Tuesday, December 11, 2012

HAKI ZA BINADAMU UINGEREZA NA MAREKANI?

Jumanne usiku, Desemba 4,mwaka huu, wakati nilipokuwa nikitazama kipindi cha televisheni ya BBC kiitwacho DIRA YA DUNIA,nikaona Salim Kikeke akisoma 'twitter' za jamaa wa TANZANIA waliohoji kwamba habari za mke wa Prince William sasa kuwa na ujauzito wa majuma 12, ziliwahusu nini Waafrika?
Habari za mke wa mrithi wa ufalme wa Uingereza kupata himila changa na kulazwa hozpitalini kwa kichefuchefu, akaanza  kutangaziwa Mwafrika,utadhani zingempa kushiba!
Naam,hii ndiyo AJENDA YA SIRI ya vyombo vyao vya habari,ili kutulisha kila upuuzi wa akina malkia na wajukuu zake,utadhani Afrika haina cha kujifunza kutoka hapa barani. 
UINGEREZA, ambayo ilifanikiwa kuzikusanya nchi nyingi zilizokuwa chini ya Utawala wa Rumi, na kuzifanya  makaoloni yake, imekuwa ikitawaliwa na wafalme tangu mwaka 829 A.D.
   Hawa wafalme, na dada zao na mabinti zao(malkia) wamewatawala Waingereza tangu karne ya tisa AD. Hakuna anayeandamana, sisi tunahamasishwa maandamano na kuaana utadhani wendawazimu!
 Hadi leo, na hakuna raia aliyekwisha andamana kutaka utawala wa kifalme na kisultani uliodumu zaidi mya miaka 1,182 ung’olewe,ili kupisha demokrasia.
 Nchi hii, inayoongoza kuata kumpindua Kiongozi wa Libya, Kanali Muammar al-Gaddafi, kwamba amedumu uongozini tangu mwaka 1949(umri wa miaka 42) imetawaliwa na wafalme lukuki,tangu Egbert na zama za Saxons na Danes.
  Mwaka 1399,Uingereza ilikuwa chini ya House of Lancaster, wakitawaliwa na Wafalme  na Duke of Lancaster,hadi miaka ya 1900  wakawa chini ya Mfalme GeorgeV,Edward VIII, George VI baadaye akatawazwa Malkia Elizabeth II, ambaye ni BINTI mkubwa wa GeorgeVI.
 Huyu Malkia Elizabeth II alitawazwa kuwa Malkia wa Uingereza Feburuari 6,mwaka 1952 hadi leo anatawala Uingereza, na hakuna wa kuhoji mamlaka yake yaliyotamalaki hata hapa kwetu Tanzania.
   Serikali ya Uingereza inayoongozwa na Mawaziri wakuu,ilianzishwa ,mwaka 1721( karne tisa baada ya Mfalme wa kwanza, Egbert; wakati huo akaanza kutawala Waziri Mkuu,  Sir Robert Walpole.
 Sir, ni cheo anachopewa mtu anayeheshimiwa sana na Familia ya kifalme.Cheo hiki, “Knighthood” ametunukiwa hata Salman Rushdie. Sir Salman Rushdie alipigwa ‘Fatwa’ na utawala wa Ayatollah Khomeini,huko Iran,hivyo hutafutwa sana auawe kwa kuikashifu dini ya Kiislam. Niachane na hayo; hayanihusu.
  Kutoka Sir Robert Walpole, hadi sasa David Cameron, Uingereza yapata mawaziri wakuu takriban 80 vya vyama anuwai, ambavyo aslani haviwezi kuhoji bungeni mamlaka ya Malkia. Malkia Elizabeth II ANA UMRI WA MIAKA 84, alizaliwa Aprili 21 mwaka 1926.
 Akifa leo, ingawa ametawala Uingereza kwa jumla ya miaka 59, atatawala mwanaye,Prince Charles, ama wajukuu zake, Prince William na Harry, hao ambao wake zao wakiwa na himila changa,tunatangaziwa dunia nzima!
Wakiwa hedhi,wakilazwa hospitalini eti kwa kichefuchefu,sisi tunatangaziwa upuuzi ule, wakati wake zetu nao wanapata kichefuchefu na kuendelea na hamsini zao tu,na siyo issue!
Novemba 2008, Malkia na mumewe,Prince Phillip, walikuja Kampala,Uganda kuburuza mataifa lukuki hapa duniani, katika mkutano wa makoloni yao ya zamani, wao wanaita Jumuiya ya Madola, The Commonwealth.
 Hata Ufaransa imetawaliwa na akina Charlegne,au Charles Mkuu(742-614 AD) hadi wakati wa Jamhuri ya Tano zama za Rais Charles Andre J.M. de Gaulle(soma Chalz de Go)aliyeishi 1890-1070.                           Ni wakati wa akina Georges Pompidou,Valery Giscard d’ Estaing, Francois Mitterand,Jacqius Chirac hadi huyu “Mzee wa Vimwana” Nicolas Sarkozy.
 Nataka kusema kwamba, hizi dola kuu zilitoka mbali,kwenye tawala za kifalme,hadi leo kinachoitwa demokrasia halisi hakuna.
 Isipokuwa, wao wanataka wafalme wa Afrika(Gaddafi anaitwa , ‘King of Afrcan Kings’) watokomezwe.
Ili, akina Malkia na wajukuu zake Harry na Prince William wabaki wakitutawala huku,kwenye Commonwealth.
  Malkia huyu, bado anaburuza mataifa mengi tu kama Canada, Austria, New Zealand,Jamaica,Barbados, Bahamas kwa kuyataja machache.
 Tena, Marekani ndiko walikoiba kura katika uchaguzi wa mwaka 2000 pale Al Gore alikaribia kushinda, wakamwibia kura. Mashabiki wake na chama chake cha Democrat walikuwa wataarabu tu,ingekuwa kwetu huku,ingekuwa kama Cote d’ Ivoire.
Hata mwaka huu Democratic walishaanza kuiba kura,wakastuka.Ukimpigia Obama,kura zilikwenda kwa Romney,hukusikia?
 Dola iliyodumu kwa jumla ya miaka 235 wakahesabu kura kwa mashine kisha kwa mikono, wakamnyang’anya kura AlGore, wakampa Bush. Kesi ikaenda mahakamani, mahakama ikachakachua matokeo na kumpa Bush mhula wa kwanza wa utawala.
  Tunajua kura za Palm Beach na Miami-Dude zilileta shida, mwezi mzima ukapita bila kujulikana mshindi. Algore alipata kura za watu wote51,000,894wakati Bush alipata 50,495,211 akaongoza Florida na kujipatia kura za ushindi za electoral 271.
  Nataka kuwagutua wanaoshabikia Uingereza,Marekani,UfaransamUjerumani n.k kwamba kuna demokrasia pevu,kuna uhuru na haki za binadamu(zipi?) wanazofanya hapa duniani?
Mwaka 1936, Uwanja wa Olimpiki wa Berlin ulijengwa na Dikteta Adolf Hitler. Michezo ya Olimpiki ilifanywa hapo Berlun, na Hitler akawa mgeni wa heshima.
 Julai 9 mwaka 1936 Mwamerika Mweusi, Jesse Owens  akawatioa kamasi Wazungu wote kwenye mbio na riadha. Akajipatia nishani nne za dhahabu kwa muda wa dakika 45 tu. Hitler akakasirika kuona Mweusi akishinda kila mara, wakati Wazungu hawakumwona. Yeye alijua mtu mweusi ni mnyama, kwahiyo akasusia mashindano ya Olimpiki kwa sababu mnyama, Owen, salishinda!
Miaka 70 baadaye, mwaka 2006,uwanja huohuo wa Olimpiki wa Berlin,ndiko fainali za Kombe la Dunia zilikofanyika, Michael Materazzi wa Italia akamtukana Zenedine Zidane Zizou,matusi ya kibaguzi.
Chukua tabia hii ya akina Hitler na Materazzi halafu uchanganye na ubaguzi wa rangi huko Afrika ya Kusini zama za Makaburu.
  Angalia, ubaguzi wa rangi dhidi ya akina Samuel  Eto’o Fills wanaoitwa nyani, ama kawaulize akina Eric Abidal Claud Makelele,Zidane, Thiery Henry, William Gallas,Louis Saha,Patrick Vieira na wenzao waliposhindwa kuipa Ufaransa ubingwa, ilisemwa kwamba ni rangi yao Nyeusi ya mkosi!
 Hapa, msomaji, unaona haki gani za binadamu huko Ulaya?Agosti 2009 huko  Berlin,Ujerumani, Caster Semenya(19) wa Afrika Kusini akawatoa kamasi Wazungu katika mbio za mita 800, wakamnyima ushindi, kwa madai kuwa yeye ni ‘Dume-Jike,’ Wazungu bwana!
 Kwa Muingereza, eti neno uhuru ni mzaha linapofika kwa Mwafrika. Mwaka 1787 mji Mkuu wa Sierra Leone, Freetown(MJI ULIO HURU)ulijengwa na Muingereza huyu kama kituo huru cha watumwa! Watumwa walijengewa mji huru wa Freetown?! Ajabu.
KIFO CHA DIANA AIBU TUPU
Kifo cha Princess Diana mwaka 1997,na kuundwa kwa tume ya uchunguzi wa kifo chake, The Paget Probe, ni kielelezo kwamba Uingereza hakuna uhuru,hakuna demokrasia na haki za binadamu. Kuna ubaguzi wa rangi na ukaburu uliotamalaki.
Princess Diana(36) na Dodi al Fayed(42) walikufa Agosti 31 mwaka 1997 katika Ponto de I’Alma Park,mjini Paris, Ufaransa, mahali penye njia ya chini kwa chini.
 Ilikuficha tetesi kwamba ‘wivu’ wa Malkia na familia yake dhidi ya Diana aliyekuwa amevuka mipaka na kutaka kuolewa na Mwarabu, Dodi, na ikasemekana alikuwa na himila changa ya miezi miwili, ndicho kitu kilichomsababishia mauti ya tashtiti.
  Vyombo vya usalama mjini Paris, baada ya ajali yakupangwa, vikamsingizia dereva,Henri Paul kwamba aliendesha gari kwa kasi sana, ili kuwatoroka ma-Paparazzi.
Kwamba, Dodi na Diana waliutia mtindi kwa sana, hawakufunga mikanda wakati Mercedes Benz S-280 SEDAN, ilipogonga nguzo ya 13 hapo barabara ya chini na kusababisha vifo vya Diana na Dodi!
   Maneno yalipokuwa mengi, ikaundwa tume ya kuchunguza vifo hivi, Paget Probe iliyokuwa na wapelelezi 15 kutoka Scotland Yard, wakatumia Dola za Marekani 7,000,000 kuwahoji mashuhuda 300.
 Hata hivyo,Mkuu wa Paget Probe, zamani alikuwa Mkuu wa Scotland Yard, Lord John Stevens alishia kukaa ‘kama kamati’ na watoto wa Diana, Harry na William na kakaye,Lord Charles Spencer na dadaze wawili, wakasema haikuwa ajali ya kupangwa.ilikuwa ajali ya kibinadamu-tragic accident!
 Ripoti ya uchunguzi yenye jumla ya kurasa 832 haikuwa na jipya. Baba wa Dodi, Bilionea wa Kimisri, Mohammed al-Fayed akaipinga vikali tume hiyo, na kusema hadharani kwamba majasusi wa Uingereza waliwaua Dodi na Diana kwa sababu ya wivu,kuona Daiana angeolewa na Dodi.
  Diana na Prince Charles walishatengana  tangu Desenba 9 mwaka 1992 wakapeana talaka rasmi Agosti 28 mwaka 1996.
Prince Charles alishaoa kimwana mwingine, Camilla Parker Bowless, lakini Diana alifungwa kuolewa na mtu kwa sababu alikuwa wa familia ya ufalme!
 Mtu wa ‘Royal Family’ kama yeye hakuruhusiwa kuolewa na mtu,tena Muislam, sasa sijui kama kweli alikuwa na mimba, sasa kama Diana  angezaa Mwarabu, anaye angekuwa anakuja Makao Makuu ya Malkia-Buckingham Palace, kuwasalimia nduguze, Harry na Prince William?
Waingereza, walimuua Diana na Dodi,ili kutupilia mbali udhia na aibu ya warithi wa Ufalme kuwa na ndugu Mwarabu halafu Muislam.
 Si unajua dini ya Anglikana ndiyo dini yao na Malkia ndiye mkuu wa dini hii ya Uingereza? Sasa, hawakutaka Mwarabu azae na mke wa mwana wa Malkia, sasa tunajua Diana aliuawa kwa sababu ‘aliasi’ na kutaka kuolewa na Dodi na alikwisha kuwa na mimba changa ya miezi miwili,ikaleta taabu.
 Unaweza kumuuliza Mohammed al Fayed, Yule tajiri wa Kimisri, babaye Dodi,kama nasema uongo kwamba Diana aliuawa na majasusi wa Uingereza huko Paris.
 Ndiyo maana tunasema Uingereza hakuna demokrasia,uhuru wala Haki za Binadamu. Labda uhuru uko kwa mashoga kuvua nguo na kuandamana hadi bungeni wakiwa uchi, kuna uhuru wa wanaume kuoa na kuolewa kama Sir Elton John na David Furnish.
 Kuna uhuru wa maaskofu na wachungaji wa dini ya Malkia kuoana wanaume na wanawake, na wanaweza kwenda baa na vimwana na kuuchapa mtindi, halafu waumini wanapoandamana kupinga wazinzi kuwa wachungaji, maaskofu wanawatetea!
 Huu ndiyo uhuru ulioko Uingereza,Marekani na Ufaransa..uhuru wa kumomonyoa maadili na sheria za Bwana Mungu. Uhuru wa kutwambia hata habari za mama mjamzito na hata anapokuwa hedhi!
itaendelea
            0786/0754-324 074
 
 
 


No comments:

Post a Comment