangu yote!Sitamjali mama wala baba yangu wala ndugu na rafiki zangu-walinipenda kwa midomo bila upendo wa myoyo-the love indeed!
Upendo wa maneno matupu! Upendo halisi ni ule wa wakati wa dhiki.Waingereza wanasema ‘To give oneself for another’ ili kuwaangaza wengine unapojiteketeza.
Mtume Paulo aliyenyongwa na Kaisari Nero,baada ya kubambikwa makosa ya kuuchoma moto mji wa Rome mwaka 64 AD,akaandika hivi:
“Ni shida mtu kufa kwa ajili ya mtu mwingine,lakini yawezekana mtu kuthubutu kufa kwa ajili ya mtu mwema(kama Admetus);KristoYesu alikufa kwa ajili yetu tulipokuwa tungali Adui zake!”Warumi 5:7-10.
Mwenye haki(Yesu) alikufa kwa ajili ya adui zake wenye dhambi-huu ndiyo upendo wa dhati wa mtu kufa kwa ajili ya asiye na maufaa kwake.
Wenye kujitoa mhanga kwa ugaidi hufatana na ahadi na manufaa na kamwe siyo Agape. Agape ni upendo uso na sababu za faida ama chumo,ni Impartiality love.
Akina dada na akina kaka yapimeni sana maneno ya ya ghiliba ‘Nakupenda sana’ kumbe uongo mtupu, inapendwa pochi yako ama unadanganywa ili utumiwe kasha utupwe mithili ya ganda la muwa!
Tamaa za ngono akilini mwa wanaume zimetamalaki, kila wakati wanaume hufikiri ngono lakini hawana upendo. Tamaa ya ngono si upendo ni tamaa ‘lustiful’ siyo kupenda
0713 324 074
 
 
 
 

No comments:

Post a Comment