Tuesday, December 11, 2012

AFRIKA KIZIMBANI

TUREJEE katika historia, ili kubaini namna Mtu Mweusi anavyodhalilishwa na kuonekana hafai, na si binadamu,bali mnyama!
Wanaoendesha vitendo hivyo,ndiyo hao hao wanaotazamwa leo kama wafadhili wa Afrika,na wenye huruma kwa wananchi wetu.
Zama za harakati za kupinga ukoloni,Mzungu aliitwa, Wasumwa Makaka!Kwamba zimwi lililowameza waafrika!
Husababisha vita hapa Barani,kwa madai ya kuwaondoa madikteta ili kujenga demokrasia na Haki za Binadamu.
Hufadhili harakati tele Barani Afrika,zikiwemo Haki za Binadamu,hata mashoga na wasagaji…hawa si lolote bali wabaguzi wa rangi!
Nitakwambia wewe uliyezaliwa baada ya mwaka 1970.
MWAKA 1936 Mmarekani mweusi ,James Cleveland Owens,(aliyezaliwa Septemba 12,1913 na kufariki dunia Machi 31,1980),aliwashinda Wazungu wabaguzi wa rangi waliokuwa wakiongozwa na Dikteta wa Ujerumani, Adolf Hitler.
 
Ni katika uwanja wa Olympic Stadium ulioko Berlin; ambako ndiko fainali ya Kombe la Dunia zilipohitimishwa Julai 9,mwaka 2006.
Berlin ni kielelezo cha kutokomeza ubaguzi.Berlin,kabla ya Ukuta wake kuangushwa mwaka 2004,ulikuwa kielelezo cha ukoloni wa kutisha,ndipo Bara la Afrika lilipogawanywa mwaka 1884.
 
James Cleveland, ambaye alikuja kuitwa na Mwalimu wake “J.C”. kama kifupi cha jina lake; ndiyo asili ya jina la Jesse Owens, aliyeweka rekodi nne za Dunia kwa dakika 45 tu mbele ya Dikteta wa Ujerumani, Adolf Hitler, aliyetaka kutumia mashindano ya Olimpiki ya Berlin mwaka huo wa 1936, kuuonyesha ulimwengu kwamba mtu mweusi ni dhalili; tena siyo binadamu, bali mnyama!
 
Jesse Owens , aliweka kwanza rekodi ya mita100, akashinda mita 200, akashinda tena kuruka juu, kabla ya kuongoza wenzake wane katika mbio za kupokezana vijiti.
 
 Hitler aligoma kutambua ushindi wa Owens, kwa madai kuwa hakuwa binadamu, sawa na mzungu! Naam, Mzungu alikuwa binadamu, Mwafrika mnyama!
Unajua Mohammed Ali,yule bingwa wa mabingwa wa ndondi duniani alikuwa akiitwa, “Clay” yaani udongo mweusi wa mfinyanzi?
 Unajua,Mohammed Ali, alipokataa kwenda kupigana vita vya Vietnam alipokonywa taji la Ubingwa wa dunia? Ilikuwa miaka ya 1967-69 hivi.
Hitler, kama wabaguzi wenzake wa rangi, aliamini kuwa mtu mweusi alikuwa dhalili mbele ya mweupe; na pia kwamba si binadamu kamili bali myama tu…hivyo Jesse Owen alimshinda Hitler katika mashindano hayo mjini Berlin , miaka 70 iliyopita. Hitler aliyekuwa Mgeni wa heshima wa mashindano ya Olimpiki mwaka 1936, aliondoka uwanjani,hakutaka kuona ‘mnyama’ akishinda mbio dhidi ya binadamu,yaani Mtu Mweupe!
 
Ni uwanja huo huo ulioboreshwa, ambako mshindi wa mechi ya 61 alikuja kupambana na mshindi wa mechi ya 62 katika mechi  ya mwisho(ya 64); ya mashindano ya Kombe la Dunia mwaka 2006 huko Berlin.
 Matarajio ya weusi wengi Duniani yakiwa kuona timu kutoka taifa moja liwe la Ulaya, Amerika ya Kusini, au Asia, kama siyo kutoka Afrika, lakini lenye weusi wengi; likiibuka mshindi wa kombe hilo la fahari; ili kukata ngebe za masalia ya wabaguzi wa rangi wa Ujerumani, kama alivyofanya Jesse Owens,MWAKA 1936.
 
Kama ushindi wa shujaa huyo aliyemshinda Hitler na wazungu wake akiwa ‘kifua wazi’ katika uwanja huo wa Berlin ; matokeo yake yangekuwa ukombozi wa mtu mweusi dhidi ya kudharauliwa, kubaguliwa na kuonywa taka mbele ya wazungu; shime watu weusi waushinde ulimwengu wa wabaguzi mafashisti kama Adolf Hitler!
 
Kutokana na ushindi wa Kaka Jesse Owens,mwaka 1936, mwaka 1976 alikuja kutuzwa medali ya Rais, ya Uhuru  (Presidential Medal of Freedom)na Rais Gerald Ford wa Marekani; akatuzwa tena medali ya Dhahabu ya Congess (Congressional Gold Medal) na rais mwingine wa nchi hiyo, George Herbert Walker Bush (Bush Baba),  mnamo Machi 28, mwaka 1990; yaani miaka 10 baada ya kifo chake.
 
Mwaka 1984 mtaa mmoja wa Berlin ukapewa jina la Jesse Owens kwa heshima yake.
Owens alikufa akiwa na miaka 66 mjini Tucson , Arizona kwa ugonjwa wa Kansa ya mapafu, kufuatia uvutaji wa sigara uliokubuhu, wa pakiti moja kwa siku.
 
Hakika, ushindi wa Kaka Owens wa majira ya joto ya mwaka 1936, majeshi ya Nazi Yalipokuwa yakijiandaa kwa vita ya Pili ya Dunia, katika uwanja uleule lipochezwa fainali ya Kombe la Dunia,  kati ya Italia na Ufaransa,mwaka 2006, ni alama ya mapambano dhidi ya ubaguzi na dharau za weupe dhidi ya mtu mweusi anayeishi katika mabara yote.
 
.Uwanja huo ulijengwa mwaka 1936 kwa ajili ya mashindano hayo ya Olimpiki; bado ni kielelezo cha kuzikwa ubaguzi na udhalilishaji wa weusi kama ule wa enzi ya Hitler.
Shime weusi washinde Kombe la Dunia huko Brazil mwaka 2014.
Katika fainali hiyo, Ufaransa ilifungwa na Italia,ikajakusemwa kwamba Ufaransa ilifungwa kwa sababu iliwaweka Weusi wengi kwenye kikosi-Weusi eti waliitia mkosi Ufaransa!
 
Timu zote za Afrika zijapofungwa na kufungishwa virago katika raundi ya awali huko Brazil,bado Afrika itashangilia timu ya kutoka Bara lolote linalojali utu,na timu itakayojumuisha wachezaji Weusi.
 
Moja wapo ya timu hizo ni Ufaransa, Uswisi na Uingereza, ukiwaacha kaka zetu wa Brazil, Saudi Arabia, Ecuador, Costa Rica, Trinidad na Tobago n.k.
Shime timu zinazojumuisha weusi ziibuke washindi nchini Brazil mwaka 2014, baada ya aibu ya Zenedine Zidabe Zizou,kutukanwa matusi ya kibaguzi huko Berlin mwaka 2006 na ndiko  liliko chimbuko la ubaguzi wa rangi wa tangu enzi za akina Dikteta Hitler, ili ukombozi kamili katika nyanja zote upatikane.
 
Natambua  na nijajivcunia mchango wa weusi katika nyanja nyingine kama masumbwi na siasa: Wapo akina Mohamed Ali , Leon Spinks, Evander Holyfield, Mike Iron Tyson, Caster Semenya, na mabingwa wengine weusi waliowahi kuushinda ulimwengu wa ubaguzi; kama Martin Luther King Jr. Kaka Andrew Jackson Young nk.
 
Bila kujali mipaka ya nchi za ulimwengu,Kombe la Dunia linalochezwa katika viwanja vya Brazil  safari hii, lazima mtu mweusi audhihirishie ulimwengu kwa mara nyingine, kwamba ni binadamu kamili mwenye uwezo na akili timamu; na kamwe si dhalili au hayawani, kama alivyodhani Hitler.
 
Mashindano ya Kombe la Dunia ni zaidi ya kutafuta heshima katika nyanya moja ya michezo, bali hata kisiasa, kiuchumi,kijamii, kiteknolojia n.k.
Kwangu mimi, naam mtu mweusi mmoja anapopiga mkwaju unaoingia kimiani, na kumwacha mlinda mlango, Mzungu, akigaa-gaa sakafuni,ni ushindi pia kisiasa na kiuchumi, maarifa, ufundi, uwezo ,akili nyingi na kila kitu, kuwazidi wazungu!
 
Weupe walidhani ni  bora kuliko weusi.Akina Hitler wa Ujerumani, Dk. Balthazar Johannes Voster wa Afrika Kusini, akina Ian Smith wa Rhodesia ya zamani sasa Zimbabwe na wengineo, walijiona wao watu sisi nyani.
 
Popote alipo mtu mweusi katika mataifa yote  yanayoshiriki kombe hilo la Dunia nchini Brazil,mwaka 2014 ; shime ashangiliwe na kutiwa moyo kwa kazi kubwa ya kuushinda ubaguzi wa rangi..chenga moja ya mweusi dhidi ya mweupe ni ishara ya maarifa na uwezo.
Kwamba, mtu mweusi ni bora kama alivyo mweupe;ni makini, ni ghali; na kwamba siku si nyingi weusi watautawala ulimwengu katika nyanja zoote kama wanavyotawala sasa katika dimba katika timu nyingi na hususan katika ligi za Ulaya,kama Uingereza.
 
Kama nilivyokwisha sema,  Afrika inayatazama mashindano hayo  ya Kombe la Dunia, ama Olimpiki, kama maandamano makubwa ya Dunia ya kupinga ubaguzi wa rangi(Anti-racist Demonstration).
Hata Afrika ilipoondolewa baada ya mechi ya Ufaransa na Togo, Ijumaa, Juni 23,  mwaka 2006 weusi tulio wengi katika mabara yote tuliwashangilia weusi wenzetu waliosalia katika kinyang’anyiro cha timu 16 kutafuta nane zilizoingia robo fainali mwaka 2006 huko Berlin.
 
Ni kwa sababu hii, Fikra Pevu hupata taabu sana kushabikia timu ya weupe; hata kama inatoka Afrika, inapocheza na timu ya taifa lenye weusi wengi hata kama ni Ufaransa, Saudi Arabia, Brazil ,Ecuador, Costa Rica, Trinidad na Tobago na nyingine!
 
Ni kwa sababu hii, Fikra Pevu zinawaona wachezaji kama Paulo Wanchope wa Costa Rica, Sol Campbell wa Uingereza, Eric Abidal, Claud Makelele, Zenedine Zidane, Thierry Henry, Gallas, Louis Saha,na wengineo wa Ufaransa na akina Patrick Mueller wa Uswisi, akina Ronaldo, Gaucho, Cafu na Wabrazili wot, na wengine woote waliochipukia kama mabalozi wa mtu mweusi katika mashindano hayo yanayoufundisha ulimwngu kwamba mtu mweusi siyo mnyama, kama alivyosema Hitler.
 
Kusema hivi si kuendeleza ubaguzi wa rangi, ni kuwaenzi wote waliopinga ubaguzi. Kama akina Nelson Mandela, Martin Luther King Jr,Jesse Owens, Askofu Abel Muzorewa ,Desmond Tutu n.k.
 
 Hata sasa mabalozi wetu wengine kama Samuel Eto’o Fils wangali wakizomewa na wabaguzi wengine wa Hispania na kwingineko Ulaya na Asia; na kufananishwa na manyani!.
 
 uwanja wa Olimpiki wa Berlin ungegeuka shimo la kuuzika ubaguzi wa rangi,lakini Marco Materazzi akaongeza kidonda kwa kumtukana Zidane,mwenye asili ya Tunisia matusi ya kibaguzi,, hata kuzidi alivyofanya Kaka Jesse Owens dhidi ya Dikteta Hitler!
Mtu mweusi atatazamwa kama chimbuko la maarifa, tija, mafanikio katika kila jambo na hata ishara ya kiongozi na mshindaji wa kila kitu; amini usiamini.
Wapo weusi walioathiriwa na kasumba ya kikoloni,hata hawajithamini,wanamwona Mzungu kuwa ndiye mtu.Alifika Afrika,mzungu huhudumiwa haraka kwa kutetemeka,Mweusi anaachwa akafie koridoni.
 
Natambua watu weusi walivyouzwa katika mabara mengine kama rasilimali watu.
Kwa hali hiyo, sitaacha kuwashangilia weusi katika harakati hizi Ujerumani hata kama watapambana na weupe wa Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara , acha Kasikazini!
 
Afrika ,siyo tena mahali penye vita, majanga, magonjwa, njaa na machafuko kama Somali, Darfur n.k ni mahali sasa pa maendeleo makubwa tangu katika soka, uchumi, riadha, ngumi, siasa na kila kitu kuzidi ulimwengu wa wazungu…kinachotuponza ni kudhani wazungu ni bora kwa kila kitu!
Nawashangaa waandishi wa habari wanaowakilisha mashirika ya Magharibi,wanadhani vita,ukimwi na wakimbizi na njaa ndiyo habari.        Kumbe ipo miradi tele ya maendeleo haitangazwi,na tumebaki ku copy na ku paste  habari za akina mke wa Prince William kulazwa hospitalini kwa kichefuchefu cha himila changa!
Badala ya Muafrika kuandika kwamba Prince William mkewe ni mvivu tu,sisi huko mama mwenye himila changa, hata awe na kichefuchefu bado huchapa kazi kama kawaida,tunatangaza kulazwa hospitalini kwa vichefuchefu vya mimba za wazungu,Shameful!
itaendelea
 
Shime watu weusi, wembe ni uleule wa Jesse Owens dhidi ya Hitler!!
Mwandishi anapatikana katika  www.congesmrambatoday.blogspot.com
0713 324 074
 
 
 

No comments:

Post a Comment