Thursday, January 17, 2013

MWANZA KUNA MASHOGA...

JANUARI MOSI,mwaka huu mpya,2013 nilikuwa Buswelu,katika Halmashauri mpya ya wilaya ya Ilemela, kwa mapumziko ya mwisho wa mwaka na mwanzo mwaka mpya.
Nimebaini kuwa wenyeji wa eneo hilo wameuza mashamba yao na kujiondokea.Wanapisha jiji linalokua kwa kasi ya ajabu. Mwanza ni Jiji la wakazi milioni moja, ambalo majumba ya fahari yanamea kama uyoga,na vitega uchumi vipya huanzishwa,zikiwemo taasisi za kigeni.
Inawapasa wenyeji kuuza viwanja na mashamba yao na kuuhama mji;wanatafuta pa kwenda kuishi.
Umasikini unapoongezeka vijijini, kuna watu hulazimika kuuza ardhi:Mashamba,viwanja na mifugo na kuingia mijini,wakijaribu kufanya biashara ndogo kwa mitaji midogo,ili kujinusuru.
Kufuatia hali hiyo ya baadhi ya wanakijiji kuhamia mijini, “Urbanization” hata Wazungu hununua mashamba ya wenyeji pembezoni mwa mji kama Buswelu,Buhongwa,Bugogwa n.k
Wakati wamasikini wa mjini huuza viwanja na mashamba na kujiondokea, wale wa vijijini huuza masahamba ma viwanja vibanda vyao na kuingia mijini,kujitafutia ajira,maana maisha ni magumu vijijini,na hakuna miundo mbinu.
Kwa sababu hiyo,ukosefu wa ajira, “Unemployment” unakimbia kutoka asilimia 30 hivi,kwenda asilimia 50.Ombaomba ni wengi,wengine huvalia suti na tai, na watoto wa mazingira magumu hashikiki.
Ukisikia ‘bomu’la watoto wa mitaani,basi Mwanza linakaribia kulipuka,litawalipukia watawala usoni.Mtu akiwapa chakula akawaambia waandamane na kufanya vurugu ama kupora maduka ya watu,hawatasita aslani.
Vurugu,maandamano na fujo za Mwanza,hufanywa na watu wa kariba hii,baadhi yao sasa ni watu wazima wasio na makazi.Huishi mitaloni na vibarazani mwa maduka ya Wahindi.Mvua yao,jua lao,na baridi za usiku wanazijua wao.
Vitendo vya ukahaba,ushoga,ujambazi,uporaji na unyang’anyi sasa hufanywa na kundi hili.
Jiji  kama New York, asilimia 80 ya wafungwa na wanaoswekwa rumande ni watu wa kundi hili,hususan Wahamiaji Weusi kutoka Latin Amerika au Caribbean.
Wakati watoto wa matajiri na wenye fursa bora za ajira na ukwasi, wakisoma shule na vyuo bora,wanajiandaa kushika nafasi za uongozi serikalini na katika jamii.Masikini hawana uchaguzi mwingine zaidi ya kuwa watumishi ama watumwa na watwana wa hawa ‘supervisors, principals and rulers’.
Licha ya serikali kuajiri polisi vijana na wengine askari wa Jiji,Mwanza hushuhudia uvunjaji wa sheria wa makusudi na mapambano ya kila mara ya wanamgambo wa Jiji,polisi na makundi ya vijana wanaojiita,Wamachinga.
Maisha magumu,husababisha uvunjaji wa sheria na vifo kila siku. Uhalifu,uvutaji bangi,ubwia unga,kutafuna mirungi. Hawa, “Drug addicted burglars” hutamani vita vitokee,wenye maduka makubwa, ‘shopping malls’ watimue mbio,wao wajimilikishe kile kinachosalia!
Nataka nikwambie,kwamba Mwanza hapa,vijana wanawachukia polisi na wenye mamlaka,kuliko kawaida. Mwanza kunanuka machafuko ‘violence’ kila kunapokucha,sababu kubwa ni umasikini kuongezeka-money shortage!
Watu wanakosa kulipa kodi ya pango(inaongezeka kila mchana na usiku),mtu huachia chumba na kwenda kujibwaga mtaloni.Fedha hazipatikani,ni balaa za pesa-financial doom.
Kila siku, polisi hufukuzana na machangudoa wanaouza miili yao katika mahoteli makubwa ya wageni,katika vilabu vya usiku na maeneo mengine ya starehe.
Unaweza kukutana na msichana wa mwaka wa pili au wa tatu katika Chuo Kikuu hapa, anajiuza ili apate mahitaji.Wengine ni wasichana warembo, na hawapendi kuitwa changudoa,wanataka waitwe ‘Wafanyabishara’ au watoa huduma ya ngono, “Commercial Sex Workers” kwa kifupi,waite “CSW”.
Maisha magumu eti yameleta uwekezaji wa ajabu na miradi ya kushangaza,biashara ya ngono,picha za uchi “Pornography”na zingine hupigwa na Wazungu mchana kweupe,wakati mamlaka ikiangalia,na kukosa meno.
YUNUS Santy, maarufu kama Angelo(67) alihukumiwa kifungo cha miaka  mitano jela, au kulipa faini ya shilingi 300,00 baada ya kupatikana na hatia ya kupiga picha za uchi na visichana viwili vyenye umri wa miaka 16 na 17.
   Angelo, ambaye ni raia wa Italia, alikutwa na visichana hivyo vyenye umri wa miaka 17(bila shaka wanafunzi) katika chumba cha Hoteli ya Paradise,iliyopo Unguja, jijini Mwanza.
    Alikuwa akifanya ngono na kasichana kamoja wakati kengine kakipiga picha ya tukio hilo. Pia, alikutwa na viungo bandia vya sehemu za siri za kiume.-toy boy.
Bila shaka, alikuwa akivitumia viungo hivyo bandia kuzima kiu ya ngono kwa visichana kama hivi.
    Ilikuwa Septemba 20 mwaka 2007, Mtaliano huyu aliyejitambulisha kama Mmisionari wa Kikatoliki, alipovichukua visichana hivyo katika mitaa ya jiji la Mwanza, akavipeleka hoteli ya Paradise(Paradiso) ili kula maraha!
      Wasichana hao wakaacha masomo ili kwenda kusaka pesa zinazosakwa leo kwa udi na uvumba, kuliko utu.
    Naam, Angelo aliposhindwa kutimiza ahadi kwa wasichana hao, walitoa taarifa polisi, ambao walimtia mbaroni kisha kumfikisha Mahakamani.
    Mwendesha Mashitaka, Inspekta Msaidizi wa Polisi, Inogu Kimasa, akaiambia Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Mwanza kwamba, Angelo ambaye ni Mmisionari wa Kanisa Katoliki, alifanya kosa la Jinai kinyume cha Sheria ya Kujamiana ya mwaka 1998.
   Siku chache kabla ya Siku Kuu ya Idi, Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Auqinea Lujwahuka, akamhukumu Angelo kifungo cha miaka mitano jela(alikiri kosa), au kulipa faini ya shilingi 300,000.
   Mmisionari huyo alilipa faini hiyo kwa kosa hilo alilotenda wakati wa mfungo wa Ramadhan. Hata hivyo, aliamuriwa kuondoka nchini, kwa sababu makosa yake yanakiuka sheria na Katiba ya nchi.
Akakabidhiwa kwa Idara ya Uhamiaji, mkoa wa Mwanza ili hatua za kumwondoa nchini zitekelezwe.Angekuwa Mswahili,bila shaka angefungwa kifungo cha maishajela au miaka 30.
     Hili ni tukio moja kati ya mengi yaliyoibuka wakati wa ujio wa Wazungu, wakiwemo watalii, wawekezaji wa migodi na wamisionari uchwara.. Hawa, wanatambua uzumbukuku, ulafi, ushamba na ulimbukeni wa wasichana wan chi hii kupenda sana kuzuzukia  kila kitu, mradi kililetwa na Wazungu.
      Naam, Filamu za uchi, “Nudie Film” hususan zile za ngono(sex film) hutengeneza pesa nyingi. Kwa sababu ya jamii tuliyomo kuwa na kiu ya ngono, anasa na pesa, filamu hizi hupendwa.
    Filamu hizi zina wateja wengi, watu wa kila rika, kila tabaka; hivyo wauzaji wa filamu hizi wananafasi ya pekee sana ya kutengeneza pesa nyingi na kujipatia maisha mazuri kwa kipindi kifupi.
   Watu wengi, hususan wanafunzi wa shule zetu za sekondari wenye umri huo wa kuanzia miaka 17 hupenda sana ngono na picha za aina hiyo.     Wasichana wa umri huu wamekubuhu sana kwa ngono kupitia filamu hizo.
   Hivyo, akitokea mtu mwenye fedha-awe Mmisionari au tapeli-akaahidi kuwalipa pesa wasichana hawa, atafanya atakavyo kwa hawa wengi sana. Watatoroka masomo, watafanya ngono hata na mbwa, midoli na chochote kile, mradi tu walipwe ujira kidogo, juisi na hata chakula cha mchana katika mahoteli haya ya Nyota Tano.
    Kisha, watarejea shuleni au nyumbani kwa na vizawadi vya kitoto, bila walimu, walezi na wazazi kubaini, ufirauni wa Wamisionari kama Angelo.
     Kwa kutumia fedha walizolipwa na akina Angelo, watanunua vivazi vya aibu, suruali za kubana sana makalioni na vijishati vinavyoacha vitovu nje. Watanunua vipodozi hata vya kugeuza midomo kuwa myekundu mithili ya radi.
   Angalia vitabu wanavyosoma watu hawa. Angalia magazeti wanayopenda kusoma. Ni yale yenye picha, maandishi ama filamu za ngono(Pornography).
       Vitabu vya ngono, magazeti ya watu wanaotembea uchi, au waliopigwa picha wakifanya ngono; na wengine waliofumaniwa! Magazeti ya aina hii hupendwa sana na watu wakizazi cha zinaa.
   Siku hizi kuna mitandao ya Intaneti; humo kunapatikana picha nyingi za ngono na za wasichana warembo walioacha utupu maungo yao ya tashtiti. Katika vibanda vyenye kompyuta za intaneti, tunaambiwa wanazuia watu kuangalia picha za ngono.
 Lakini, siku hizi hata katika simu za mkononi kuna intaneti; na mtu aweza kupokea picha ama kuzituma kwa yeyote. Siku hizi, visichana hujipiga picha vikiwa maliwatoni vikioga, picha hizo za utupu husambazwa kwa njia za kisasa sana kama ‘broadband’ wakati mwingine vitendo vya ngono na fumanizi hurushwa moja kwa moja.
Wiki chache zilizopita, zaidi ya wanafunzi 20 wa Seminari ya Nyegezi inayomolikiwa na Kanisa Katoliki,walitimuliwa masomo kwa kosa la kujihusisha na ushoga!Wavulana hao wa sekondari,walibainika ni mashoga,wakafukuzwa shule,kwa sababu Kanisa Katoliki limesema,halitavumilia matendo hayo ambayo ni kinyume na maadili ya dini.
Sasa,unaweza kuna namba Mwanza,vijana wa kiume na kike wanavyohama kwa kasi ya ajabu ‘KUTOKA ANOLOJIA KWENDA DIGITALI’.
Mwanza,kiunga cha Sodoma na Gomorrah,kwa sababu mamlaka inakaribia kurasilimisha biashara ya ukahaba na ngono-sexual entertainment businesses.
Biblia,inapinga ushoga:Mambo ya Walawi 18:22.Lakini katika zama hizi za maisha magumu na uchumi mbaya,nani amfuate Bwana Mungu ili akafe njaa?
Aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mwanza,Zelothe Stephen(sasa kastaafu) aliwahi kusema, “Haijatungwa sharia ya kuwatia hatiani watu wenye mwelekeo wa ushoga ama makahaba.Tunapowatia mbaroni,tunawashitaki kwa makosa ya Uzembe na uzururaji”, alikuwa akitoa maelezo kwa wanahabari juu ya mvulana aliyekutwa asubuhi akiwa kavaa heleni,vivazi vya kike, ana akiwa kapaka wanja wa midomo huko Mabatini!
Mwenyekiti wa Wenye Viwanda,Biahsra na Kilimo(TCCIA)Joseph Kahungwa, hawezi kusema biashara ya ngono nayo itambuliwe na Chamber of Commerce!
Labda,wanafanya hivi kwa kuwa Rais Jakaya Kikwete aliwahi kusema,Mwanza utajengwa ili kuwa mithili ya Los Angeles.Uwekezaji mkubwa!
Jiji lenye uhaba mkubwa wa ajira,lenye wahamiaji wapya,wageni wanywa mchuzi wa mbwa(hot dogs) fukweni mwa maji ya ziwa kubwa Victoria. Jiji hili ni vigumu ku ‘accommodate the latest influx or poor marching guys!
Jiji la vijana wanaoishi ghetto,ndani ya majengo ya magorofa marefu, skyscrapers, wakati wengi wanapoishi vilimani.Naam, mapangoni na mtaroni. Ndani ya makazi ya mbavu za mbwa-slums!
          Umasikini,panya,magofu ndani ya Jiji la fahari
Nihitimishe kwa kusema, Rais Jakaya Kikwete akifanya ziara katika makazi ya polisi,hususan Kigoto, atakutana na mabango makubwa ya watoto wa polisi na wake zao yameandikwa hivi:
“Rais tuokoe mapanya buku yanatumaliza huku!” Lingine litaandika, “Tumechoka kukaa katika maghala ya Wahindi kama pumba!” na linguine litasema,  “Walinda usalama wa raia wakati hatuna usalama katika magofu yaliyoachwa na Wahindi!”
Naam,Rais akifika Kigoto na kukumbana na mabango haya ya jamaa za polisi(nasikia polisi wenyewe wamekula kiapo cha kutoandamana au kubeba mabango kama raia wa Mtwara)basi Kikwete atashuka kwenye Limousine yake na kuahidi kuwasaidia hao akina mama wenye kuhema kwa kubeba mabango yenye ujumbe mzito! Ataahidi polisi kupewa makazi bora.
Vinginevyo,mapanya buku yaliyojazana katika magofu ya Kigoto wanakoishi polisi wa Mwanza,yatawamaliza vidole,yanakomba hata mboga chunguni! Usalama wa Raia pasipo usalama wa Polisi?
0786 324 074
 
 
 

No comments:

Post a Comment