Wednesday, September 25, 2013

KAGAME NA MUSEVENI NI NOMA



APRILI 6 mwaka 1994,Rais wa Rwanda, Juvenal Habyariana, na  mwenzake wa BurundI,Ntaryamirwa Cyprian, wakiwa ndani ya ndege aina ya Falcon-50, wakatunguliwa kwa kombora na Waasi wa Kitutsi,RPF.
Huu ndiy mwanzo wa mauaji ya Halaiki ya Rwanda,nakichocheo cha vita Burundi na hata Mashariki mwa Congo,JK Kongo.
Migogoro ya Watu-tsi na Wahutu,inayotiwa mafuta na Mabwana wa Vita(WAR-LORDS)Paul Kagame na Yoweri Kaguta Museveni,sasa cheche zake hutishia hata amani ya Tanzania.
Wakimbizi maelfu wanakimbilia hapa Tanzania,kufuatia vita baina ya Wahutu na Watu-tsi wa Rwanda,Burundi na hata walewaliotimkia Jamhuri ya Kongo,kwa sababu na muda tofauti.
Tuwatazame wanaojiita Waasi wa Congo,M-23,CNDP na FDRL wanaosababisha Jenerali Kagame aanze kututukana huku.
FDRL(Democratic Forces for The Liberation of Rwanda) ni kikundi cha wanamgambo wa Kihutu ambao ni adui wakubwa wa KAGAME na nduguze Watu-tsi.
Kama jina lao lilivyo,baada ya mauaji ya halaiki, wakatimkia Congo ambako hata leo wanaota kumtimua Kagame mamlakani.
Hawa,ni Wahutu(raia wa Rwanda0 wanaompinga Kagame.
Sasa,Rais Jakaya Kikwete akiwa Addis Ababa, akamshauri Kagame ambaye naye alihudhuria moja ya mikutano ya AU kukaa meza ya mazungumzo na hao Waasi wa Kihutu wa FDRL ili kuleta amani na utangamano Maziwa Makuu,likawa kosa kubwa kwa Kagame na kuanza kurushamakombora ya  kama alivyozoea.
Kingalipo kikundi kingine cha wanamgambo wa Majimaj(Mai mai) ambacho pia kimejichimbia misitu ya CONGO ,kinapeleka mauti huko Jamhuri ya Congo,kinaitwa ADC.
Ndani ya Congo kuna jamaa zake Kagame na rafikiye,Museveni yaani M-23.
Jina hili hutokana na tarehehe 23 Machi mwaka 2009,siku ambayo serikali ya Congo ilifikia makubaliano ya Amani na kundi la Waasi wa CNDP,wakajumuishwa katika majeshi ya serikali.
Naam, hawa ndiyo M-23 Movement ambao ni kikundi cha Waasi kama 5,500 hivi waliojichimbia Kivu ya Kaskazini na kuuza kifo kwa raia wa Kongo,na hapa kwetu wamesababisha kilio kwa kupoteza wanaeshi wetu.
Wametokana na misuguano isiyoisha baina ya serikali ya DRC na hawa wanaojiita Waasi kwenye mipaka ya Uganda,Rwanda na Burundi.
Hawa M-23 wametokana na CNDP(Congress for the National Defence) kilichoanzishwa na ‘jamaa’ za akina KAGAME na Museveni,mmoja anaitwa Jenerali Nkundabatware,Desemba 2006 huko Kivu.
Januari,2009 CNDP Kilikosa umuhimu,kikaparaganyika,hadi eti Nkunda akakamatwa na majeshi ya Rwanda,ambayo sote tunajua yalimpa chakula,nguo,fedha,silaha n.k
Sehemu ya kundi hilo Iliongozwa General Bosco Ntaganda, ambacho kiliingia mkataba wa amani na serikali ya Congo Machi 23, mwaka 2009.
Wapiganaji hawa walipounganishwa na jeshi la Congo,CNDP kikawa chama cha siasa,wanachama wao wakaachiwahuru magerezani.Rais wa kundi hilo akiitwa Askofu Jean-Marie RUNIGA Lugerero!
Utaona ‘maaskofu’ wa siku hizi wakiongoza vikundi vya wanamgambo na kuua raia! Jihadhari sana na wanaojiita Maaskofu,Manabii na Mitume wa siku hizi!!
Rais wa kundi la M-23 akiitwa ‘General’Makenga Sultan-wote hawa mabwana wa vita walikuwa CNDP.
Hawa hawakuwahi kuaminiwa na serikali ya mjini Kinshasa,hata baada ya makubaliano,Rais Joseph Kabila wa Kabange aliamuru Jenerali Nkunda akamatwe Aprili 11 mwaka 2012.
Hawa ni Watu-tsi,ambao ni adui wakubwa wa kile kikundi cha Wahutu cha Democratic Forces for the LIBERATION OF Rwanda(FDRL).Hawa wote wanaendesha harakati zao za kigaidi ndani ardhi ya Congo,ndiyo maana kuna shida kila kukicha.
Bila shaka, msomaji unapata picha kwamba, kuna vikundi vya Wahutu(FDRL) waliokimbia Rwanda wakati wa genocide, walitimkia Cogon a huko wanaendesha harakati za kumpinga Kagame.
Hawa Watutsi walimsaidia Papaa Kabila(baba0kumwondosha Mobutu madarakani, na baada ya vita hivyo,walijumuishwa katika majeshi ya serikali.
Hawa Watu-tsi, wanapokea msaada kutoka Rwanda na Uganda, eti sasa mazungumzo ya kuleta amani Congo hufanyika mjini Kampala chini ya usimamizi wa Kaguta Museveni! Kichekesho kikubwa.
Majeshi ya serikali ya mjini Kinshasa(FARDC) yamekuwa hayawezi kuwatimia hawa jamaa za Kagame na Museveni huko Mashariki mwa Kongo,kwa sababu ambazo sasa tayari umeziona kufuatia mfululizo wa makala haya.
Wakati mwingine, majenerali wa FARDC walijidai kujisalimisha kwa Waasi,wakawapa zana za vita na chakula katika kinachoitwa ‘mapigano makali’ ambamo Waasi wanawateka askari wa serikali!
Wanafanya usanii huo huku majeshi ya Umoja wa Mataifa(MONUSCO) yakiangalia hata ujambazi unaofanywa kwa raia wa Congo.
Hawa MONUSCO wakati mwingine kazi yao ni kupora madini na kuuza Ughaibuni,na wala siyo kulinda raia wa Congo kama walivyotumwa na Umoja wa Mataifa,
Baada ya majeshi ya Tanzania kujumuishwa katika jeshi la MONUSCO, sasa kampeni ya kuwaswaga hao M-23 inaleta tija,wanapigwa ilivyo,ndiyo maana wanasisitiza mazungumzo kuendelea Kampala,ili ikiwezekana warejeshwe jeshini Kinshasa,viongozi wao wapewe mishahara na serikali ili wadumu kufanya ujambazi!
Watanzania tunasema kwa uchungu mkubwa kwa sababu tumekwishamwaga damu ya askari wetu huko Kongo, tayari M-23 ni adui yetu wa dhati,ndiyo maana Kagame anachuki ya wazi kwetu.Ingekuwa heri Umoja wa Mataifa ungeongeza jeshi ili hawa waasi watwangwe vilivyo,wanapoingia Rwanda kupewa chakula,nguo na bunduki,Rwanda wapewe kibano!
Kuna njia tele za kuipa kibano serikali ya Kagame ikiwa ni pamoja na Vikwazo vya kiuchumi, ama kunyimwa msaada wa kijeshi na kuuziwa silaha na mafuta.
Kuishinikiza serikali ya Kinshasa kuzungumza na Waasi,wakati kukiwa na wakimbizi 200,000 au zaidi wanaokimbia mapigano huko Goma,kuna leta ukakasi.
Kagame akiambiwa kufanya mazungumzo na FDRL anakasirika;wakati hao M-23 wakitwangwa vikali na maiti zao kubanikwa na majeshi ya serikali, kelele zinapigwa za mazungumzo mjini Kampala!
Mazungumzo hayo yalianza Desemba 9,mwaka 2012.
M-23 ilianzishwa rasmi Aprili 4,mwaka 2012 wakateka Goma kirahisi sana,kabla ya Makomandoo wa Tanzania kuwachakaza vikali hao Waasi na kuwatimua Goma chini ya mwamvuli wa MONUSCO.
Hawa jamaa za Kagame sasa wamejificha Rwanda! Inasemwa wako mpakani,huku makombora yanapodaiwa kutua Rwanda ili kuwasindikiza huko,ama wanafanya mchezo wa kuchongea kwamba MONUSCO wameivamia Rwanda!
Rais Kikwete anapotaka Rwanda inayoongozwa na serikali ya RPF(ya Watu-tsi) kukaa meza moja na Waasi wa Kihutu,FRDL waliokimbilia Kongo ili kuongeza vurugu huko maana yake nini?
·       Kwamba,ni mazungumzo ya amani wanayotaka Kagame na Museveni na jamaa zao wa M-23 waongee na serikali ya mjini Kinshasa.Ni sawa na namna ambavyo Kagame angezungumza na FDRL ili kuleta amani Maziwa Makuu.
·       Hata RPF(Rwandan Patriotic Front) walipokuwa Waasi wa Rwanda walianza kuzunguza na Habyarimana.
·       Mazungumzo ya mani(Peace talk and cease fire agreement)mwisho huweza kuzaa mikataba ya amani(peace accord) na kuleta amani na utangamano kati ya nchi za migogoro.
Sasa tujiulize Kagame anapojidai kutuliza uhasama kati ya Watu-tsi na Wahutumbaada ya genocide mwaka 1994, anaposhauriwa na Kikwete kuzungumza na FDRL anakasirika nini?
Ili kuleta usalama Mashariki mwa Kongo Waasi wa M-23,CNDP,Maimai n.k wanapozungumza na serikali ya Kabila mjini Kampala, si busara pia Kagame kuzungumza na Wahutu wa FDRL mezani sasa ili kualiza vita Ukanda wa Maziwa Makuu?
Mbona hata Waundi wamekuwa wakipatanishwa na akina Nyerere,Mandela,Bill Clinton,Mwinyi n.k
 Hawa walitia saini makubaliano ya amani mjini Arusha mwaka 2000 chini ya Mandela na Clinton.
Ndiyo maana,wanamgambo wa Kitu-tsi walioko Kongo tunasema wametumumiwewa kuangamiza Wahutu waliokimbiliahuko! Wahutu nao ni binadamu,wahurumiwe.
Rais Kikwete anajua mambo haya, alipomwambia Kagame kuzungumza na FDRL ligusa kizinga cha moto wa visasi,moto ukalipuka.
Wapo watu wanasema:
“Kikwete,kama siyo kuropoka,imemhusu nini kuingilia Rwanda dhidi ya Waasi wa FDRL?”
Swali la kijinga kwelikweli!
Hawa waasi ama Wakimbizi wa Rwanda wanapokimbilia Kongo,hususan Wahutu wanapoleta balaa la vita huko, ama wanapokimbilia kwetu,Kagame na Museveni hawatakuja hata huku kwetu kuwasaka Wahutu ili kulipa kisasi?
Tumeeleza kisa cha mauaji ya Kanungu zama za Kibwetere.
Tumezungumza umuhimu wa Amani Maziwa Makuu.
Wanamgambo wa Intarahamwe-adui za Kagame-ni wakimbizi wa vita kama wakimbizi wengine.
Sheria gani inasema wawindwe na kuuliwa tena katika ardhi ya Kongo?
Kwa nini wasizungumze kama Kongo wanavyozungumza?
Mbona tunazuia genocide(1994) ili kufanya genocide nyingine dhidi ya Wahutu wa FDRL?

R




No comments:

Post a Comment