Tuesday, August 14, 2012

MBIO,KUTOKA KWA SHETANI ILI KUTAFUTA HIFADHI YA UKIMBIZI KWA PEPO WACHAFU(3)


KIMSINGI,tunakubaliana hapa kila mtu kwamba, sisi tuna matatizo. 
Kila mtu ni chimbuko la shida yake mwenyewe,ingawa ziko shida zinazoletwa na matokeo ya uchaguzi mbaya wa wenzetu.
Mabaya yaliyotendwa na jirani,matokeo yake yataathiri wengine-tunashiriki dhambi na matokeo ya dhambi za watu wengine-corporate sins.
 Hii ndiyo dunia tuishiyo.
Maisha yamekuwa magumu, watu tunakata tamaa, si kwa sababu Mungu kapenda; ni tabia mbaya na uchaguzi wetu wenyewe, wa wenzetu ama sote tunashiriki kuchagua jambo baya,kwa kujua makusudi,au kwa kutokujua. Mungu halazimishi watu kuchagua jambo lolote.
 Mungu hakutuumba kama treni,lisivyoweza kuamua pa kupita,hata kama reli imefurikishwa na maji au imebomoka. Mungu hakutuumba kama misukule ama zombies. Alimuumba Lusifa kama kiumbe mkamilifu, Lusifa akachagua kuasi-Hii ndiyo tamu- chungu ya demokrasia.
 Mmomonyoko wa maasili tunaolilia sasa, haukujileta wenyewe kama mashine inayojiendesha yenyewe, automatic machines,mabaya yanaletwa na mimi,na wewe na mwenzetu mjinga Fulani, n.k
Rushwa, ufisadi,wizi wa mali ya umma,uporaji,ujambazi,ushoga,ulawiti, hata virusi vya Ukimwi na Ebola, vimefanywa kwa mapenzi ya watu wenzetu,wakapandikiza kwa jamii ya sokwe-si Mungu aliyeleta Ukimwi,Ebola na Magonjwa ya hatari.
Sisi wenyewe ndiyo chimbuko la matatizo yetu-kila mtu anachangia kwa kiwango chake,mwisho wa siku, mawimbi madogo madogo ya uhalifu na dhambi huwa mawimbi makubwa yanayogharikisha kizazi chote.
Fanya zoezi hili; nenda baharini inapokuwa tulivu,shwari. Nenda hata ziwani au katika dimbi la maji tulivu,tupa kijiwe kidogo tu ndani ya maji tulivu. Unaona nini? Mawimbi madogo madogo yanatembea pole pole,hatimaye huwa makubwa sana na matokeo yake hatuyajui.
Ukipora mke wa mtu, matokeo ya dhambi hiyo huyajui. Labda watoto wake waliokosa malezi ya mama,watakuwa wavuta bangi,wabwia unga na wezi! Sasa, utalalama, ‘matoto ya siku hizi’ pindi wakikupora mitaani usiku?
Watoto wa mitaani, wametoka wapi? Kosa ni lao wenyewe au la serikali? Ni kosa la nani kama siyo la jamii hii ovu?
Naam, dunia ina shida sasa. Tatizo ni jinsi ya kuondoa shida hizi.Wengine wanapendekeza tupigane vita kama Rwanda(mwaka 1994) au kama Burundi, Somalia n.k
Wengine wanapendekeza itumike njia ya mapinduzi ya kijeshi kuondoa mafisadi! Hawa hawajui, fisadi siyo mtu mmoja-ni mfumo,ni kizazi kiovu,utaondoa huyu, atakuja mwingine mwovu kupindukia.
Kwamba wanaojenga matabaka miongoni mwa walionacho na wasionacho, watu wasio wazalendo, wasiojali utaifa wauawe!
Katika mfululizo wa makala haya,nimetangulia kueleza namna watu walivyowahi kupinga dhuluma katika nchi hii, tangu zama za Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere..
Nimeeleza ndege ilivyotekwa nyara na vijana waziba viraka vya matairi ya gari, wakailazimisha kwenda London.
Tukio hilo la kwanza la aina yake hapa nchini,liliunganishwa na harakati za siasa za Mkimbizi maarufu wa Tanzania, Oscar Salathiel Kambona.
Kambona, akiwa London alikanusha kujihusisha na utekaji nyara ndege hiyo. Baadaye, Kambona alirejea Tanzania wakati wa mfumo wa vyama vingi,mwaka 1992.
Ilisemwa, Kambona hakuwa raia wa Tanzania, alikuwa raia wan chi ya Joyce Banda, anayekuja pupa na atavuna pupa.Ameruhusu ushoga, sasa anataka Ziwa Nyasa-Pato la Pupa!
Kambona hakuzaliwa Malawi. Alizaliwa Agosti 13, mwaka 1928 huko Kwambe,jirani na Mbamba Bay,Mbinga.Ni  Kusini mwa Ziwa Tanganyika. Alikufa baadaye mjini London mwaka 1997,Julai.
 Kwa faida ya wasomaji, iko siku nitasimulia kisa cha ugomvi wa Kambona na Nyerere. Kwanini alikuwa Waziri wa kwanza wa Mambo ya Nje kama Mzee Bernard Membe leo, halafu akaja kusemwa siyo raia?!!
Msomaji,unapaswa kufikiri. Usiwe kama dodoki; unalishwa kila jambo,unakubali na kuanza kulalama,hujui ukweli ni upi.
 Jifunze kufikiri,usijifunze kusema na kusoma!
Tunajadili chimbuko la shida,ufisadi,unyama,rushwa,madaraja kati ya walionacho na makabwela-watoto wa masikini, ambao mwisho ni watawaliwa na watumwa wa milele.
Haya hayako Tanzania tu. Wanaotaka kujitoa mhanga, wasubiri kidogo tuwaambie. Chanzo ni watu kuukataa ukweli,na haki. Nimejadili sana ukweli ni nini,kulingana na mwanafalsafa mkuu wa pili duniani, Aristotle.
Mwingereza, George Orwell, alishaandika kabla sijazaliwa kejeli(satire) iitwayo SHAMBA LA WANYAMA.Aliandika kuhusu viongozi waliochaguliwa kuanza kujiona wao ni bora kuliko wananchi wanaoongozwa. Kumbuka aliandika yaliyotokea Uingereza, siyo Tanzania.
George Orwell, aliandika namna viongozi wa SHAMBA LA WANYAMA, akina Mzee Nguruwe, walivyoanza kukiuka AMRI,Katiba,makubaliano waliyojiwekea, wakaanza kushibisha matumbo yao, bila kujali raia.
Hizo Amri zilizomo katika Animal Farm ya George Orwell,ndiyo MAADILI tunayosema yameporomoka.
 Nani hutaka kufuata sheria pasipo kushurutishwa?
 Asilimia 30 ya watu hufuata sheria kwa sababu polisi,wapo na mahakama zipo na sheria ni kali. Asilimia 65 ya watu hawataki kutii sheria hata mahakama zikiwepo na polisi wakiwepo.
 Ni asilimia 5 tu ya watu walio tayari kuishi maisha adili hapa duniani hata kama mahakama na polisi wasipokuwepo. Mtu hakulipi haki yako hadi umburuze kortini?
Yooo! Mawe!! Halafu mnasema maadili! Kutii bila shuruti. Kutii taratibu,kanuni za maisha,kufuata sheria-bila shuruti, unazifuata?
Maadili ni nini?
 Maadili,kwa Kiingereza, “ETHICS” katika Uandishi wa Habari kwa mfano,ni Kiwango cha ubora wa Tabia kilichowekwa ili jamii ifuate na kuishi hivyo.
Kwa Kiingereza, Ethics is a Standard of Behavior. Maadili ni tabia njema.Sasa jifunze kufikiri vizuri kwa kichwa, siyo kwa tumbo. Maadili mtu huzaliwa nayo?
Kila mtu ana kiwango bora cha tabia? Unakuwa na kiwango bora cha tabia kutoka wapi?
Viongozi wa dini wanataka viongozi wa serikali wawe waadilifu; wawe na kiwango bora cha tabia njema-A high standard of Behavior!
Viongozi wa dini,ni waadilifu? 
Wanataka watu wengine wawe waadilifu sana, wakati wao sasa ni kituko,ni waovu sana,wako chini ya kiwango cha ubora wa tabia njema.
Wanataka mtu mwingine ashike maadili, sheria,kanuni ambazo wao wamezihalifu sana. Huu ni unafiki, Ufarisayo,ushetani na upofu-soma Mathayo 23:13-36.
Maadili mema,huletwa na mtu kujitambua kati ya mema na mabaya.”
To distinguish between Right and Wrong, or in some cases, between two wrongs”
Sasa,nani atakuwa tayari kusema ubaya kwa jina lake halisi na ukweli kwa jina lake halisi?
Si ndiyo siasa hizi? Mnatambua makosa,mbona mwatetea watoto kuwa mashoga? Nani anawajibika kwa makosa yake?
Maadili,maanayeke ni kila mtu kuwajibika kwa kosa lake.Wajibu ni deni.Wajibu ni kila mtu kuwa na deni-Under Obligation-Wanaoongoza kulaumu wenzao, hawatambui wajibu wao,ila kusukumia wenzao lawama. Mtu mzembe,fisadi, ni mwepesi na fundi wa kukosoa-Criticism.
Alhamisi,Aprili Mosi mwaka 2010,gazeti la Rai liliandika makala yenye kichwa, “Matendo ya ‘kishetani’ yalichafua Kanisa Katoliki”.
Makala hiyo iliandika tabia ya makasisi wa Kanisa Katoliki kulawiti watoto wa kiume,wanaosoma katika shule za kikatoliki duniani.
Papa Benedicto XVI amekuwa akienda kila mahali duniani na kuomba radhi kwa matendo hayo.
 Kuomba radhi hutokana na kukiri makosa-yapo yanatendeka kweli,na amewaomba msamaha waathirika, siyo wahanga.
Sasa, wasikie makasisi wa Kanisa hilo wanavyomkosoa sana Rais Kikwete na serikali yake kwa ufisadi,utadhani ufisadi ni kupora fedha za umma tu,kumbe na kulawiti watoto chekechea ni kitu gani? Soma Wagalatia sura ya 5.
Siyo Kanisa Katoliki tu,takriban viongozi wa dini zote,wengine hujiita Manabii na Mitume,wachungaji sijui watumishi,masheikh,maimam- miongoni mwao ni wakora, matapeli na mawakala wa shetani.
Ni waporaji wa zaka na sadaka za waumini,wanajilisha na kondoo wa Bwana wao, wanachagua kondoo walionona, wanakula polepole, wamevunja ndoa za watu n.k
Juzi, nikisikiliza highlights za magazeti,nikasikia Kiongozi mmoja machachari anayefanya miujiza hadi anafananishwa na Mungu, anashitakiwa na waumini wake kufakamia mali ya kanisa kama yake binagsi!!
Jamani, anaikosoa serikali huyu hadi anataka ipinduliwe! Sasa unajiuliza: Hini ‘Unethical Practices” ni nini kama siyo wizi,utapeli, ulawiti,uzinzi,uporaji wa zaka na sadaka za waumini n.k?
 Nadhani, hata viongozi wa kidini akina Vibwetere hawa,hawajui Dhambi ni nini? Hawajui kwamba Dhambi ni Uasi wa Sheria ya Mungu(Amri 10 zinazokataza uongo,wizi,uzinzi na ufiraji).
 Gidion M. anaandika kwamba hawa jamaa wa dini hutumiwa na Freemasons,halafu wanakuwa wakali kama pilipili.
Sijasema wasiikosoe serikali. Nasema hawa wanajidai kuujua ukweli,mbona kuna kashfa hizo hadu juzi BBC wametangaza Vatican inamburuza jamaa mahakamani kwa kuvujisha siri za wizi! Naam, ufisadi Vatican?
Ukitazama kwa jicho la tatu, sasa utaona si viongozi wa dini, siyo wanasiasa wala jamii sote tumeoza-mafisadi tu-Soma Wagalatia sura ya tano.
Waandishi wa habari na wahariri wao ni matapeli,iko siku nitasema ukweli.Manabii na Mitume wa siku hizi ni wezi kuliko Yule wa Msalabani. Jamii imechafuka sasa.
 Robert Charles Darwin, alisema kila mwenye nguvu ndiye anayekula leo,wengine tunanyauka. Mbuzi hula kulingana na urefu wa kamba yake;kamba ni madaraka,cheo hata cha kanisani na msikitini-ni uporaji tu,kila Nyanja.
Hii Falsafa ya Darwin ya Survival of the Fittest, inawafanya watu maskini kugeuka mbolea ya kuwastawisha wakubwa na matajiri hapa duniani.
Siku hizi hata makanisani na misikitini,ni kugombea madaraka-supremacy struggle-hakuna anayekubali alichosema Mungu, Amri za Mungu, maadili,uzalendo,upendo,unyoofu n.k Sisi sote tu waovu,wachafu,hakuna wa kujigamba.
Hakuna wa kumcheka mwenzie,tujisahihishe,tumeacha MAADILI.
Maadili ni Ethics kwa Kiingereza. Waingereza wanasema, Ethics is a system of principles that guides your conduct and helps you to distinguish between Right and Wrong.
Nguvu inayomtambulisha mtu mazuri na mema,ni ya Roho Mtakatifu, sasa hawa jamaa wa dini hawana Roho Mtakatifu,bali Roho Mtakavitu!
  Kutambua mema na mabaya huja kwa njia ya SHERIA YA MUNGU,sheria ya Mungu, Amri 10 za Mungu ni kioo cha kutuonesha tongotongo!
Tumekataa Amri 10 za Mungu tangu ngazi ya familia,tutakuwaje raia wema,viongozi wema au tukapa rais mwema?
Sisi ni waovu, hatutaki ukweli na haki. Nani atunza sheria ya Mungu moyoni?
 Tumebaki kulalama,na kutafuta kugombana kwa vita ili kuondoa shida miongoni mwetu. Hii wanafalsafa wanasema ni kutafuta njia ya kumkimbia Shetani kwa kuomba hifadhi ya ukimbizi kwa Lusifa!
“Looking  a way from Satan, and seeking refuge from the Devil!”
Itaendelea
0713 324 074





No comments:

Post a Comment