Tuesday, June 25, 2013

MLA NYAMA ZA WATU



JEAN BEDEL BOKASSA,alizaliwa Feburuari 20 mwaka 1921 huko Afrika ya Kati,Central African Republic(CAR).
Ni mmoja wa madikteta wabaya Barani Afrika, ambaye alipinduliwa Septemba 20 mwaka 1979 na David Dacko. Mwaka 1979 ulikuwa mwaka wa mapinduzi dhidi ya Madikteta,akina Amin Dada wa Uganda, Marcius Nguema na huyu Bokassa.
Baada ya kupinduliwa alikimbilia uhamishoni kwa rafiki zake Ufaransa, baadaye akarudi nchini na kukamatwa kasha kushitakiwa kwa makosa ya uhaini na ulaji wa nyama za watu-cannibalism.
Alifungwa kifungo cha maisha,kasha akaachwa huru. Mtu huyu alifariki dunia Novemba mwaka 1996. Alianza kama Sajenti wa jeshi la kikoloni; na aliingia madarakani kama walivyofanya madikteta wenzake, akina Amin,Nguema n.k
Ilikuwa Januari mwaka 1966 mtu huyu alipoingia mamlakani, akajitangaza kwamba sasa ni ‘Rais wa Maisha’ mithili ya mtu aliyemhusudu sana, Emperor Napoleon Bonaparte.
 
Mwaka 1977 alitawazwa kuwa ‘Emperor’ kwa sherehe iliyogharimu Pauni za Kiingereza milioni 10,ni kama shilingi za Tanzania Bilioni 25 hivi sasa.Ni kama Dola za Marekani milioni 20 hivi; hadi nchi ikafilisika kabisa!
Fedha hizo zilihusika gharama za kiti cha enzi na taji ya dhahabu iliyonakshiwa kwa almasi.Kama alivyokuwa Idi Amin Dada wa Uganda, Bokassa alipenda sifa, hadi akajibandika nishani nyingi, akajiita yeye ndiye Mhandisi wa kwanza nchini humo, akajiita ndiye mwanandinga nguli kuliko wote katika nchi-The First Footballer.
Amin Dada yeye alijivika vyeo na nishani nyingi, Mshindi wa Dola ya Kiingereza, ‘Victoria Cross’ Mfalme wa Mwisho wa Uskochi n.k tutakujulisha habari zake katika mfululizo huu wa madikteta.
Mmoja wa wakeze alikuwa na kiwanda cha kutengeneza nguo,na maduka yake yakawa yanauza nguo hizi.
Ilitungwa sheria kupiga mtu mwingine yeyote kuuza sare za shule,isipokuwa huyo mama peje yake. Basi, wanafunzi wa shule wakaandamana kupinga kuuziwa sare za shule  kwa bei ghali na duka hilo, wakapigwa risasi wanafunzi 100 hivi!
Baadaye, alikamatwa na kushitakiwa kwa makosa ya uhaini na mauaji ya watoto hawa 100; lakini akaja kuachwa huru.Alishitakiwa pia kula nyama za watu. Tumeona pia Teodoro Nguema akila korodani za wapinzani wake, na Amin alisemwa alikula maini na moyo wa adui zake!
Wafaransa ndiyo waliomsaidia Bokassa kuingia madarakani,na alipopinduliwa na David Dacko alitimkia Ufaransa huko huko hiyo Septemba 20 mwaka 1979, mwaka 1981 kukatokea mapinduzi mengine safari hii chini ya Jen. Andre Kilingba.
Hii nchi ilipata uhuru mwaka 1960, Agosti 13.Hii ni nchi ya almasi,uranium,pamba,kahawa na tumbaku na mataifa kama Wafaransa na Wachina wanainyatia.
Ni nchi ndogo ya watu kama milioni 5 tu wanaoongea Kifaransa, Sangho,Kiarabu,Hunsa na Kiswahili.Nchi ina ukubwa wa maili za mraba 240,200 jirani na Congo(DRC),Sudan upande wa MASHARIKI,Chad na Cameron upande wa Magharibi.
Huyu ndiye Jean Bedel Bokassa, aliyekula nyama za watu huku akijisifia kwa kila sifa.
0786 324 074

No comments:

Post a Comment