Tuesday, September 17, 2013

AKINA KAGAME



              


ilikwenda mahakamani?
    Wapo watu wanadhani mtu kushinda uchaguzi ni kupata kura nyingi za umaarufu(Popular vote); na wengine wanadhani Rais mzuri ndiye aliyependwa saana.
 Rais mwema anamjua Mungu.
Mfalme Sauli alipewa kura nyingi na Waisraeli wa kale kwa sababu tu alikuwa mrefu na ‘handsome’ lakini akaja kuboronga sana na kukiingiza kizazi katika ushirikina mkubwa… Mungu hafuati urefu wa Mfalme wala kura nyingi za wapigakura mbumbumbu.
    Wala safu hii haitetei wizi wa kura wa Rais yeyote.
Isipokuwa, ni vigumu Rais wan chi moja kuanza kumkosoa mwenzake.
Hapa kwetu kuna madai ya wizi wa kura yaliyotolewa hata kabla ya uchaguzi wa Kenya .
 Kibaki alimkosoa Rais Karume au Mkapa?
   Mseveni mwenyewe alidaiwa kuiba kura Uganda na kumsweka rumande Kanali Dk Kizza Besigye.
Kibaki alikosoa udikteta huo wa kumsweka rupango mpinzani wa Museveni?
    Forum for Democratic Change(FDC) cha Dk. Besigye, kimekuwa kikilalamika kwa kufanyiwa mchezo mchafu na  National Resistance Movement.
Rais gani hapa Afrika aliyekataa kutambua ushindi wa Museveni; na kutambua ule wa wapinzani?
    Wafuasi wa Besigye jijini Kampala walipata kupigwa mabomu ya machozi na risasi za mipira hata za moto, walipopinga kukamatwa kwa kiongozi wao.
 Rais gani alimkosoa Museveni hadharani, achilia mbali kutotambua ushindi wake halali toka kwa Tume yake ya Uhaguzi?
 Kuna suala la Dk. Kiza Besigye kuzuiwa kwenda kazini kwa miguu,maarufu ‘Walk to Work” ambalo limeleta sana shida mjini Kampala.

          Makomandoo wa Rais Museveni, Black Mamba Urban Hit Squad, waliwahi kutinga Mahakama Kuu ya Kampala na kuzingira, Kanali Besigye alipoomba dhamana.
Ilikuwa kitisho kwa      Majaji.
Wee Black Mamba wamezingira kiti chako utajidaije kumpa haki mpinzani? Kampala ni undava-undava!
    Dikteta Nduli, Joka Kuuu, Idi Amin Dada, aliwahi kutuma makachero wa Ikulu, The State Research Bureau, wakaingia mahakama hiyo Kuu ya Uganda , na kumkamata Jaji Mkuu, kisha kumtia ndani ya buti ya gari yao na kutoweka naye. Hakuonekana hadi Amin anazikwa Saudi Arabia.
   Sasa Majaji wangefanyeke kazi katika mazingira haya?
Ilibidi baadaye wagome tu, halafu Rais Mseveni akaomba radhi.
Kumpa haki mpinzani siyo rahisi. Viongozi wetu ni wababe sana ; hata wao kwa wao huogopana. Wee Bush akishindwa hata kura ya maoni Irak, utasema kashindwa? Thubutu.
    Naam, nampenda Jenerali Kaguta Museveni, ni kiongozi wa wenzake katika Shirikisho letu la EAC. Tena basi, Museveni ni mzoefu wa siasa kuliko Kibaki, Kikwete labda na Raila Odinga.
    Kushinda na kushindwa uchaguzi yeye ndiye anayejua zaidi kuliko hawa wengine.Ni na hofu na mkuu huyu kuongoza Afrika Mashariki(EAC) na kupatanisha migogoro hapa Maziwa Makuu.

       JENERALI MUSEVENI NI NANI?
Aliwahi kushindwa ubunge, kwao.
Chama chake cha Uganda Patriotic Movement kiliambulia kiti kimoja tu, ingawa kilisimika wagombea 44.
Akaanzisha mapambano ya msituni dhidi ya serikali Desemba 1980.
    De Mabior, Samora wamekufa kifo kimoja cha ajari za ndege.
Kabila aliuawa Ikulu ya Kinshasa mwanzoni mwa 2001 tena na mlinzi wake, ambaye naye alilimwa risasi.
    Museveni ni mwanasiasa kwa kusomea. Ana shahada ya UDSM.Licha ya kujua mapinduzi ya kijeshi, amekuwa waziri wa Ulinzi tangu 1979 katika serikali ya Yusuf Lule.
    Museveni ameingia madarakani Januari 26, mwaka 1986 akamtoa Marehemu Jenerali Toto Okello.
Ninachotaka kusema ni kwamba, Jenerali Museveni si mbumbumbu hata atambue ushindi wa siasa hapa Afrika Mashariki,na anajua si vita vya msituni tu,bali hata fitna,kupindua serikali na kuwaweka madarakani akina Kagame n.k
   Naam, amesoma siasa na kuhitimu chuo kikuu. Ameshiriki mapambano ya kudai uhuru, ameingia msituni na kupindua serikali. Sasa amebadili Katiba ili asalie madarakani tangu hiyo Januari 29,mwaka 1986 alipoapishwa kuwa Rais wa Uganda .
    Wenzake akina Samora, de Mabior na Kabila wamekufa yeye yupo madarakani.
    Mtu aliyesoma sayansi ya siasa(Political Science) na kuhitimu miaka hiyo ya 70 UDSM, atakuwaje mbumbumbu wa kushindwa kujua mshindi wa uchaguzi hata Marekani, achilia mbali Nairobi ?
Ndiyo maana Kikwete kamwambia kumshauri Kagame aache jeuri hapa Afrika Mashariki,yeye ana madaraka ‘chakupewa’ toka mbawani mwa Museveni!
   Mtu ambaye majeshi yake yamewahi kuingia Kongo na kuchapana na majeshi ya  mshirika wake wa siku nyingi, Meja Paul Kagame, Rais wa Rwanda , hukohuko Kongo; hajui nani  mwenye Afrika Mashariki?

          JENERALI PAUL KAGAME NAYE NANI AFRIKA MASHARIKI?

    Paul Kagame alikuwa katika Jeshi la Museveni wakati wa mapambano ya msituni.
Kagame alitoka msituni akaenda Marekani kusomea medani ya kijeshi, kabla ya kuitwa kuwaongoza RPF.
    Jenerali Museveni aliyemsaidia hata Kagame kutawala Rwanda si mwanafunzi wa siasa za Afrika kama wengine wanavyomfananisha kijiweni.
Anapotaka kuwa Rais wa kwanza wa Shirikisho la Afrika Mashariki(EAC) anajua na habahatishi.Watu wawe makini na wajue maslahi ya akina Museveni,Kagame na wenzake hatutawataja hapa.
Anapopeleka majeshi yake Congo,bila shaka kupora madini na pembe za ndovu huko,inajulikana anachofanya! Hujui pesa za magendo hufanya nini?
    Naam. Jenerali Museveni anamjua Raila Amolo Odinga. Anajua kuwa naye si haba. Odinga aliwahi kukimbilia hapa Tanzania  akiogopa kutiwa mbaroni kufuatia harakati zake za siasa. Odinga na Museveni wanajuana.Wameishi hapa-hapa kwetu ni kimbilio la hapa ambao leo wanajidai kutudhaharu!
Odinga aliwahi kutuhumiwa kwa kesi za uhaini zama za Rais Moi.
   Odinga ni Mhandisi na si mwanajeshi.
 Museveni ni mwanasiasa wa kusomea Chuo Kikuu na ni mwanajeshi wa cheo cha ‘General’.

      Jenerali Museveni(69), amebaki pekee mkongwe katika siasa za Afrika Mashariki.
Anajuana vilivyo na Bush na Gordon Brown,Nick          Clegg,Obama na wengine,
. Malkia Elizabeth II katoka  mjini Kampala kuhudhuria mkutano wa Commonwelth. Miaka michache iliyopita.
 Museveni anaijua Afrika Mashariki kuliko Kagame. Amepigana vita msituni Tanzania,Uganda,Musumbiji dhidi ya Wareno na ndani ya Congo!
Hata hivyo,Museveni na Kagame wamefanikiwa sana kufuatia urafiki wao na Marekani.Wasije wakamsahau Charles Taylor.
   
.

CHARLES TAYLOR, Rais wa zamani wa Liberia ambaye sasa anafungwa jela miala 50 baada ya mashitaka ya uhalifu wa kivita, alikaririwa na gazeti la Africa Now la Mei mwaka juzi 2011, akisema: “Boss wako anapokuwa adui yako, umeangamia!”

Taylor, alikuwa akizungumza na gazeti hilo kueleza hisia zake jinsi Dunia leo ilivyo katika hatari kuliko hata kipindi cha Vita baridi.

Hata hivyo, Taylor anayataja mataifa makubwa kama ‘ Mabwana wakubwa’ wanaoitawala dunia ya utandawazi kwa kutumia nguvu zao za kiuchumi, kijeshi na hata kwa kutumia Taasisi za Fedha kama IMF, Benki ya Dunia na Shirika la Biashara WTO, kuukandamiza Ulimwengu.

Kulingana na Taylor aliyekariri kauli ya Waziri wake wa Habari, kwamba “Bwana Mkubwa (Boss) anapokuwa adui yako, umeangamia”, alikuwa akiilenga Marekani inavyouburuza Ulimwengu, bila kuogopa ,upinzani toka Umoja wa Mataifa (UN) au hata kutoka nchi za Mashariki, kama ilivyokuwa kabla ya Vita baridi kumalizika miaka ya 90.

Tunatanguliza maneno haya kwa moyo wa unyenyekevu, kueleza hali halisi ya Ulimwengu tuliomo, ambamo gazeti kama hili haliwezi kuepuka nguvu zilizotajwa na Charles Taylor.



 Msomaji wetu mmoja, Pierre Kumaro, aliyejitambulisha kama raia wa Rwanda, aishiye Dar es salaam, amelalamika kama kichwa cha makala hii kilivyosema!

Pierre Kumaro,alimwandikia mwandishi wa makala hiyo barua pepe ambayo tutaichapa hapa chini , ili wasomaji wetu wenye mchango wao wasiache kutoa maoni yao kupitia gazeti hili linalodhihirisha kuwa ni jukwaa halisi la kusemea wanyonge, tangu Tanzania, Rwanda, Burundi, Nigeria , Congo na hata Iraq!

Jambo moja ambalo lazima wasomaji wetu na wenye mamlaka za kisiasa na kisheria wanapaswa kuweka maanani, ni kwamba maoni ya Pierre Kumaro, siyo msimamo wa gazeti hili, kuhusu mgogoro wa Rwanda wa mwaka 1994, uliopelekea mauaji ya Kimbari.

Kwa upande mwingine, sheria zinazokataza “kumtukana” rais wa nchi rafiki (kama Rwanda, Kenya, Burundi, Uganda, Marekani, Uingereza n.k) kwa namna yoyote, zisitafsiri maoni ya raia wa Rwanda kama kashfa.


“Kwa nini unaandika mambo ya mbali, ukasahau mtu kama Paul Kagame wakati ndiye wa karibu?
Ninyi Watanzania mnaogopa kuandika mateso ya Wanyarwanda wanayopata sababu ya ‘ Kibaraka’ Kagame!

Au hamjui, ama mmepewa kitu kidogo…mnaandika mateso ya Iraq, Liberia, ya Rwanda hamtaki kuwajulisha Watanzania! Hebu wewe niambie , kama umewahi kusikia maandamano ya chama cha Upinzani Rwanda; au mkutano?

Jiulize: Rais wa zamani anawekwa ndani,eti anataka kuunda chama!
Jiulize: Rwanda wanapata wapi silaha za kupigana hadi kukamata Congo(DRC) nzima. Jiulize, tangu rais Paul Kagame awekwe madarakani (Meja Paul Kagame aliapishwa rais wa Rwanda Aprili 22, mwaka 2000)na Marekani ,ukiwa Waziri Mhutu, ukimaliza tu  mhula wako ni jela au ukimbilie nje, la sivyo unakufa!

Nashangaa sana Tanzania… jinsi wanavyotuonea sisi Wahutu, hamtaki kuweka mambo hadharani! Sasa hivi kuna mtu, mwezi uliopita alikuwa Arusha kwenye Mahakama ya Umoja wa Mataifa(ICTR), alikuwa Mlinzi wa (Rais Paul) Kagame,alisema namna Kagame alivyotoa amri ya kuangusha ndege iliyomuua (Hayati Rais Juvenal) Habyarimana”.

(Marehemu Habyarimana ambaye alikuwa Mhutu, na Rais wa Burundi, Cyprien Ntaryamira, waliuawa katika ajali ya ndege ambayo hadi sasa chanzo chake ni siri, Aprili 6, mwaka 1994.

Walikuwa wakitoka Dar es salaam kwenye mkutano wa usuluhishi wa migogoro ya nchi zao. Walipanda ndege moja, na ndipo ajali hiyo ilipotokea. Ntaryamira alichaguliwa rais wa Burundi Januari 1994, akafa Aprili mwaka huo.

Wakati Habyarimana alikuwa ametoka kutiliana saini mkataba wa Amani na Waasi wa Kitutsi wa Rwandan Patriotic Front(RPF) Agosti 1993. Baada ya ajali hiyo, yalianza mauaji ya Kimbari yaliyochukua maisha ya watu 800,000!)

“Yeye (Kagame) alishiriki mia kwa mia”, Pierre ameendelea kusema “Mtu huyo(Mlinzi wa rais Kagame) alitoa ushahidi wa kutosha, lakini Mahakama ya Arusha inakataa kumkamata, kwa sababu Marekani hawataki! Kwa nini vitu kama hivi msiandike? Wakati vipo hata kwenye internet?

Watutsi, walioua watu Congo hadi leo, eti wanasema kuna Wanyamurenge! Wanyamuremge wako wangapi Congo, wakati ni Wanyarwanda watupu! Wewe (mwandishi) nenda Ubalozini, uwaulize ni wafanyakazi wangapi Wahutu?

Wote, kuanzia Balozi ni Wahutu hapa Dar es salaam. Walinzi wawili tu (wa Ubalozi) ni Watanzania; wengine ni Watutsi, wakati Rwanda hawafiki hata milioni moja! Wahutu ni milioni saba… sasa wapi na wapi?

Sisi (Wahutu) Wacongo tuliishi nao vizuri; Kagame kawaingiza kwenye vita. Wanaiba madini wakisaidiana na Marekani…wanawatesa Wacongo hawajui vita, wanajua Ndombolo na kupenda starehe,hususan wanawake! Muwe na tahadhari na Kagame katika  Ushirikiano wa Afrika Mashariki (EAC); kwani sera yake ni kuleta Tutsiland!

Wamarekani wamempa(Kagame) Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.(kitendo cha Marekani kutoingilia kati mgogoro wa Congo hapa kimeitwa kumpa Kagame Congo) Mtutsi akiuawa ni Genocide(mauaji ya kuamgamiza) kama vile Muisraeli akifa! Mpalestina akifa, Waisraeli  siyo wauaji!

 Lakini, Muisraeli akifa, Wapalestina ni wauaji…Anza kuandika vitu vilivyopo karibu yako. Mambo ya Iraq baadaye. Sawa?” aliniambia
       

Baada ya machafuko hayo ya Rwanda, takriban Wahutu na Watutsi milioni mbili walikimbilia uhamishoni Congo na mahali pengine, ambako pia walikufa kwa maradhi kama Kipindupindu na majanga mengine.

Majeshi ya Umoja wa Mataifa yaliingia Rwanda Juni 23 mwaka 1994 ili kulinda amani( safe zone).
Meja Paul Kagame aliapishwa kuwa rais wa nchi hiyo Aprili 22, mwaka 2000.Miezi michache iliyopita waliadhimisha miaka 19 ya mauaji hayo.

Kwa kuwa suala hili la mauaji ya Hayati Habyarimana na Ntaryamira ni siri, vema maoni ya Pierre yakachukuliwa kama mawazo binafsi, kwa kuwa hakuna ushahidi kuwa Rais Paul Kagame aliamurisha vikosi vya waasi wa RPF kuitungua ndege iliyowachukua.
 Kwa kusema hivi hatumtetei rais huyo au kumvua lawama zinazomzunguka.

Hata hivyo, gazeti hili linatarajia mjadala mkali juu ya maoni ya Pierre Kumaro. Jambo moja ni dhahiri juu ya ubabe wa Marekani duniani. Hadi sasa Marekani inawasaidia wababe wa kivita wa Somalia (Warlods) kuvifyeka vikundi vya wanamgambo wa Kisomali, kwa madai ya kuwa na uhusiano na mtandao wa Al-Qaeda.
Hili ni jukumu la ulimwengu mzima kupinga tabia hii ya kibabe. Kama Umoja wa Mataifa umeshindwa kuikemea Marekani, wa kazi gani basi?

Vita hivyo vya aibu Afrika, leo vimesababisha silaha za hatari kama AK-47 kuuzwa  kwa zaidi kidogo ya Dola moja ya Marekani( sawa na sh. 1300); na hivyo kuhatarisha eneo zima la Mashariki na Pembe ya Afrika. Kama silaha hizo zitafika mikononi mwa majambazi, hali itakuwaje?
 Au Marekani haioni aibu kuchochea vita Somalia kwa mara nyingine kwa sababu ya ile hofu ya Ukomunisti wakati wa VITA Baridi ?

Oktoba 4, mwaka 1993 askari 100 wa Marekani waliivamia Somalia kwa helkopta  12, na kukamata walinzi 19  wa Mbabe wa kivita, Jen. Muhammad Farrah Aydeed mjini Mogadishu.

Helkopta moja ilitunguliwa na wanamgambo wa Aydeed.
Askari 12 wa Marekani waliuawa na wengine 75 wakajeruhiwa vibaya katika mapigano yaliyodumu kwa saa 15.
Hapa, aibu ya kutisha ikaikumba Marekani, maana maiti ziliburuzwa mitaani kwa shangwe mjini Mogadishu! Bado tabia hii haijakoma; Marekani imerejea Somalia  kwa kisingizio cha ugaidi!

Kama alivyosema Taylor, “Boss wako akiwa adui yako, si umeangamia?”  Kama Umoja wa Mataifa umeshindwa kuikemea Marekani juu ya ubabe wake na upendeleo wake kwa baadhi ya Madikteta, jumuia ya Kimataifa ifanyeje?

Waandishi wa Tanzania hawajapewa ‘kitu kidogo’ na Rais Paul Kagame, ili kunyamazia mauaji ya kimbari ya Rwanda.
Kulingana na sheria (kila nchi inasheria zake) kuandika masuala tete kama mauaji ya hao marais wawili mwaka 1994 kwamba Marekani inachelea kumkamata Kagame, ni suala lililoanza kuzungumzwa na Majaji wa Kifaransa mwaka 2006.

 Kuhusu mauaji hayo, jambo moja ni dhahiri:
Kwamba Juvenal Habyarimana na Cyprien Ntaryamira walikufa pamoja na watu wengine wanane, katika ajali ya ndege ya  Aprili 6, 1994. Ndege hiyo inadaiwa kuangushwa kwa kombora na watu wasiofahamika, ingawa inahisiwa ilitunguliwa na waasi wa RPF.

Kagame kama rais wa nchi, ana staha yake na haki zake katika kujibu madai hayo, yeye mwenyewe, msemaji wa serikali yake, au Ubalozi wa Rwanda jijini Dar es salaam Kamwe hakuna wa kumsemea au kumyima uhuru na haki hizo.
Labda mpaka ushahidi kamili kama unaodaiwa kutolewa na huyo “mlinzi” ICTR utakapopatikana.

Suala la Kagame na lile la Bush na Blair ni tofauti, kwa kuwa UN wamekiri juu ya uvamizi dhidi ya Iraq; wakati kilichotungua ndege ya marais hao kimefanywa kuwa siri.

Aidha,  Marekani yenyewe au jumuia ya kimataifa hajapaza sauti kueleza chanzo cha ajali hiyo ya ndege iliyochukua uhai wa viongozi hao wa nchi jirani, na kusababisha vita na mauaji makubwa katika Afrika ya Kati.

Pia, kama alivyosema Taylor, “When your Master is your enemy, you are doomed!”
(Bosi wako anapokuwa adui yako, umekwisha!) si vita lelemama inayosubiri Tazama pekee, bali ulimwengu mzima upaze sauti kukataa dhuluma ya kutisha inayofanywa na Marekani, namna hii.

Kwa kusema hivi, hatujivui jukumu la kusema ukweli na kuilinda jamii dhidi ya uovu.Bali tunatanguliza staha ya kila mtu ,haki zake mbele ya jamii, utu wa mtu yeyote, tangu kibarua wa ngazi ya chini, hadi kiongozi machachari kama rais  Kagame

. Zaidi ya yote tunatanguliza uzalendo wa Afrika, ili kutochochea mateso zaidi kama alivyosema Pierre, ama mauaji ya kuangamiza kama ya mwaka 1994!
 RAIS OMAR HASSAN al-Bashir wa Sudan , yeye akikanyaga nchi yoyote inayoheshimu ‘waranti’ ya Mahakama ya Kimataifa(ICC) iliyoko Hague, Uholanzi, atakamatwa.
   Sheria za kimataifa hazitoi upenyo kwa Rais aliyeko madarakani kukamatwa. Kwa sababu,rais anayo kinga ya kidiplomasia iitwayo, ‘diplomatic immunity’.
    Lakini, Rais Omar Hassan al-Bashir ambaye amefunguliwa mashitaka ya kushirikiana na ‘mabedui’ wa Kiarabu wa Janjaweed, ya kuwaumiza raia Weusi wa Jimbo la Darfur nchini Sudan , akikanyaga nchi yoyote inayoshirikiana na Mahakama ya The Hague, atatiwa mbaroni kuanzia sasa.
   Katika kipindi kisichozidi miaka miwili, al-Bashir anakuwa Rais wa pili Barani Afrika kutishiwa kukamatwa na kushitakiwa katika mahakama za uhalifu wa kivita.
  Meja Paul Kagame wa Rwanda , anatishiwa na mpelelezi wa mauaji ya Kimbari ya Rwanda , ya mwaka 1994, Jaji Jean-Louis Bruguiere.
Jaji huyu wa Kifaransa, anasema Paul Kagame anahusika sana katika mauaji hayo.
     Anasema, Kagame aliamurisha Waasi wa Kitutsi, Rwandese Patriotic Front(RPF) kutungua ndege iliyokuwa imewachukua marais wawili wa Rwanda na Burundi .
   Rais Juvenal Habyarimana na mwenzake wa Burundi , Cyprian Ntyaramirwa, walikuwa wakitokea Dar es salaam Aprili 6 mwaka huo wa 1994, ndege yao ikapigwa kombora kali jirani na kasri la Rais, ilipokuwa ikijiandaa kutua mjini Kigali .
   Walikuwa wakitokea mkutanoni Dar es salaam , ambako walikuwa na mazungumzo na Rais Ali Hassan Mwinyi, wakati huo.
 Huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa mauaji ya Kimbari(genocide); mauaji ya siku 100 yaliyochukua roho za Watutsi na Wahutu wa msimamo wa wastani kati ya 800,000 na 900,000.
   Jaji Bruguiere, alisema Kagame akiwa Kiongozi wa Waasi wa RPF aliamurisha ndege hiyo iliyowachukua viongozi hao wawili kupigwa kwa makombora mawili makali, hadi ikadondoka na kuwaua viongozi hao.
   Rais Kagame anakanusha vikali na kusema ni Wafaransa waliohusika kuiangusha ndege hiyo kwa sababu walikwishamchoka ‘rafiki yao ’ yaani Rais Habyarimana.
    Kwa sababu hiyo, Wafaransa walishatangaza kutaka Kagame aondolewe kinga, ili akamatwe na kushitakiwa katika Mahakama ya Umoja wa Mataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR), iliyoko Arusha , Tanzania .
   Mahakama ya Umoja wa Mataifa( ICC) ya mjini Hague inashughulikia makosa ya kivita.
 Ina mwanachama mmoja wa kudumu-Uholanzi-ambako mjini The Hague kuna jopo la majaji 15 wanaoshughulikia kesi zinazohatarisha amani na usalama katika mamlaka za Kimataifa.
 Mahakama hii ya Hague imeshughulikia kesi nzito, hususan zinazowahusu viongozi wa  nchi kama Charles Ghankay Taylor wa Liberia, Slobodan Milosevic wa Serbia na wahalifu wengine kama Pierre Bemba wa Jamhuri ya Kimdemokrasi ya Congo, Kiongozi wa Waasi wa Revolutionary United Front(RUF) wa Sierre Leone, Marehemu Foday Sankoh, Adolh Hitler na wafuasi wake n.k
 Kulingana na Tangazo la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu la Desemba 10, mwaka 1948, watu wote wanaopora haki za msingi za kuishi, wanastahili kushitakiwa.
   Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lenye wanachama wa kudumu kama Uchina, Uingereza, Marekani, Ufaransa na Urusi na nyingine 10 huja na kuondoka, linapaswa kuwashughulikia wote wanaosababisha vifo ama maangamizi ya raia wa dunia.
  Mfano ni huo wa Sierra Leone ambako Rais Charles Taylor wa Liberia wakati huo, alishirikiana na ‘rafikiye’ Foday “Poppay’ Sankoh, kuendesha vita kali ili kujipatia na kuuza almasi.Masoko ya Ulaya na Marekani ndiyo yaliyofaidika na almasi za Sierra Leone mwaka 1999.
  Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Pierre Bemba alikamatwa kuhusika na vita. Rwanda, mwaka 1994 Paul Kagame na maofisa wake wa kijeshi wanatuhumiwa kuanzisha vita vilivyoshindwa kuzima maangamizi, na Darfur, Sudan Omar Hassan al-Bashir anatuhumiwa kuua na kuwasaidia Janjaweed kuumiza raia wa jimbo hilo.
  Ni kwa sababu hii, kuna wanaharakati wanaoona Waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza, Tony Blair na Rais Mstaafu wa Marekani, George Walker Bush, nao wanastahili kukamatwa kuhusika na vita Irak na Afghanistan kinyume na matakwa ya Umoja wa Mataifa(UN).
   Yaani, Uingereza, Marekani na washirika wao walipeleka vita na hasara ya mali na maisha nchini Irak, walipindua serikali ya Saddam Hussein kwa kisingizio cha kuwepo silaha za maangamizi, Umoja wa Mataifa ukaja kubaini kuwa hakukuwa na silaha.
   Kufuatia ukweli huo, si Jaji Jean-Louis Bruguiere wa Ufaransa, wala Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Mahakama ya Uhalifu wa kivita, Luis Moreno-Ocampo,  ama Fatou Bensouda,waliokwishatoa ‘waranti’ ya kumkamata Bush ama Blair ili nao wakabili mashitaka ya umwagaji damu nchini Irak, kama siyo Afghanistan .
Sasa, wanakwenda Syria akina Obama na Hollande,Umoja wa Mataifa uko kimya,ingawa umekataa kupeleka maangamizi huko.
   Wakati Luis Moreno-Ocampo anadai kuwa ushahidi mzito wa kumtia hatiani Rais Omar Hassan al- Bashir wa Sudan , kwa kuamuru majeshi yake kuteketeza watu wa Makabila ya Fur, Masalit na Zaghawa, na kuathiri wengine wapato milioni 2.5 wa kabila la Zaidiya.
 Bado hajafikiria kuwapeleleza Tony Blair na Bush angalau kwa kusema uwongo, kwamba Irak kulikuwa na silaha za maangamizi(mass destruction wepons), kumbe siyo kabisa!
  Ni kwa sababu hii watu wanasema Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, lenye wanachama wa kudumu na nguvu za ‘Veto’ kama Uingereza, Marekani, Ufaransa, Uchina na Urusi, wana macho yenye ‘makengeza’ kuona makosa ya wahalifu wa Barani Afrika, wakashindwa kuona yale ya Mabwana wakubwa kama Bush na Blair!
Hawa ndiyo maana wanatazama Kagame kama hana hatia hadi sasa ila iko siku watabadilika.
   Aidha, mashitaka dhidi ya Slobodan Milosevic, Foday Sankoh, Charles Taylor, Adolf Hitler na wafuasi wake wa ki-NAZI, nay ale ambayo yangewakabili watu kama Marehemu Dikteta Pinochet wa Chile , na wengine waliomwaga damu duniani.
   Yana tofauti gani na Bush na Blair kupeleka majeshi Irak na kupindua serikali  ya Saddam Hussein; kisha wakashindwa kukomesha umwagaji damu?
   Nchini Rwanda, tumeona mchakato wa kumtia mbaroni Rais Paul Kagame ulishaanza, baada ya Mkuu wake wa Itifaki, Bibi Rose Kabuye kukamatwa mjini Frankfurt, Ujerumani na kupelekwa Paris, Ufaransa ili kukabili mashitaka yale ya kuhusika na genocide.
   Ni kwa sababu hii Afrika inajiuliza: Je, mahakama hii ya Umoja wa Mataifa, haioni kwamba Bush na Blair kuiongopea Umoja wa Mataifa na kwenda kupindua serikali, wakashindwa hadi sasa kuleta utangamano Irak na Afghanistan , siyo kosa kama la Kagame, al-Bashir, Taylor na wenzao?
   Msumeno leo hausemi hivi ili kuwalinda marais Paul Kagame wa Rwanda na Omar Hassan al-Bashir wa Sudan , wasikamatwe na kufunguliwa mashitaka kwa uovu waliofanya, maadam akina Ocampo na Jaji Bruguiere wana ushahidi mzito.
   Hapa, tunahoji tabia ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lenye wajumbe wa kudumu kama Marekani, Uingereza, Uchina, Ufaransa na Urusi na wenzao  10 wa kuja na kuondoka, linaona makosa ya viongozi wa Afrika peke yake, na kuwaacha akina Bush na Blair kula 'good time’ bila kushitakiwa?
   Je, Baraza la Usalama halijasikia kwamba hawa hawakuwa na ushahidi wa kuivamia Irak?
Kwa sababu Mkaguzi wa silaha wa Umoja wa Mataifa, alishasema hapakuwa na silaha za maangamizi Irak.
  Nataka kusema kwamba, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na Makama ya Uhalifu wa Kivita(ICC) wanakuwaje na ‘makengeza’ kwa makosa ya akina Bush na Blair?
    Foday Sankoh, Milosevic, Taylor, Kagame, al-Bashir, Pierre Bemba wameshupaliwa. Tunajua hata akina Jonas Malheiro Savimbi walisaidiwa sana Shirika la Ujasusi la Marekani(CIA) kuihujumu Angola .
   Yaani, Waafrika wanapofanya uhalifu kwa maslahi ya Uingereza na Marekani watakamatwa baada ya maslahi kutoweka.Wakifanya uhalifu akina Blair na Bush, UN inapata makengeza na kushindwa kubaini makosa?
Ndiyo Maana Kenya wameamua kujitoa katika Mahakama hii ambayo hata Marekani na mataifa mengi ya Ulaya,hawamo.
   Akina Bush na Blair wakipeleka vita Afghanistan , Irak , Iran , Korea Kaskazini na popote wanapopingwa sana , hawakemewi.
Wanasema, Bush na Blair au Barack Obama na Gordon Brown wakiipindua nchi kwa maslahi yao , basi siyo magaidi bali ni ‘liberators’ .Mtu mwingine akiua wananchi kwa maslahi ya milki yake, basi ndiye mwalifu wa kivita!
  Ni kwa sababu hii  naona“double standards” katika maamuzi ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na utendaji kazi wa Mahakama ya The Hague .
  Waafrika kama Bemba, Jonas Malheiro Savimbi, Charles Taylor, Sankoh na wenzao wakifanya vita, kisha wakaiba almasi, dhahabu na mafuta na kumuuzia Mzungu, mwisho wa siku watakamatwa wao na kufungwa jela, na wala aliyewatuma na kuwapa silaha haulizwi!
  Charles Taylor alishawashangaa sana Marekani kwa sababu aliposhirikiana na Foday Sankoh kupigana vita na serikali ya mjini Freetown na kuiba almasi mwaka 1999, aliwauzia wao!
    Sasa, walipoona watabainika, wakatangaza Taylor na Sankoh wakamatwe.
 Taylor yuko jela,baada ya kuhukumiwa Hague, wakati Sankoh alikamatwa lakini akafariki dunia huko mjini Hague.
  Je, huu ni uungwana?
  Anayebisha, akatazame filamu iitwayo, Blood diamond, atawaona Wazungu kuhusika katika vita hivi vya almasi za damu nchini Sierra Leone.Wakati Taylor na Poppay Sankoh walibadilishana na Wazungu almasi kwa bunduki, Umoja wa Mataifa haujaona Mzungu aliyesaidiana nao katika biashara hii ya damu, ila kawaona Taylor na Sankoh tu!
   Hizi ndizo ‘double standards’ tunazozungumza. Vita walivyoanzisha Wazungu, Baraza la Usalama halioni. Maasi ya akina Sir Mark Thatcher kule Guinea ya Ikweta, ili waibe mafuta, Mahakama ya uhalifu wa kivita haioni!
  Ni kwa sababu gani Jean-Louis Bruguiere wa Ufaransa na Luis Moreno-Ocampo, hawajaona rasilimali za Afrika zinazoporwa baada ya wao kuanzisha vurugu na vita?
Vita vya Kongo kuna mkono wao kwa akina Paul Kagame,ndiyo maana wako kimya, angekuwa Mugabe wangesema akamatwe haraka!
   Tumeona Blair, Bush, Bemba, Poppay Sankoh, Taylor , Milosevic, Hitler, Kagame na Omar Hassan al-Bashir, wa na kesi moja!
  Sasa, kwanini washitakiwe wengine akina Bush na Blair wabaki?
  Marekani, Uingereza, Urusi, Ufaransa, Uchina hawaoni kwamba hawa jamaa wana kesi ya kujibu The Hague, sambamba na Kagame, al-Bashir, Taylor na Bemba?
   Wanaendekeza ‘double standards’ katika masuala ya msingi ya amani na usalama wa dunia eeh?!!
Ndugu yangu raia wa Rwanda, aliniandikia hivi:


“ Kuhusu Bush, Blair  ,Sadam na Tayor kweli napenda sana kuona munajali sana kwandika mataifa ya mbali na munajitaidi kwelimisha wa Tanzania.

Lakini, unapoandika Vibaraka kama Sadam na Taylor namuna Marekani waliatumia kuua ndugu zao ukasahau mtu Kama Kagame wakati ndiye mtu wa hapa karibu!  Kwanini
ninyi Watanzania munaogopa kwandika mateso ya Wanyarwanda wanaopata kwasababu ya Kibaraka kagame?
 Yani ni kwamba hamujue au mumepata kitu kidogo kwasababu ninyi munandika tu mateso ya wa Iraq , Liberia mambo ya Rwanda hamutake kuyajurisha watanzania?
Ebu wewe niambie kama umewayi kusikia maadamano ya chama cha upinzani Rwanda, umewayi kusikia chama cha upinzani Rwanda kinafanya mkutano wewe jiwulize Rais wa zamani anawekwa ndani eti kwasababu anataka kuunda chama
abu jiwurize wewe Rwanda wanapata wapi silaha wapi za kupigana hadi kukakamata Congo nzima wewe juwulize tangu Kagame awekwe madarakani na Wamerikani?
 Ukiwa wazili(Waziri) Muhutu ikimariza tu ni jera au injee au unakufa wewe jiwurize mimi nashangaa sana Tanzania jinsi wanatuonea sisi wahutu hamutake kuweka mambo hazarani sasa ivi kuna mtu yupo ata last month alikuwa Arusha kwenye ire mahakama(ICTR) yeye arikua Murinzi wa kagame anasema namuna Kagame aritowa amuri ya kungausha ire ndenge na ndege iyo ndio mwanzo wa mauwaji yeye arishiriki mia kwa mia anatoa ushahidi wa kutosha lakini iyi mahakama inakataa kumukamata kwa sababu Marikani hawataki kwanini vitu kama ivyo hamubyandike wakati vipo ata kwenye Internet
watutsi wariuua watu uko Congo hadi leo ati wanasema kuna wanyamurenge wanyamurenge wagapi uko congo wakati ni wanyarwanda watupu  wewe nenda uko Ubarozini uwurize niwafanyakazi wagapi wahutu wote kwanzia Borozi ni watutsi hapa tu Dar es salaam only warinzi watanzania tu wengine ni watutsi wakati Rwanda hawafike ata 1m wakati wahutu ni 7m sasa wapi na wapi wewe wuriza wacongo mateso wanayopata kutoka kwa wanyarwanda watusi sisi na wacongo tuliyishi nao vizuli lakini tangu Kagame amekuja amawaingiza kwenye vita tama tu ya yeye ya madini ya akisaidiana na usa wanawatesa wa congo unajuwa wacongo mambo ya vita hawajuwe wanajua tu Ndombolo na kupenda wanawake tu!
lakini Kagame ameamua kuwatesa
muwe makini na kumwingize katika EAC kwababu watu wa kagera warsha sema nia ya Kagame ni kureta Tutsi –Land!
wewe kama unaitaji mengi zaidi
sema lakini mujuwe kama Wanyarwanda tumevamia na Kagame na wa wamerikani kwa sababu ya madini ua congo ni kwamba wamerikani wamuhandi kumpa Madaraka yeye akawapa Congo ndio mana anauua hawaseme kitu mutsi akifa ni Genocide kama vile Isaiel yani Mparistina akifa sio mauuaji lakini mwisirael akifa ni mauuaji yani ndungu tuakufa kama sio binadamu sasa wewe anza kua unadika vitu vipo karibu yako ayo mambo ya Iraq badaye sawa”, aliniandikia rafiki yangu raia wa Rwanda, ambaye jina limehifadhiwa.
Hivi ndivyo Wanyarwanda waliotimkia Ughaibuni,kumhofia Kagame wanavyolaumu vyombo vya Habari vya Afrika,hususan Tanzania,kushindwa kuandika ukweli kuhusu Paul Kagame na wenzake wanavyofanya!



Kufuatia hali hiyo, naamua kuyajibu maswali hayo kwa kunukuu vyanzo anuwai vya habari,kikiwemo kijarida kitolewacho kila baada ya majuma mawili na Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agostino(SAUT) jijini Mwanza, Malimbe Campus.
  Kijarida hiki,kinaitwa CURRENT AFFAIRS, na unaweza kukipata pia kupitia website:www.saut.ac.tz/Current Affairs.
Kichwa cha makala ”Umoja wa Mataifa wa Marekani” hufanana na kichwa cha makala ya Amani Nkurlu,mmoja wa wahariri wasaidizi wa Current Affairs, katika toleo la Aprili 8-25 mwaka  2011.
   Amani Nkurlu,aliandika katika ukurasa wa nne, kwamba The United Nations of America” huku akieleza malengo ya kuanzishwa Umoja huo wa Mataifa Oktoba 24, mwaka 1945 kwamba ilikuwa ni kuondoa utumwa na vita duniani,ili kustawisha Haki za Binadamu,Amani na kuleta maendeleo kwa wakazi wa dunia.
  Kinyume chake, Umoja wa Mataifa(UN) ukiwa mithili ya ng’ombe aliyefungwa kamba shingoni na Marekani, unaburuzwa kwenda kuua mamia ya maelfu ya watu Afghanistan, Irak, sasa Libya,Yemen, baadaye Uturuki, Iran n.k
 Umoja huu(UN) uko mbioni kupeka vita vya maangamizi Iran, Yemen,Uturuki na katika nchi nyingine zilizoko jirani na Mfereji wa Suez na Bahari ya Mediterranean, ambazo huzalisha kwa wingi mafuta takriban asilimia nane za mahitaji ya dunia.
   Nimeandika pia makala iitwayo, “Safari ya miaka 59 ya Afrika,kutoka Uhuru kurejea Utumwani” ,nikieleza ubeberu na mpango wa mabepari wa Marekani na washirika wake,na mashirika yao ya kijasusi, kama Central Intelligence Agency(CIA) na lile la kibaraka wao, Israeli(Mossad)kuvuruga amani katika eneo lenye mafuta mengi,huko Mashariki ya Kati.
   Awali, walitumia Shirika la Makaburu wa Afrika Kusini(BOSS) kuhujumu harakati za uhuru,wakawaua wanamapinduzi wa Afrika,kama Samora Moises Machel,na wengine ndani ya Afrika Kusini, wakawafunga jela Nelson Rolihlahla “Madiba” Mandela n.k
   Kwanza, niwapongeze wajumbe wa Bodi ya uhariri na waandishi wa Current Affairs:Theresia Christian,Gregory Gondwe, Amani Nkurlu na wenzao, kwa kuuona ubeberu na ubepari kasha ukoloni mamboleo, ukipindua mamlaka za nchi zenye rasilimali nyingi kama mafuta.
 Visingizio vyao eti ni kuleta amani na demokrasia katika nchi hizo, na kasha Haki za Binadamu!
 Marekani, Uingereza na Ufaransa,wamempindua kibaraka wao Hosni Mubarak,kwa sababu ya Mfereji wa Suez uliojengwa na Ufaransa na Uingereza mwaka 1859-1869.
Walianza kuupigania,Misri ikautaifisha Julai 28 mwaka 1956.
 Una urefu wa maili 103 unatumiwa na mameli kuziunganisha Bahari ya Shamu(Red Sea) na Bahari ya Kati-Mediterranean.
  Misri pia kuna mafuta mengi na madini mengine,na ina ushawishi katika nchi nyingi za Kiarabu zenye utajiri wa mafuta.
Huko Libya, kosa la kwanza la Kanali Muammar al-Gaddafi,lilikuwa kutaifisha visima vya mafuta mara baada ya kuingia madarakani mwaka 1969, kwa maslahi ya wananchi wa Libya, na aslani si kwa maslahi ya makampuni ya Ulaya na Marekani.
   Utaifishaji, katika macho ya wakiloni hawa,mabeberu ni kosa kubwa na hatari kwa maslahi yao-wao na Mashirika yao kama  International Monetary Fund(IMF) na Benki ya Dunia(WB) wanataka dunia nzima itekeleze amri yao iitwayo UBINAFSISHAJI!!
 Hapa kwetu,tumebinafsisha hata makampuni na mabenki yaliyojiendesha kwa faida kubwa na kuwapa ajira wananchi,kwa sababu tunawaogopa hawa mabwenyenye na taasisi zao za Breton Woods.
  Marekani na washirika wake, wanauburuza Umoja huu wa Mataifa(United Nations of America?), wanawafadhili waasi nchili Libya kwa silaha nzito na fedha,ili wapigane vita vyao walivyoanzisha tangu mwaka 1986 vya kumpindua Kanali Muammar al-Gaddafi.
 Kwa sababu, Gaddafi alikuwa na kiburi cha kutowafungulia mlango makampuni ya Marekani na Ulaya, na alithubutu kuhujumu ndege ya Pan American Airways(PAN AM) huko Lockerbie, Scotland mwaka 1988.
 Akasalimu amri nusu nusu kwa kulipa fidia ya mamilioni ya Dola za mafuta, ili sasa wamwondoe katika ramani ya Mhimili wa Uovu(The Axis of Evil),kumbe wapi bwana!Wanae tu.
  Hapa kwetu wanatuingilia hata jikoni, eti kwa sababu wametufunika kwa chandarua cha kukinga Malaria! Gaddafi, alitaka Afrika iunde taifa kubwa-The United States of Africa!
 Hii ndiyo ilikuwa njozi ya akina Kwame Nkurumah, Gamal Abdel Nasser, Julius Nyerere, Patrice Emery Lumumba, Ahmad Sekou Toure na wenzao, wakaishia kuwekewa vikwazo vya uchumi na kuuawa.
 Na Gaddafi anarejea kosa la wenzake,kutaka mafuta ya Afrika,madini na gesi view kwa maslahi ya Waafrika tu.
 Kama Umoja wa Mataifa(UN) ulianzishwa ili kulinda amani baada ya Vita  vikuu vya Kwanza na Vya Pili,kuhifadhi Haki za Binadamu na kuleta maendeleo kwa watu:
  Kwanini Umoja huu(UN) uwe wa Marekani na washirika wake,Uingereza na Ufaransa,na wajiamulie wao kwenda Afghanistan kupindua serikali na kuweka watu wao,kasha wakaenda Irak na kumkamata Saddam na kumchinja kwa kitanzi huku wakiua mamia kwa maelfu?
  Irak, wameua watu zaidi ya 700,000 sasa na wanatesa raia wanaowapinga kwa vifungo jela huko Guantanamo Bay na Abu-Ghraib.
 Wanawafunga jela watuhumiwa hata kabla ya kuwafikisha mahakamani. Je,huku si kuhujumu Haki za Binadamu wanazodai zinakiukwa Misri, Yemen,Tunisia,,Iran,Korea Kaskazini na nchi adui zao?
 Umoja wa Mataifa unaburuzwa kupelekwa Iran,ili wakampindue Mujahiddin Mahmoud Ahmadnejad, aliyeachia madaraka juzi,kwamba alirutubisha madini ya Uranium kwa ajili ya silaha za nyuklia.
Wako mbioni kwenda Syria,baada ya kuvuruga Misri na kwingineko Ulimwengu wa Kiarabu.
  Wametoa amri ndege za Gaddafi zisiruke angani Libya kuwapika waasi(rafiki zao na vibaraka wao) kwa amri ya “No Fly Zone”!
Gaddafi alishakufa,sana Osama na Saddam.
 Sasa msomaji, badala ya amri hii, “No Fly Zone” kutolewa na Katibu Mkuu wa UN, Bwana Ban-Ki Moon huko 1st Avenue, New York,inatolewa na akina Obama, Hillary Clinton na Robert Gates, huko White House, mjini Washington!!
 Kumbe, ndiyo maana tunasema UN ni Umoja wa Mataifa wa Marekani!
 Na hii siyo mara ya kwanza kwa mabepari kuchochea vita duniani,mahali kulipo na alamasi,dhahabu,mafuta,gesi,uranium na mifereji kama Panama na Suez na bahari kama Mediterranean n.k
 Katibu Mkuu wa Pili wa Umoja wa Mataifa,huu wa Marekani(The United Nations of America)Mswedeni, Darg Hjalmar Agne Carl Hammarskjold, aliyefanya kazi tangu Aprili 10 mwaka 1953-Septemba18 mwaka 1961, alikufa kwa ajali ya ndege Congo,leo DRC.
Akina Kagame wanaendeleza yale waliyoanzisha Mataifa Makubwa huko Kongo.
  Nani alichochea vita Congo?
Kwa nini? Ni Marekani na washirika wake na majasusi wa CIA walileta uasi na vurugu huko Shaba na Katanga,wakamkamata mwanamapinduzi, Patrice Lumumba na kumuua.
 Lumumba, alikuwa na sera za kijamaa,za kutaka madini ya Congo na rasilimali zingine kuwa mali ya raia wa Congo—ooh, akawakosea hawa.
 Wakawachochea akina Moise Tshombe,Joseph Kasavubu na vibaraka wao wengine kama Joseph Desire Mobutu Sesesseko, wakamuua Lumumba.
 Sasa, Katibu Mkuu wa UN wakati huo Dk. Darg Hammarskjold akasafiri kwa ndege kwenda Congo kutafuta amani, Septemba 18 mwaka 1961 akafa kwa ajali ya ndege.
 Hadi leo, Umoja huu wa Mataifa wa Marekani(United Nations of America)HAUJATULIZA VITA Congo.
 Badaye, walimweka kibaraka wao Mobutu, wakaiba madini wee, Mobutu alipora Dola za Marekani milioni sita akaficha Ulaya-fedha hizi ni nyingi sawa la deni la nje la nchi nzima.
   Salim Ahmed Salim, alijaribu kugombea Ukatibu M kuu wa UN. Marekani walimkataa kwa sababu alikuwa anatoka nchi ya kijamaa,na hasa ujamaa wa akina Nyerere!
  Umoja wa Mataifa wenye nia ya kuboresha maslahi ya watu duniani,ukatae ujamaa?
Aliwekwa Boutros Boutros-Ghali wa Misri kuwa Katibu Mkuu wa sita,Januari Mosi mwaka 1992.
 Nataka nikwambie msomaji.
Huyu Boutros Boutros Ghali, alikataliwa na Marekani asigombee mhula wa pili,kwa kisingizio kwamba alishindwa kuzuia mauaji ya Kimbari-genocide-huko Rwanda, kisha hakuzuia vita Angola!
Natumai umekwishaona nani walisababisha genocide Rwanda mwaka 1994.
 Nani alichochea vita Angola?
Siyo Marekani na washirika wake na majasusi wa CIA waliomfadhili Jonas Malheiro Savimbi,ili kukwamisha juhudi za akina Agostino Neto?
 Nani alihujumu MPLA? Ndiyo, walimtoa kafara Boutros Ghali, kwa sababu alishindwa kubeba maslahi ya Marekani, akataka kuleta uarabu-arabu huko.
  Alikuwa Katibu Mkuu wa kwanza wa UN kutumikia mhula mmoja tu, wakati huko Cabinda, Angola tunajua kuna mafuta mengi na Marekani wananchochea maasi,
 Naam, Umoja wa Mataifa(UN) ni ng’ombe wa maziwa wa Marekani!
Kisha,twajua Umoja wa Kujihami wa Ulaya Magaharibi(Northern Atlantic Treaty Organization) ULIANZISHWA NA Rais Franklin Roosevelt wa Marekani na Waziri Mkuu Winston Churchill wa Uingereza mwaka 1941 ili kujihami dhidi ya Urusi na washirika wake wa Warsaw Pact.
 Sasa, NATO kuishambulia Libya, maana yake Gaddafi aliwashambulia NATO lini? Marekani inayochangia UN kwa zaidi ya asilimia 30 ilimweka Kofi Annan,wa saba wakamburuza hadi mwenyewe amekiri kuhenyeshwa.
 UN ni ng’ombe wa Marekani wa maziwa na kafungwa kamba shingoni.Wanakotaka kwenda Marekani, na UN inakwenda.
 Rwanda walikufa watu 800,000 bila msaada wa UN kwa sababu hakukuwa na mafuta. Bosnia na Herzegovina mwaka 1995 walikufa 200,000,Irak wameuliwa watu 700,000, Afghanistan wamekufa mamia kwa maelfu, UN wapo tu hadi ofisi zake zikalipuliwa kwa bomu.
 Hawana kazi! Hakuna wanachokataa juu ya Misri,Libya,Yemen, Uturuki n.k Huu Umoja wa Mataifa umeshindwa kuleta amani duniani,unaleta kiza na wakimbizi kuliko wakati wa Vita vya Kwanza na Vya Pili vya Dunia.
  Hata Ivory Coast, UN hawatafanya kitu, Laurent Gbagbo kakamatwa Aprili 11, mkewe Simone akabakwa na wafuasi wa Ouattara Dramane, watu wanaweza kuuana kikabila na kidini,lakini utaona UN inatazama mafuta, kakao na mbao zaidi kuliko kulinda watu!
 Vita vya kwanza vya Dunia(1914-1918) vilisababisha wanajeshi 8,418,000 na raia 1,3000 kupoteaa maisha.
 Vita vya Pili vya Dunia(1939-45)viliua wanajeshi 16,933,000 na raia 34,305,000 wakiwemo babu zetu. Vita ambavyo Marekani Vietnam(1962-70)Vikaua watu 500,000,Korea wamekufa wau milioni nzima mwaka 1950-53. Kasome kitabu kiitwacho CONFICT ON THE TWENTIETH CENTURY cha David Wood(Institute for Strategic Studies),London.
 Nataka msomaji wangu ujue kwamba Umoja wa Mataifa(UN) unaoburuzwa na Marekani na washirika wake kwa tabia hizi, kamwe hawaleti amani na maendeleo-ni vita,njaa na wakimbizi,na maradhi na mauti.
 Hakuna uhuru,kama raia wanaamuliwa nani awatawale na Marekani,tena kwa muda gani. Umoja huu una umri wa miaka 66, una Makatibu Wakuu nane:
Trygve Lie wa Norway,Hammarskjold wa Sweden, Dk U-Thant wa Burma, Kurt Waldheim wa Austria, Javier Perez de Cueller wa Peru,Boutros Ghali wa Misri, Kofi Annan wa Ghana na Ban Ki Moon wa Korea Kusini nchi rafiki yao.
 Hawezi kutokea Katibu Mkuu wa UN Uchina, Urusi,Tanzania ama Korea Kaskazini!Wakitaka kuvamia Yemen,Uturuki au Iran kwamba kuna nyuklia, hawa watakataa.
 Kinachotakiwa na Marekani na washirika wao,ni kuwapigia goti tu, na ukiwapinga ni kupigwa vita vikali kwa visingizio vya demokrasia na haki za binadamu ambazo wao wamezivunja mno.
  Ndiyo maana, Biblia katika Ufunuo wa Yohana 13:11-18, inawasema Marekani kama Mnyama kama mwanakondoo aliyekuwa na demokrasia na Uhuru wa dini, sasa ni Ibilisi anayewalazimisha watu wote kuwekewe vikwazo vya kiuchumi-economic sanctions!









No comments:

Post a Comment