Monday, January 7, 2013

ati,Marekani na Ulaya kuna demokrasia?=5



         
MATAIFA MAKUBWA ya Ulaya na Marekani, ambayo pia yana sauti kubwa ama kura ya veto katika Baraza la  Usalama la Umoja wa Mataifa, yanaiburuza Dunia kupindukia.
Walioumizwa na Marekani,Uingereza na Ufarasa na washirika wao ni wengi hapa Duniani.
Kuna AJENDA YA SIRI ya mataifa haya babe sana kuitawala  dunia wakati wote, na pia kuiweka katika mikono ya mawakala wao.
Martin Luther,yule Kasisi wa Katoliki aliuliwa huko Ujerumani zama za Matengenezo ya Kikristo(Christian Reformation),yupo Martin     Luther King Jr wa Marekani,Malcom X(Malik al Shabaaz) alipigwa risasi na Majesuits mwaka 1963,Bruce Lee, mcheza filamu maarufu aliuliwa huko Hong Kong.
Nikusimulie kidogo kuhusu meli ya TITANIC,ambayo hata BCBG wameimba juu yake.Ilianza kujengwa 1909 huko Belfast,Ireland chini ya kampuni ya White Star.
Ilianza safari zake Aprili 10,mwaka 1912 iliongozwa na Kapteni SMITH ambaye alipewa maelekezo kwenda Atlantiki kwenye mabonge ya barafu ili kuigongesha meli hiyo na kuua watu.
Nataka nikwambie msomaji. Kulikuwa na matajiri wenye mali,wenye fedha nyingi.Mali zao zilikuwa za thamani ya Dola Bilioni 12 ambao wote walizamishwa Aprili,mwaka 1912.
Hawa ni Benjamin Giggenheim,Isidor Strauss ambaye alikuwa Meneja wa Marcy’s Department Store,na John Jacob Astor.
Hawa walikuwa matajiri wa Kimarekani na walikuwa wapinzani wakubwa wa AJENDA YA SIRI ya kuitawala dunia kwa nguvu ya pesa,nguvu ya utajiri,kupitia mabenki makubwa kama Benki ya Dunia(WB) na Fuko la Kimataifa la fedha(IMF).
 TUREJEE kidogo katika somo la Kuzama kwa Meli ya Titanic.
Kwamba, ilizama kwa maelekezo ya Freemasons.
ahodha wa Meli ya Titanic, E.J.Smith, alielekezwa kuizamisha meli ili kuwaulia mbali matajiri waliokuwemo.
 Matajiri hawa walioangamia katika ajali hiyo  ni John Jacob Astor,Archibald W.Butt,Charles M. Hayes,na mkewe na binzi zao, W.T.Stead,Benjamin Guggenheim, F.D.Millett na G.D.Widher.
Wengine walioangamia ni Isidor Strauss, na mkewe,J.B Thayer,J,Bruce Ismay,Henry B. Harris na mkewe na Washington A.Roebling.
Sina haja ya kulumbana na mtu kwamba Freemasons ambao kimsingi ni mawakala wa Ibilisi hawasababishi ama wanasababisha kutokea kwa majanga.
Sote tunajua kuna nguvu mbili zinazoshindana duniani, nguvu ya wema na ile ya kufanya mabaya. Freemasons ni mawakala wa Ibilisi wenye kazi maalum ya kuhadaa watu,wakidhani wanafanya mema.
 Hata hivyo, Alex Mayoge wa Moshi,Kilimanjaro aliniandikia SMS kusema kwamba TITANIC ILIZAMA ili kuwaua matajiri hao ili Freemasons wapore fedha zao kwenda kugharimia VITA VYA KWANZA VYA DUNIA.
Titanic ilizama Aprili 1912 na ni miaka miwili baadaye,mwaka 1914 vita kuu ya kwanza ya Dunia ikaanza kwaka 1914.
 Vita vina  lengo Fulani, na aghalafu vita wanavyoanzisha Freemasons ni vya kupora rasilimali ama kuweka mamlaka yao mahali wanapopingwa,nguvu za ushawishi zinaposhindikana.
Unaweza kuona vita visivyokwisha Jamhuri ya Congo,ukaona ni nani chimbuko la vita vile kama siyo Mataifa makubwa?
Vita vya Pili vilianza 1939 vikakoma 1954. Tulishajadili jambo hili kwa kina,na anayetaka aangalie Blog yangu kuhusu vita hivi na matokeo yake.
Malengo ya maharamia hawa yangalipo duniani,ndiyo maana kuna vita leo Congo na maeneo mengine kama Mali na tuliona Revolutionary United Front wakipewa silaha kuharibu serikali ya mjini Freetown,ili wapore ALMASI ZA DAMU.
Mwisho wa siku Fodday Sankoh alikamatwa na kupelekwa The Hague ambako eti alifariki ama kunyamazishwa, leo niandikapo hapa Taylor amehukumiwa kifungo cha miaka 50 kinachotekelezwa   huko jijini London,Uingereza.
Wapo Marais hata wa Marekani waliowahi kuuliwa kinyama kwa sababu walikataa kukubaliana na sera za mabwenyenye za kupeleka vita kote duniani,ili wapore rasilimali.
 Abraham Lincoln, McKinley  na wenzao wengi.Walitafuta vita fedha za kugharimia vita vya kwanza vya dunia. Hitler mwanzoni alijiunga katika vita hivi vya kwanza,ili ajipatie mshahara,maisha yake yalikuwa magumu.
Baadaye, mwaka 1939 wakaanzisha vita vua Pili ya Dunia kwa udhamini wa Makampuni makubwa kama ROTHSCHILD,na Federal Reserve Bank.
Ukiona Waasi wana silaha katika nchi Fulani,ujue zimenunuliwa na magenge ya matajiri Fulani ili kutimiza majukumu Fulani.Hawa watalipwa mishahara na gharama za vita zinalipwa kwa fedha kutoka mahali Fulani,ili matokeao yake maslahi Fulani yapatikane.
Sasa watu wajinga wakisikia kuna Uasi labda Congo au Jamhuri ya Afrika ya Kati(CAR) wanadhani uasi huja hivi tu.
Kunakuwa na fungu la pesa kutoka mabenki haya makubwa ya Ulaya na Marekani,na wanapigana vita kwa lengo mahsusi,siyo tu kumwondoa mtu Fulani madarakani.
Wengine wamekalia kujilaani sisi Waafrika,hawajui vita na machafuko huchochewa kutoka Ulaya au Marekani kwa lengo la kuchukua rasilimali Fulani na kutimiza MASLAHI yao.
Njama kama hizo ndizo zilizowahujumu Wayahudi milioni sita.Umewahi kuona filamu iitwayo ESCAPE FROM SOBIBOR?.Sobibor ni Poland,waliuliwa Wayahudi hususan watoto wa kiyahudi katika makambi ya mateso.Itafute filamu hiyo uone.
Leo, wewe unapoona vifo cha akina Saddam Hussein akina Osama bin Laden ambao kabla walikuwa washirika wa CIA,usifikiri sababu wanazokwambia wao.Gaddafi alikuwa mshirika wao wakaja kukosana,sasa waliitaka roho yake kama walivyoichukua ya Jonas Malhiero Savimbi wa UNITA huko Angola.
Wakimuua mtu kwa sumu au kwa risasi,utasikia wanatangaza kafa kwa maradhi ya moyo au kisukari ama ajali.Nilishasimulia kifo cha Princess Diana,kwamba kilitekelezwa na maajenti wa majasusi wa Uingereza na Ufaransa.Usikose kusoma safu hii.
Hata vuguvugu la siasa za Tanzania haliko salama,limeingiliwa na majasusi hawa na yumkini uchaguzi wa 2015 ukaleta kasheshe!!
Kuna visingizio vingi ili kuuhadaa Ulimwengu.Unakumbuka David Coresh la kundi la Branch Davidian?
Labda ulikuwa motto mwanzoni mwa miaka ya 90.Walisingiziwa kuwa walikuwa na silaha za hatari na kwamba walitaka kuangamiza watu katika jengo la MAOUNT CARMEL huko Waco,Texas.
Wale Branch Davidians walizingirwa na FBI na askari wa kudhibiti madawa ya kulevya(BATF) wakawashambulia Branch Davidians kwa risasi,sumu na kuwachoma moto.
Propaganda zikasema kwamba walibaka watoto wa washiriki wao,waliwaua wote na sababu kubwa ni MISIMAMO YAO MIKALI,  “extremism” kama akina Gaddafi,Osama,Saddam na wengine watakaokuwa na misimamo kama hii huko tuendako.
Tunakwenda kwenye pesa mpja,uchumi mmoja,dunia moja. Hapa Afrika Mashariki tumeshaanza kutekeleza masharti yao kwa kutumia pesa moja ya Afrika Mashariki,East African Monetary Union(EAMU),sasa wewe jitie ‘extremist’ utajuta kuzaliwa.
Kuna mauaji zaidi ya watu 520 huko Kanungu,Uganda zama za Kibwetere. Kuna vifo vya akina J.F Kennedy.
Ilikuwa Ijumaa,Novemba 22 mwaka 1963.Saa 6.30 mchana kweupe,JF Kennedy alipouliwa kwa risasi na Lee Harvey Oswald.
Ikaundwa Tume, Warren Commission kuchunguza kifo cha JF Kennedy. Nimesimulia katika mfululizo huu jinsi alivyouliwa Princess Diana,ikaundwa Tume,Paget Probe, ikaishia kuficha ukweli na kusema uongo.
Marekani walificha kifo cha JF Kennedy,na siku mbili baadaye, Jack Ruby akamuua Oswald,ili kumziba mdomo na kuficha ukweli.
Sababu za kifo cha Rais J F Kennedy,ilikuwa vita vya Vietnam, na siri waliijua Federal Reserve Bank.
Rais J F Kennedy alituma wapelelezi Vietnam,akina Mc Namara na Taylor, wakaleta Ripoti iliyomshauri Rais kuondoa majeshi Vietnam,akawakosea hawa mabeberu wa Ulaya na Marekani!
Waliazimu J F Kennedy aondoke wao waendeleze vita vya maslahi yao Vietnam.Sasa hata Obama hawazi kujidai kufunga Guantanamo au    Abu Ghraib huko Irak, ama kuwaondoa wanajeshi Irak na Afghanistan,atakosea atauliwa kama wenzake-ndiyo maana nikasema katika makala zilizotangulia kuwa Obama na Osama ni wale wale tu.
Makanisa nayo huchochea vita,Rwanda tuliona makasisi wakichochea vita.Makanisa huwa na watumwa,hasa ya Uingereza, Anglican lilikuwa na watumwa wa kulima mashamba,Barbados na kwingineko.
Madhehebu ya dini yameua watu wengi walioyapinga,hasa zama za Matengenezo-Christian Reformation.
Nataka ujue kwamba,a nayeongoza Marekani siyo Rais kama Obama,ni MASLAHI na walinda maslahi.Ukikosana na maslahi ya Marekani hata ukiwa Rais,unakwenda!
Wanaoongoza Marekani ni mabeberu,mafreemasons ambao hata Obama walishataka kumkataa wakasema ni Mkenya akazaliwa Kenya,naye akawafanyia ‘Umafia’ wa kusema alimuua Osama!
Basi,akapewa mhula wa Pili. Hata wauza madawa ya kulevya,MAFIA wana ushawishi mkubwa katika mataifa haya,ukijidai mjanja unauliwa kama Waziri Mkuu  Aldo Moro.
Wasimamizi wa maslahi haya ni Central Intelligence Agency, na wenzao na wamepandikiza mamluki hata KGB,KFB hata katika madhehebu ya kidini.
Fedha,dhahabu,almasi,ruby na madini yote na mafuta,gesi n.k hutafutwa chini ya usimamizi wa Benki Kuu ya Marekani, “Federal Reserve Bank” wanapanga mbinu,wewe unadhani inatokea kwa nasibu tu.
Ripoti za Tume zinazoundwa hudanganya watu wajinga.Baada ya mauaji wauaji hulipwa pesa na wengine huuliwa ili kuwaziba mdomo.
Haya ndiyo makosa ya akina Mahtma Ghandi,Idira Ghandi,Sanjay na Rajiv Ghandi.Waliwakosea wakubwa. HaPA Afrika kuna vifo cha mashaka kala vile vya Samora Machel,Garang,Sokoine,Kabila,Neto,Yitzhak Rabin aliuliwa na MOSSAD,Mwaka 1997. Mossad ni shirika la Ujasusi Israeli na washirika wa CIA.
Ogopa kuongoza Tume za mauaji ya watu kama hawa halafu ukasema ukweli,utapotezwa haraka!
Itaendelea




No comments:

Post a Comment