Tuesday, September 17, 2013

wahalifu wa Afrika

JENERALI KAGAME NA MUSEVENI

 
ALIPOTANGAZWA mshindi wa kiti cha Urais, Rais Emilio Mwai Kibaki wa Kenya ,  mwaka 2007,hazikupita siku nyingi, Museveni akatambua ushindi wake na kumpa pongezi.
   Licha ya lawama na makelele, kwamba Tume ya Uchaguzi ya Kenya(ECK) iliiba matokeo na kumpa Kibaki ushindi, rais Museveni alimpongeza Kibaki  kwa ushindi.
 Alisema ukweli ulio kuwemo moyoni mwake.
  Wapo watu walimlaani Museveni kwa kitendo hicho.
 Walitegemea aliaani upungufu katika Tume ya Uchaguzi(ECK) aliyoiunda Rais mwenzake.
Tanzania kuna Tume inayoundwa na Rais.
 Zanzibar(ZEC) ilitangazwa  na Rais Karume.
 Hata Kenya ilikuwepo Tume ya Mwai Kibaki.
   Nadhani, Rais anapokosoa tume aliyochagua yeye, anajikosoa mwenyewe; kisha anapokosoa tume ya Rais mwenzake, anamkosoa Rais mwenzake pia.
Rais Museveni hakutaka kumkosoa mwenzake kwa yaliyofanyika; hata kama hayakwenda sawa.
   Hili la Rais kuteua Tume ya Uchaguzi ili imwondoe yeye mwenyewe madarakani nadhani ni tete kidogo.
Demokrasia ya Afrika inawajibu wa kutazama upya muundo wa Tume zenyewe, ambazo wengine wanaziita, ‘huru za uchaguzi’.
 Nadhani Kenya ECK illitwa huru kabla ya ‘kumchagua’ Rais Kibaki.
    Naam. Nampenda Rais Museveni kwa kushindwa kuwa mnafiki kwa kumpongeza Rais mwenzake kushinda nchi jirani.  Yuko wazi,ili kila mkazi wa Afrika ashariki apate kujua Museveni ni mtu wa aina gani?
Hivi watu walitegemea Museveni amtambue Raila Amolo Odinga wakati huo?
   Je, kama Museveni angemtambua Odinga, halafu Kibaki akasalia madarakani,(alikwishatangaza Baraza la Mawaziri), hata baada ya akina Gordon Brown na wajumbe wa Bwana mkubwa Bush kushindwa kupata suluhu, ingekuwaje mwaka 2007?
   Hivi, John Kufour angeshindwa kuwapatanisha Odinga na Kibaki, na Kibaki akasalia madarakani, watu walitaka urais wake usitambuliwe?
Hayo yalipita,ingawa watu 600 walipoteza uhai,wengine 1400 wakakosa makazi na kutimkia huku kwetu Tanzania. Tuyaache.
    Jenerali Yoweri Kaguta Museveni ni jasiri; nitaeleza historia yake.
Rais Jakaya Kikwete alipokwenda Washington  mara baada ya kuapishwa, Bush akamchokonoa kuhusu kelele za Kenya .
 Aliposema kidogo tu kwamba huenda watatoana macho na kutwangana ngeu, watu wakamtukana kwamba, aliingilia mambo ya nchi hiyo!
Ilikuwa 2007,na kweli walitoana ngeu wakakimbilia hapa kwetu Tanzania. Walikasirika wakati huo kama Kagame anavyokasirika sasa;
 
   Kwanini azungumze mambo yetu na Bush? Kwani nani kamchagua Kikwete kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya?” walisema.
 Kwa kuwa hata uchaguzi mkuu uliopita yalikuwa  ‘mambo yao ’ ndiyo maana Kikwete angali kimya.Hata hivyo alikwenda kuwapatanisha wakaacha vita.
 
   Nakiri, safu hii siyo msemaji wa Rais Kikwete, juu ya kuchelea kuonyesha msimamo wake  juu ya nani  alikuwa mshindi halali Kenya mwaka 2007 .
Wapo wanaomlaumu kwa ukimya wake; wanadhani kulaani ni kupayuka tu kama tunavyofanya katika vijiwe vya kahawa!
Haya yalishapita,Wakenya walishayasahau na kuganga yajayo.
    Naam. Museveni nampenda sana . Anasema anachofikiri.
 Kwamba Kibaki alikuwa mshindi kulingana na tangazo la Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Nchi hiyo. Wewe Tume ya watu imesema Bush kamshinda Alfred Gore (mwaka 2000), halafu nyie mnasema hakushinda!
 Mbona basi  AlGore alikiri kushindwa mwezi mmoja baadaye, ingawa kesi ilikwenda mahakamani?
    Wapo watu wanadhani mtu kushinda uchaguzi ni kupata kura nyingi za umaarufu(Popular vote); na wengine wanadhani Rais mzuri ndiye aliyependwa saana.
 Rais mwema anamjua Mungu.
Mfalme Sauli alipewa kura nyingi na Waisraeli wa kale kwa sababu tu alikuwa mrefu na ‘handsome’ lakini akaja kuboronga sana na kukiingiza kizazi katika ushirikina mkubwa… Mungu hafuati urefu wa Mfalme wala kura nyingi za wapigakura mbumbumbu.
    Wala safu hii haitetei wizi wa kura wa Rais yeyote.
Isipokuwa, ni vigumu Rais wan chi moja kuanza kumkosoa mwenzake.
Hapa kwetu kuna madai ya wizi wa kura yaliyotolewa hata kabla ya uchaguzi wa Kenya .
 Kibaki alimkosoa Rais Karume au Mkapa?
   Mseveni mwenyewe alidaiwa kuiba kura Uganda na kumsweka rumande Kanali Dk Kizza Besigye.
Kibaki alikosoa udikteta huo wa kumsweka rupango mpinzani wa Museveni?
    Forum for Democratic Change(FDC) cha Dk. Besigye, kimekuwa kikilalamika kwa kufanyiwa mchezo mchafu na  National Resistance Movement.
Rais gani hapa Afrika aliyekataa kutambua ushindi wa Museveni; na kutambua ule wa wapinzani?
    Wafuasi wa Besigye jijini Kampala walipata kupigwa mabomu ya machozi na risasi za mipira hata za moto, walipopinga kukamatwa kwa kiongozi wao.
 Rais gani alimkosoa Museveni hadharani, achilia mbali kutotambua ushindi wake halali toka kwa Tume yake ya Uhaguzi?

No comments:

Post a Comment