Monday, January 28, 2013

siyo vurugu,ni ukosefu wa kazi!!

      VURUGU  MWANZA
      Wananchi wadai mabomu ya machozi,risasi za moto ,magereza makubwa,  siyo suluhisho
Na conges mramba,mwanza
NI UKWELI USIOPINGIKA, kwamba Jiji la Mwanza linakabiliwa na ‘milipuko ya Volkano’ya machafuko mara kwa mara.yaletwayo na makundi ya vijana wasio na ajira rasmi,kila kunapokucha.
Kwa miaka mitatu sasa Mwanza inashuhudia,mirindimo ya risasi za moto,mabomu ya machozi na virungu, ambavyo hutumika kuwatawanya na kuwadhibiti vijana wenye mawe,magongo,matofali na magogo ya miti waofunga barabara,kuchoma moto magari na majumba,wakati mwingine huvunja maduka hususan ya wafanya biashara wa Kiasia na kupora mali nyingi za thamani.
Siku moja baada tu ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010,(Jumatatu,Novemba Mosi) makundi ya vijana,waliodaiwa wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA)walifunga barabara ya Makongoro iendayo Uwanja wa ndege,mahali paitwapo,Nera na kuichoma moto ofisi ya CCM ya kata ya Isamilo,ambayo iliteketea pamoja na mali nyingi za thamani.
Jumanne, wiki iliyopita(Januari 22,mwaka huu) katika barabara hiyo ya Makongoro,jirani na eneo hilo la Misheni na Nera, kundi kubwa la waendesha pikipiki maarufu kama ‘Bodaboda’ walikivamika kikosi cha polisi(TASK FORCE) kilichokuwa kikiendesha kampeni kamambe ya kudhibiti makosa ya Usalama Barabarani.
Ilikuwa saa 3.30 hivi,asubuhi, polisi waliwatia mbaroni waendesha Bodaboda wasiozingatia sheria na kuwatoza faini.
Wakavamiwa na makundi ya waendesha bodaboda na kupigwa mawe hadi walipolazimika kufyatua mabomu ya machozi na risasi za moto hewani,ili kuwatawanya.
Kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza,Ernest Mangu, amesema waendesha bodaboda wasiozingatia sheria waligoma kukamatwa na waliazimu kuwatorosha wenzao waliokuwa chini ya ulinzi.
“Hawakuwa na leseni,na wengine walipakia abiria zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja,maarufu kama mishikaki,hawakuwa na kofia ngumu,helmet,wakati mwingine hukatisha barabara na kuwagonga waenda kwa miguu na kutokomea pasipo kujali…tumeamua tu ‘deal’nao,tuliwatoza faini ndipo wakatokea wahuni kutaka kupora pikipiki zilizokamatwa kwa nguvu”,alisema Kamishna Msaidizi wa Polisi,Ernest Mangu,Jumanne iliyopita.
Kamanda Mangu akaongeza kuwa hao Bodaboda walikuja juu wakafunga barabara hiyo iendayo uwanja wa ndege kwa mawe makubwa na matofali,polisi wakawadhibiti na kuwatia mbaroni baadhi yao wengine wakatokomea.
Alisema kwamba, waendesha bodaboda 26 walitiwa mbaroni,10 kati yao wakalipa faini wakati wengine waligoma kufanya hivyo wakaanzisha vurugu.
“Tumewadeaka wanne wanaisaidia polisi na pikipiki 13 zilikamatwa za wale wengine waliotimka wakaacha pikipiki zao nyuma,wakichelea kutiwa mbaroni na kufikishwa mbele ya sheria”,amesema Kamanda Mangu akipa kuwa ni lazima jeshi la polisi lisimamie sheria za usalama barabarani.
“Hatutakubali Bodaboda wavunje amani ya nchi.Wanasababisha ajali nyingi;vifo vingi vya wasio na hatia,na hata wakimgonga mtu hukimbia,hawataki kusimama..tulifikiri tuwavumilie tuwafundishe kuihshimu sheria,kumbe hawataki…wamejipalia makaa ya moto vichwani!”amesisitiza.
Katika makabiliano hayo ya wiki iliyopita,hakuna aliyefariki dunia. Lakiki,katika matukio yaliyotangulia, watu walikufa ama kujirehiwa kwa risasi za moto.Mwaka 2004, wakati wamachinga wakichoma moto matairi barabarani,mtu mmoja alifariki kwa kupigwa risasi alipojaribu kuvamia duka la SH Amon,Barabara ya Nyerere.
Kamanda Mangu,alipoulizwa kuhusu hali za polisi waliodaiwa kujeruhiwa vibaya katika vurugu hizo, alisema alipatwa michubuko midogo tu,kitu ambacho hutegemewa kila mara na Jeshi hilo wakati wa makabiliano na wahalifu.
Mwaka 2011 makundi ya vijana waliojiita Wamachinga, walifanya vurugu na kuvamia maduka na nyumba za ibada za Wahindi katika mitaa ya Rwagasore,Lumumba,Makoroboi na Barabara ya Nyerere nakuvunja na kupora mali nyingi za thamani,huku wakisema ‘Wahindi waondoke’.
Vurugu hizo zilifuatia kampeni ya Halmashauri ya Jiji ya Usafi wa mazingira, hali iliyosababisha aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani,Shamsi Vuai Nahodha kufika Mwanza ili kujionea uharibifu.
Kulingana na wasifu, wa Jiji la Mwanza(Mwanza City Profile) Jiji hili lina watu wasio na ajira rasmi wanaovuka asilimia 30, ambao hukaa vijiweni kutwa wakisubiri machafuko yatokee ili wakapore ngawira madukani na majumbani mwa watu.
Kufuatia hali hiyo,Mwanza kuna makundi ya vijana na watoto wa mitaani, ambao huota vurugu iwepo ili wapore mali za watu.
Changamoto lilimuuliza RPC,Mangu kwamba sasa sura ya Jiji la Mwanza ni ipi,ikiwa RPC Liberatus Barlow kauliwa Oktoba 13 mwaka jana huko Minazi Mitatu,Kitangiri, maduka ya Wahindi na nyumba za ibada zimeporwa,majumba yamechomwa moto na vijana hawa?
Je,wawekezaji toka nje wanaweza kuwa na moyo mgumu kuja kuwekeza Mwanza yenye vurugu za wamachinga na waendesha bodaboda za kila siku?
“Mwanza ni shwari ka ukuaji wa uchumi na vitegauchumi,isipokuwa wakorofi wachache ambao tutawadhibiti”,alisema.
Wataalam wa Soshoolojia waliofanya mazungumzo na gazti hili wiki iliyopita,wamesema changamoto kubwa inayolikabili Jiji la Mwanza na makundi ya watu kutoka vijijini katika mikoa yote ya Kanda ya Ziwa,na hata Sindiga,Rukwa na Kigoma ili kuja Mwanza kutafuta ajira.
Wanapokuta ajira hakuna na maisha ni magumu,chakula hakuna,hujiingiza katika vitendo vya uvunjaji wa sheria.
“What the hell do you do about a whole generation of unemployed people? What they do is turn to crime”, wamesema wataalam hao kwa masharti ya kutotajwa majina,wakimaanisha kwamba kizazi cha wasio na ajira,wasio na kazi hugeuka kuwa wahalifu,endapo serikali haitafanya mkakati wa kuboresha uchumi na miundombinu ya uchumi huko vijijini ambako vijana hukimbia ili kuingia mjini kutafuta maisha.
Wananchi waliofanya mahojiano na Changamoto wamesema,kama serikali haitaanzisha  sheria ya Nguvu Kazi iliyokuwepo zama za Mwalimu Nyerere na kuboresha miundombinu vijijini,vijana watazidi kuingia mjini,kufanya vurugu na kupora mali za watu,wengine watakuwa bodaboda wasiozingatia sheria.
“Sheria kali,kuimarisha na kujenga magereza makubwa,magari ya upupu,mabomu ya machozi na risasi za moto hazitakomesha machafuko,fujo na maandamano na uhalifu wa kila siku Jijini Mwanza,ikiwa serikali na jamii hawatatafuta njia mwafaka ya kupunguza tatizo la ajira na wimbi la vijana kukimbia vijijini na ku

No comments:

Post a Comment