Friday, September 13, 2013

HONGERA KENYA KUKATAA UKOLONI WA MZUNGU ICC


                          
Nalazimika kurejea sehemu ya makala yangu iliyokuwa nakichwa cha habari, “AFRIKA KIZIMBANI”,ili kujaribu kuzibua akili zilizoziba za Watanzania ‘Fuata Upepo” kwa kila kinachosemwa mitaani!
Makala hiyo iliyotwaliwa katika Jarida maarufu sana, New African la Julai, 2012 iliyokuwa na kichwa cha habari, “Is Africa on Trial?’
Kulikuwa na kichwa kidogo(sub heading), “The Role of the ICC(International Criminal Court) examined”.
Julai Mosi, mwaka 2012, Mahakama hii ya Kimataifa(ICC)ilikuwa inatimiza umri wa miaka 10;sasa ina miaka 11,wengine wanaota ilikuwepo miaka milioni nyingi,Afrika tu sasa inajifaragua kutaka kujiondoa katika mahakama hiyo!
Nataka wenye akili baridi wasidhani ilikuwepo zamani wakati Adamu na Hawa wanaumbwa Edeni,mwaka 4000 BC.
Ni mahakama iliyoishi kwa muongo mmoja,kufuatia Mkataba wa Rome, wa 2002.Nchi nyingi za Afrika zilijiingiza kichwa-kichwa katika uanachama wa mahakama hii,kufuatia Senegal kuwa mwanachama wa mwanzo.
Kuna akili mgando zinazoweza kusema Afrika haiwezi kuanzisha Mahakama kama hii hapa ikatoa haki,kwa sababu viongozi wetu-Madikteta- hawana Political Will-utashi wa kisiasa wa kuwa na haki na demokrasia!
Wanasema Afrika ndiyo nyumba ya utawala mbaya,rushwa na mauaji.Huu ni umbumbumbu wa kutojua dunia nzima hii hakuna haki wala uhuru na demokrasia,sembuse Afrika?
Kasumba ya Kikoloni(colonial mentality) imewaibia akili Waafrika kudhani hakuna haki na maendeleo kama hakuna Mzungu! Hawa ni watumwa wa hiari.Wanatimiza unabii wa akina Hitler,Botha na Makaburu wengine wabaguzi wa rangi.
Sasa angalia wewe msomaji mwenye akili.Hata sasa  wendesha Mashitaka Mkuu wa ICC,Fatou Bensouda,toka Gambia,Afrika Magharibi,ni Mweusi tena mwanamama.
Waafrika Weusi wanashika ‘Key Positions’ katika Mahakama hiyo ya The Hague,Uholanzi(kumdanganya Mwafrika);kwanini Umoja wa Afrika(AU) isianzishe Mahakama yake,Nairobi,Arusha,Abuja ama popote?
Afrika haiwezi kuwatia kabala Madikteta na wauaji wanaofanya vita hapa Afrika? Najua vita nyingi Mwafrika hutumiwa kama kinyangarika ili kutekeleza maslahi ya Mzungu,halafu lawama hubeba yeye mgongoni.
Kufuatia ujinga wa Mwafrika,hata hao akina Bensouda huko ICC huendesha mashitaka na kutoa hukumu inayolinda maslahi ya Mzungu na aslani siyo Mwafrika!
Mahakama za Umoja wa Mataifa kama ile ya Sierra Leone,ya Mauaji ya Rwanda(ICTR) na ile ya mjini Hague(ICC) ati hushughulikia mauji ya Kimbari-genocide-na matendo yaliyokinzana na haki za binadamu na uhalifu wa kivita.
Sasa tafakarini:Paul Kagame(rafiki wa Marekani) aliua         marais wawili,Juvenal Habyarimana wa Rwanda na Cyprian Ntaryamirwa wa Burundi,Aprili 6 mwaka 1994.
Ana kesi inayomkabili?
Kagame akiongoza Waasi(rebels) wa RPF aliua maelfu ya watu raia wa Rwanda hadi Wahutu wakaanzisha Intarahamwe ili kulipa visasi,kwa kuwa wao  ni wengi.
Kosa la Kagame halikutazamwa kuwa ni kosa,kosa Wahutu kulipa kisasi!
Pili,Kagame hakuingia Kongo na kupigana vita(kuua) ili kuwateketeza Waasi wa Intarahamwe? Kuvuka mpaka na kuingia nchi ya KONGO siyo kosa katika Jumuiya ya Kimataifa? Ama hakuna ushahidi The Hague!
Kuwatafuta waasi wa Kihutu ndani ya Kongo na kuwaua,bila kuwafikisha mahakamani,ndiyo nini?
Kagame Mtu-tsi,anapowasaka Wahutu na kuwaua ni nini kama siyo genocide?
Siyo, crimes against humanity? Siyo, war crimes?
Kagame na rafikiye Museveni wanawasaidia Waasi wa Kongo(M23,Bosco Ntaganda,Jen. NKUNDABATWARE n.k hii nini?
Wewe unawasaka waasi wa  nchi yako ndani ya ardhi ya nchi nyingine, unaona uasi ni unyama unastahili adhabu kali ya kifo,wakati huo huo unawaunga mkono waasi wan chi ya jirani na kuwalea!
Ukiambiwa kuzungumza nao ‘peace talk’ au ceasefire agreement, unakuwa mkali unatukana watu! Hii nini sasa?
Hiyo ndogo, wewe unaingia nchi ya watu na rafiki yako,mnapora madini,mbao,pembe za ndovu n.k mnaanza kupigana ndani ya nchi ya watu,mnabaka akina mama,mnaua watoto kwa risasi,halafu Wakongo wakisema,mnasema mnawatafuta Intarahamwe!
Mbona ICC haijaona kosa la Museveni na Kagame,hata kama Jaji wa Ufaransa,Jean Louis Bruguire ,alisema Kagame akamatwe na kupelekwa Arusha,baadaye wakasema ana Diplomatic Immunity?
Sasa tujiulize, Omar Hassan Ahmad al Bashir wa Sudan,siyo Rais? Hana diplomatic Immune? Mbona anasakwa akamatwe hadi akakimbia Nigeria juzi,kwa kuwa Nigeria ni mwanachama wa Icc?
Hivi makosa ya hawa wote,hayafanani na makosa ya Bush na Blair kwenda kuipiga Irak na Libya na kumuua Saddam na Gaddafi,bila ridhaa ya Umoja wa Mataifa?
Hiyo nini kama siyo Impunity? Yaani mtu anafanya makosa mabaya, anaachwa bila kushitakiwa mahakamani!
Sasa upendeleo mnaosema madikteta wa Afrika wakianzisha ICC, Addis Ababa itakosa shabaha,hamwoni kitu hicho hata sasa? Mna makengeza!
Sasa akina Obama wanakwenda Syria(nitaeleza kisa hicho toleo lijalo) bila ruhusa ya Umoja wa Mataifa,wanajifanya wao polisi,mahakama,mgambo,hakimu na waendesha mashitaka kwa wakati mmoja!
ICC inakazi gani sasa kama bunduki za Marekani,Uingereza,Ufaransa na wapambe wao wana ruhusa ya kukamata,kuua na kuzika bila mtu kukohoa! Guantanamo na Abu Ghraibu huashiria demokrasia na haki za binadamu enhe?
Mahaka ya Hague ina faida gani,kama watuhumiwa wa ugaidi wanafungwa Guantanamo Bay bila mtu kuhoji?
Wanavyo fanya hawa, kwenda Syria na kuua watu ni sawa na anavyofanya Kagame bila kuulizwa-double standards- sasa Hague ina faida gani hapa Afrika?
Inaona makosa ya akina Uhuru Kenyatta,Ruto,Gbagbo na Watu Weusi wasio na maslahi na Magharibi tu?
Wenye masikio na wasikie.Ni uzumbukuku kusema Afrika ina madikteta wakati baadhi yao ni vibaraka wa maslahi ya Marekani,mwingine akikosea anakatwa na kufungwa jela Hague.
Charles Taylor kafungwa Ulaya miaka 50 kwa kufanya unyama Afrika,kwa hiyo Afrika hakuna jela? Uzumbukuku waMwafrika!
Mwafrika,Bensouda na wenzake,kaajiriwa katika mahakama ya Mzungu ili kumfunga Mwafrika mnashangilia! Ndiyo haki na kuondoa Impunity Afrika!!
Makampuni ya mafuta na gesi huleta vurugu Afrika na kuua watu,kampuni za madini hutiririsha kemikali na kuua watu na wanyama Tarime na kwingineko Afrika, hii kesi haina mashiko The Hague wala kokote! Upumbavu gani huu nyie?
Wao wakiua watu Afrika nani awashitaki The Hague? ICC ina wanachama 66 miongoni mwa zaidi ya nchi 200 duniani,hizo nchi 130 hazijalaumiwa kwa makosa?
Wanashitakiwa wapi? Marekani si mwanachama wa ICC, tumshitaki wapi?
Kenya wanapojiondoa ICC akili zilizoganda zinasema ni hatari! Hatari Kenya kuondoka ICC wakati nchi 130 ikiwemo Marekani yenye makampuni ya mafuta yanayochafua mazingira Nigeria n.k mbona hailazimishwi?
Ken Saro-Wiwa aliuawa na nani wewe kama siyo kampuni ya Shell ya Uingereza,Chevron na Royal?
Tusifikiri kwa kutumia tumbo;tutumie kichwa. Fatou Bensouda hawezi kuajiriwa mahakama za Afrika akatoa haki hadi Ulaya tu?
Tuutafute ukweli kwa darubini,Bensouda anaweza kusaini waranti kumkamata Obama kupeleka vita Syria kinyume cha sheria za Umoja wa Mataifa?
Ukoloni mamboleo ulishajaa akilini mwa watu wanadhani Afrika ndiko kwenye makosa na vita. Magharibi wakipeleka silaha Kongo wakawapa akina Kagame maelekezo kufanya vita,utalaumu Afrika?
Charles Taylor akitolewa jela,akapewa assignment kusaidiana na Fodday Sankoh kuua na kupora almasi,utasema Dikteta na Taylor tu anayestahili kufungwa na akina Sankoh kufia ICC?
‘Critical Mind’ inaweza kutambua ninachokitazama hapa,na waafrika mbumbumbu ni sumu ya maendeleo na uhuru wan chi,demokrasia na harakati za kweli.
Tazama vyama vyenu vya siasa vinavyokunja mikia miguuni kwa akina Cameron,Bush n.k wanaamrishwa ushoga n.k halafu mnasema ni NGUVU YA UMMA wa akina nani?
IMF,WB,WTO,ICC nk ni colonial tools za kumkandamiza Mwafrika hadi awe Mtumwa kifikra,ukiambiwa ukweli unakasirika na kusema Mwafrika ni dikteta.Hongera Kenya kukataa ukoloni.
Itaendelea



No comments:

Post a Comment